Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Kuna majitu hayana akili duniani yaani ,jitu limeshaingia kwenye kumi na nane za mabeberu lakini halielewi linajiingiza mpaka kwenye sita kwa sita .Subiri mabeberu waanze kuvuta mpini maana limeshika Makali hata halijielewi .
 
Kuna dikteta zaidi ya yule alienyofowa kipengele cha ukomo wa uongozi na akaweka kipya hakuna mwanachama kwenda mahakamani kuhoji ukihoji unafukuzwa chama!
Haya mambo yako ccm, nakumbuka Sofia Simba alifukuzwa, lakini wakamuacha Emanuel Nchimbi na Kimbisa. Alisema kila kiongozi cheo kimoja yeye ana viwili. Akiambiwa aachie kimoja hataki eti nchi haitatawalika. Anawatishia wabunge wasifanye kampeni za urais atawafukuza kwenye chama, sasa mbaya hata kuihoji serikali ambalo ndilo jukumu la wabunge limepigwa marufuku ccm, Kina nape waliambiwa watch out, yule dada wa kamati ya budjet akaachia uwenyekiti. Chezea HIV lakini siyo CCM.
 
Uzoefu unaonyesha kuwa endapo jambo lolote likienda kujadiliwa bungeni na ukaona wa bunge wa CCM wanaliungana mkono japo kwa hoja dhaifu na hoja za msingi zikawa zinatolewa na wabunge wa vyama vya upinzani na jambo hilo likapitishwa; majibu yake ni kwamba jambo hilo halina tija na maslahi mapana kwa watanzania walio wengi, ni mwendelezo wa dharau kwenye jukwaa la kimataifa, kwa maana nyingine halina tija kwa taifa letu zaidi wanaonufaika ni watanzania wachache na wageni.

Hii ina maana kuwa, CCM, wabunge wake, na viongozi wake pia hawana nia nzuri na nchi hii na ndiyo maana tangu tumepata uhuru hadi hivi sasa bado tuko kwenye kundi la nchi masikini LDCs wakati jirani zetu Kenya na Rwanda wamekwisha toka huko kitambo na sisi pamoja na rasilimali nyingi tulizonazo bado hazitusaidii tu; ni aibu kweli kweli, budget ya nchi hadi hivi sasa bado ni tegemezi.

Bado hadi muswada kama huu wenye mapungufu kibaoooo tena ya msingi halafu umepitishwa!! Yaani hawa jamaa ni hovyo kabisa sijapata ona katika dunia hii ya sasa.
 
wabunge mnaopitisha kila mswada bila kuona mbeleni, mkae mkijua hamtokua wabunge milele! utafika muda tu mtakuwa raia wa kawaida.
 
Back
Top Bottom