KUTOKA BUNGENI: Rais Magufuli kuhamia Dodoma rasmi mwaka 2020

2020 atahama wakati anakuja Rais mwingine na serikali nyingi?? Lambda anahamia yeye na family yake kama Rais mstaafu hapo sawa
 
Kwa hiyo mpakaka 2020 viongozi wa serekali watendelea kutumia fedha za walipa kodi kwenda DSM kumfuata Rais.
 
Mtani ukitaka nifunge tu
Bhana
Ila kuhamia Dodoma si sawa na kuhamisha ng'ombe za bibi yako zile za kinyankole
 
Rais wangu ana machare kawatanguliza wenzake wakapime kina,kina kikiwa kirefu haendi DOM na waliotumwa kupima kina watarudisha majembe DSM.
 
Ni kweli kabisa,
hili linatekelezeka, lakini washukuriwe wananchi pia waliopiga kelele kuwaamsha washika vibendera wanaoamua mambo bila ya kutafakari.
waziri mkuu aliishi Dodoma miaka mingi tu, hata Pinda alikuwa mkazi halizi wa Dom. Lowasa alianza kujenga nyumba ya waziri mkuu na majaliwa anaimalizia. Yeye kuhamia sasa hamna tatizo kwa kuwa nyumba yake imeshakamilika.
Hayuko fair kwa kuwataka mawaziri na makatibu wakuu wa wizara nyingine wafanye hivyo sasa, kama alivyofanya kwake kwa kuamua kuhamia baada ya nyumba kukamilika alipaswa amalize nyumba za mawaziri kwanza.
Tungemsaidia kufikiri katika hili.
kuna wizara zilizokuwa zimeshafika Dodoma, zinapaswa zifanye hivyo. so phase one iwe kuhamisha rasmi wizara zote zilizokuwa zina ofisi kamili Dodoma, lakini hawa wapewe muda wa mwaka mzima kuhamishana. ukigawa wizara na idara, utaongeza gharama Zaidi ktk utendaji. hakuna idara itakayoweza ku-operate bila ya signatories, hapa tunamsema katibu mkuu, kwa hiyo trip za Dar - Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha proposal, halafu wakaipitie kama idara then waje kupitisha pesa kwa katibu mkuu, hii haiko cost effective.
kweli wahame kwa phases, lkn ziwe wizara na sio mawaziri na makatibu. or else waende mawaziri na manaibu tu, wawaache makatibu wakuu, wakurugenzi na wakuu wa idara. siku zote katibu mkuu ahame na group kubwa ili wizara ziendelee kufanya kazi.
Umetoa ushauri sahihi katibu Mkuu ahame na kundi kubwa
 
Ambao mnaonana nae mkumbusheni kua jengo letu pale Magogoni asiondoke na kitu maana 2020 anakuja mwenzake ambae habari ya Dodoma hana ili tuondoe usumbufu wa kurudisha vitu.
 
Serikali ya kisanii hii. Mwigulu alituaminisha kwamba wizara yake ingehamia Dodoma ifikapo mwezi August 2016, lakini hadi leo bado yeye na watendaji wake wanaendelea kupigwa na joto hapa hapa Dar.
 
Kwani Jenister Mhagama na waziri mkuu bado hawajahamia Dodoma?

Ndiyo imetoka hivyo., na sasa imebaki story.
Kilichonipa faraja bi kwamba maoni ya JamiiForums yamefanyiwa kazi...kile kilichosomwa leo bungeni na Majaliwa ni kazi kubwa iliyofanywa na wanachama wa JF
Huu ni ukweli na sio kujikweza atakayebisha amuombe moderator azilink zile post zote hapa tulizoandika
 
Hotuba ya waziri mkuu imenionyesha kua kweli serikali imeanza kufanya kazi. Hongera sana serikali ya JPM
 
Tulidhihakiwa sana tuliposema kuwa haiwezekani kabisa kuhamia Dodoma kwa kukurupuka
Daima uongo hupanda lifti bali ukweli hukwea ngazi
Mkuu,kina watu wanapenda kujiona wao wana akili zaidi kuliko wengine.sasa wanaumbukaaa,mizuka haitakuja lisaidia taifa hili hata kidogo
 
Tumtizame yeye PM kwanza maana alisema yeye atahamia baada ya vikao vya bunge kumalizika,Je atakwenda?
Kuhamia Dodoma sio tamko la kukataza mikutano na vikao vya kisiasa nchini ila kama yanafanana matukio haya,ebu tazama
Mikutano ya vyama vya siasa mpaka 2020 na mtoa tamko atahamia DOM 2020,kuna nini hapa?
 
Back
Top Bottom