KUTOKA BUNGENI: Tanzania kuuza tani milioni 2 za mihogo China

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Serikali imepata soko nchini China, kupeleka tani milioni 2 za mihogo zenye thamani ya Dola 300 milioni za Marekani.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masalla (CCM).

Masalla alitaka kufahamu jitihada za Serikali katika kuwatafutia wakulima nchini masoko ya mazao yao.
Akijibu swali hilo, Mwijage alisema mbunge huyo amewahisha masuala ya bajeti ijayo na kwamba, Serikali tayari imepata soko la mihogo nchini China.

Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Hamida Mohamed Abdallah (CCM) alitaka kujua Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda ya Mwaka 1996-2020, jinsi inayolenga kuvifanya viwanda vya usindikaji mazao kuongeza thamani na kukuza uchumi.
 
Hawa watu wanachekesha; unatafuta soko wakati hata wakulima wadogo wanakosa mbegu ya mhogo;
Tuuze kwa wachina ili wakatengeneze POP na chaki watuuzie kwa dollar;
fufueni viwanda vyetu ili tuzalishe bidhaa zetu kwa kutumia mazao yetu;
 
Hawa watu wanachekesha; unatafuta soko wakati hata wakulima wadogo wanakosa mbegu ya mhogo;
Tuuze kwa wachina ili wakatengeneze POP na chaki watuuzie kwa dollar;
fufueni viwanda vyetu ili tuzalishe bidhaa zetu kwa kutumia mazao yetu;
Mamndenyi siku zote unakuwa na mawazo kama yangu sema unaniwahi kupost, nakupenda Bure,
 
Maeneo kama Mbinga, Songea,Iringa walikuwa walimaji wazuri wa mihogo lakini kimya sasa mihogo inaanza kuhadimika hebu tilieni mkazo hiki kilimo hats kwa kuwabubulia mbegu wananchi kisha fufueni viwanda haraka ndiyo raw materials hizo tupange bei wenyewe
 
Nanukuu maelezo ya Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Bw. Uledi Mussa
'Kama wakulima watafuata viwango vilivyowekwa katika kulima na kutayarisha mihogo vizuri, wanaweza kuuza nje ya nchi ambako ongezeko la mahitaji linakuwa kila siku' Mwisho wa kunukuu

Nafikiri watendaji wajipange hata wanapokuwa wanaojiwa na waandishi wa habari wafikirie maelezo ya kuwapa wananchi, maneno ( kama & wanaweza) hayafai, kinachotakiwa ni kutoa elimu/taarifa sahihi na kwa wakati kwa wakulima, mfano ni aina hipi ya mbegu inafaa kulimwa kwa ajili ya kulenga soko la China, kilimoc cha kisasa ambacho kitakuwa na mavuno yenye tija katika hekali moja, na pia ni sehemu nyingi muhogo unamea sasa ni jukumu la wizara kushirikiana na afisa kilimo, watendaji kata, vijiji, etc kutoa elimu ya kilimo chenye tija ili kufanikisha hizo tani zinazohitajika katika soko la China na kupunguza maneno ya 'kama' & 'wanaweza'
 
Back
Top Bottom