Kutoka Bungeni: Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa wapitishwa kuwa Sheria

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Spika Ndugai ameipongeza Serikali kwa kazi nzuri na Muswada umepita kwa kura za Ndiyo



======
BAADHI YA NUKUU (KUTOKA UPINZANI)

Kambi ya rasmi ya upinzani bungeni imekosoa muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa wa mwaka 2018 ikisema ni uonevu mkubwa dhidi ya vyama hivyo.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo bungeni leo, msemaji wa kambi hiyo, Ester Bulaya amesema wabunge wana uwezo mkubwa wa kuzuia uonevu huo ikiwa watapenda kufanya hivyo.

Bulaya ametoa mfano wa vifungu vinavyoonea katika muswada huo kuwa ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kuingilia mfumo wa uchaguzi ndani ya chama akisema kutapunguza uhuru wa vyama kufanya chaguzi bila mashinikizo kutoka ofisi ya msajili.

Kingine amekitaja ni kinachotoa masharti ya namna ya utoaji wa elimu ya uraia kuwa masharti hayakutilia maanani kuwa vyama vya siasa vina mahusiano ya kiitikadi na vyama rafiki toka nje ya nchi.

“Ni haki yao ya msingi ya kueneza itikadi za vyama vyao bila kujali mipaka ya nchi…huu ni upungufu mkubwa kwani msajili anaweza kukataa tu kutokana na maslahi yake bila kuongozwa na sheria inayopendekezwa,” amesema.

Halima Mdee:

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amesema baadhi ya vipengele vya muswada wa marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018 vinavunja Katiba.

Akichangia muswada huo bungeni leo, Mdee amesema miongoni mwa kinachovunja Katiba ni kile kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kukifuta chama ambacho kitashindwa kuwa na kumbukumbu za wanachama wake.

“Muswada huu unataka vyama vya siasa viweke rejista kila ngazi. Kuna wanachama wanaingia na wanatoka kila siku na kununuliwa kila leo. Sasa chama kitakuwa hakina kazi nyingine zaidi ya kuweka kumbukumbu,” amesema.

Amesema muswada huo unasema kuwa chama kitakachoshindwa kufanya hivyo msajili atakifuta lakini Katiba inasema mazingira ambayo inaweza kukinyima chama usajili ama kukifuta.

Mdee amependekeza kifungu hicho cha 8 (C) kifungu kidogo cha 3 kifutwe kwa kuwa kinakwenda kinyume na Katiba.

Amesema ibara ya 13 ya Katiba inasema ni marufuku kufanya ubaguzi lakini baadhi ya vifungu vya muswada huo vinakwenda kinyume.

“Uvunjwaji wa Katiba si jambo dogo. Tunataka ufanye marekebisho utakapokuja hapa (Waziri katika ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, vijana, kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama)” amesema.

Mdee amesema kifungu kingine wanachokitaka kifutwe ni kinachohusu zuio la vikundi vya ulinzi: “Hakuna asiyefahamu kuwa vikosi vya ulinzi wakati wa uchaguzi vimekuwa vikifanya kazi ya CCM. Polisi wanalinda maboksi ya kura. Kusingekuwa na shida kama majeshi yangesimama katikati.”

Salome Makamba:

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Salome Makamba amesema Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018 ukipitishwa kuwa sheria, itawachinja walioitunga.

“Dua la kuku halimpati mwewe. Leo mnaitazama kesi ya CUF mnaitazama Chadema. Sheria itakuja kuwachinja walioitunga kwa kumpa mamlaka makubwa msajili ya kufuta vyama vya siasa,” amesema Salome akibainisha kuwa kazi ya Msajili wa vyama ni ulezi kwa vyama.

Zitto Kabwe:

Mwaka 1933, Adolf Hitler alipeleka Muswada wa Sheria Bungeni (enabling act), wabunge wa chama chake wakaupitisha kwa mbwembwe. Miezi 6 baada ya kuanza kutumika Ujerumani haikuwa na chama cha siasa. Hitler aliitumia sheria ileile ilopitishwa na Bunge kuhakikisha vyama vinafutwa na hata wanasiasa wanaikimbia nchi

Madhara ya Muswada huu yanakwenda zaidi ya Ushindani wa chama tawala, CCM dhidi ya Upinzani. Msajili anapewa mamlaka makubwa na muswada huu yatakayoleta hali ngumu huko mbeleni. Mwalimu Nyerere alijaribiwa kupinduliwa takribani mara 8 sababu ya kudhibiti uhuru wa wananchi na uhuru wa kufanya siasa lakini tangu tumekuwa na vyama vingi hakuna jaribio lolote la wananchi kuipindua serikali.

Katiba ya Tanzania ya sasa inaruhusu Uhuru wa Kukutana lakini Sheria hii inaenda kuua Uhuru huo. Msajili alitakiwa anapoona chama kinafanya makosa basi watu wangepelekwa kwenye jopo (Tribunal) ili watu wahukumiwe kwa haki.

Demokrasia si uadui!

Kati ya 2007 - 2012, data zinaonyesha kuwa watanzania takribani 1,000,000 waliondolewa ktk umasikini na ndo wakati demokrasia ilishamiri nchini. Kwa takwimu za karibuni za Benki ya Dunia, tangu Magufuli aingie madarakani 2015, watanzania takribani 2,000,000 wamekuwa masikini

=====

NUKUU KUTOKA CCM:

Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji amesema Muswada wa Marekebisho ya Vyama vya Siasa wa mwaka 2018, unalenga kuondoa uhuni na kuvifanya vyama vya siasa kufanya kazi kwa ukomavu.

Akichangia muswada huo bungeni leo Januari 29, 2019 Lusinde amesema muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa.

