Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

Yaani hata ukisikia sifa siyo hizi.
1.Unajiuliza huyu jamaa kasoma au ndiyo kajitoa ufahamu.Maana wasomi huongea Kwa takwimu Na utafiti
2.Hayo anayosema ndiyo mwono Na mtazamo wa chama chake au mawazo binafsi?Angetafakari Kwanza kabla hajaaibisha chama
3.Alisoma vema katiba kweli au anatoa maoni yake
4Hata kama Ni kutafuta Huruma apewe uwaziri tena,ajitfakari kilichomtoa
 
Sisi sio China. Na hatukutaka na hatutaki kuwa China. Ndio maana hakuna wananchi waliofungua kesi wakipinga uwepo wa hivi vyama tangu kuanzishwa. Jamii ya Tanzania inataka vitu simple sana' elimu, Maji, umeme, chakula, Malazi,njia ya kipato na Afya. Hata miji yetu isipokuwa na ghorofa hata moja vikawepo hivyo tutakuwa na furaha kuliko nchi yoyote Ile iliyo endelea.
 
1548963990560.png

ASASI isiyo ya kiraia ya Alliance For Democratic Organization (ADO) imewapongeza wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa huku ikiwataka baadhi ya wanasiasa kutoka vyama vya upinzani kuheshimu maamuzi hayo. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi wa asasi hiyo Habib Mchange, alisema kupitishwa kwa Muswada huo ni hatua kubwa kwa siasa za Tanzania na zaidi wanachama wa vyama hivyo na wananchi kwa ujumla.

Alisema anaamini hatua hiyo italeta mabadiliko makubwa na hasa katika kuweka uwazi na uwajibikaji katika uendeshaji wa vyama vya siasa na kuondoa kila aina ya ubabaishaji aliodai umekithiri ndani ya siasa za Tanzania tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi. “Kwa dhati kabisa niwapongeze wabunge wote waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha muswada huu unapita ili uweze kuleta mabadiliko ya kweli katika siasa za Tanzania tukiamini kuwa sote lengo letu ni moja kuijenga nchi hii,” alisema Mchange. Aidha alisema endapo Muswada huo utasainiwa na Rais na kuwa sheria, mapendekezo yake kwa serikali ni kwamba isiishie kubadili vipengele vilivyomo ndani, bali inapaswa iende mbali na kuwachukulia hatua watu wote watakaokwenda kinyume na sheria husika.
 
View attachment 1009987

Ha ha ha ha ha ha ha matapeli hawaishi mjini!
How, tapeli ni nani. Habibu si yule wa CCM. NGO hii kaianzisha lini?
 
Si waseme tuu kuwa ccm imelipongeza bunge kwa kuuwa demokrasia nchini!
 
Yes tumefika pazuri Tanzania yenye maendeleo itakuja bila kelele nyingi. Asante Bunge la Matonya.
 
Kuna 'Wapinga Ufisadi ' wamechukia Sana kuja kwa Sheria Hii Mpya itakayodhibiti Vyama vya Siasa kugeuzwa Vitalu vya kurthishana Uenyekiti Mtu Na Mkwewe
 
Hatuwezi msaidia habiba kutafuta cheo,hatunamda wa kubishana nae!! Bora akalime siasa hawezi
 
Back
Top Bottom