“Tukomae tufanye kazi za ukomavu, siyo kuzunguka kwenye corridor (viambaza) za mabalozi. Sheria zinatungwa ndani ya Bunge, viatu vinaisha soli,” amesema.

Amesema muswada huo unakwenda kuvitaka vyama vya siasa kutambua tunu za Taifa ikiwamo Mwenge na Mapinduzi ya Zanzibar.

“Msajili alikuwa akihudhuria kama mualikwa sasa anasimamia na kuangalia demokrasia kama inatekelezwa ndani ya chama,”amesema.

Amesema muswada haukatazwi kulindwa kwa chama chochote cha siasa na hakuna chama ambacho kimekatazwa kuwa na mlinzi wa kukilinda.

UPDATES:

"Bunge limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa utakaoongeza uwajibikaji miongoni mwa vyama vya siasa na kukuza demokrasia nchini" Dkt Hassan Abbasi, MsemajiMkuu wa Serikali

View attachment 1008495

MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Mwaka 2018, umesomwa kwa mara ya pili bungeni huku vyama vya siasa vinavyopata ruzuku ya serikali, vikitakiwa kuwa na akaunti maalumu ya benki kwa matumizi ya fedha hizo, ambazo vyama vitakavyoshindwa kuzisimamia vitafutiwa. Aidha, muswada huo ambao uliwasha moto nje ya Bunge, umempa nguvu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu wa mapato na matumizi ya fedha za vyama vya siasa.

Akiwasilisha muswada huo jana bungeni, Waziri wa Nchi, Osi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu), Jenista Mhagama alisema lengo la akaunti hiyo maalumu ya ruzuku ni kuhakikisha fedha za ruzuku zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na sheria.

“Lengo ni kuhakikisha chama cha siasa kinachopata ruzuku hakichanganyi mapato na matumizi ya fedha za ruzuku na fedha kutoka katika vyanzo vingine,” alisema Jenista. Alisema Kifungu cha 24 cha muswada kinakusudia kurekebisha Kifungu cha 18 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ili kumpa msajili mamlaka ya kusitisha ruzuku kwa chama cha siasa, kinachoshindwa kusimamia matumizi ya fedha hizo, kwa lengo la kulinda fedha za umma zisitumike vibaya. Vile vile, kifungu hicho kinataka kumpa msajili mamlaka ya kumuomba CAG, kufanya ukaguzi maalumu mapato na matumizi ya chama cha siasa, ili kumwezesha msajili kubaini .

upungufu uliopo katika mapato ya matumizi ya chama cha siasa. Alisema Kifungu cha 21 cha muswada huo, kinakusudia kuweka Kifungu kipya cha 12 C cha Sheria ya Vyama vya Siasa ili kuvitaka vyama hivyo kutoa tamko la mapato na matumizi katika chama cha siasa.

Jenista alisema Kifungu cha 22 cha muswada kinakusudia kurekebisha Kifungu cha 13 cha Sheria ya Vyama vya Siasa ili kujumuisha vyanzo vya mapato vya chama cha siasa ya ndani ya nchi katika vyanzo vya mapato, vinavyopaswa kuwekwa wazi kwa msajili, lengo nikuwezesha msajili kuratibu vyema mapato na matumizi ya vyama vya siasa.

“Lengo pia ni kuvitaka vyama vya siasa kuteua Asa Msuhuli atakayesimamia mali za chama, lengo ni kuwezesha kila chama cha siasa kuwa na mtu anayewajibika katika mapato na matumizi ya chama, ili kudhibiti mfumo wa uwajibikaji katika utunzaji wa mali za taasisi,” alisema.

Alisema Kifungu cha 25 cha muswada kinakusudia kufuta na kuweka kifungu kipya cha 18A cha sheria ili kuweka sharti kwamba mwaka wa fedha wa kila chama, unapaswa kuwa sawa na mwaka wa serikali, kwa kukitaka chama kuwasilisha taarifa za hesabu zake kwa CAG kwa ukaguzi na kutoa taarifa ya hesabu zilizokaguliwa kwa msajili. Alisema Kifungu cha 11 cha muswada kinakusudia kuongeza vifungu vipya 8C, D, na E katika sheria, ambapo Kifungu cha 8E kinaweka katazo kwa chama cha siasa kuanzisha kikundi cha ulinzi na usalama au kuendesha mafunzo ya kutumia nguvu au silaha ya aina yoyote kwa wanachama wake au mtu yeyote.

“Kifungu cha 7 cha Muswada kinaongeza sehemu mpya IIA na kifungu 6A, B na C ambapo katika sehemu IIA inahusika na uundwaji wa vyama vya siasa ambapo Kifungu 6B kinaweka sifa za mtu anayeomba kusajili cha awe raia wa Tanzania na kifungu 6C kinataka mwanachama awe raia na kinakataza raia wa nje kushiriki katika kufanya uamuzi ya chama,” alifafanua waziri
 
CCM ni ukoo wa panya—babu mwizi, baba mwizi, watoto wezi, wajukuu wezi, vitukuu wezi, vilembwe wezi na vining’ina wezi! Ukoo huu wa panya walikuwa wanasafiri katika boti la muhogo, lakini kwa sababu ya uroho wao, walianza kulitafuna boti! Kilichofuata ni ukoo mzima wa kizazi cha panya kuzama na kuangamia.

CCM wameanza kuitafuna nchi tangu mwaka 1961 lakini ukomo wao wa kutafuna rasilimali za nchi ni mwaka 2020 kwani hakuna mtanzania mwenye hamu ya kuongozwa na chama cha kifisadi kama CCM ambacho kimeshindwa kuboresha maisha na ustawi wa watanzania. Wananchi wamechoka kubebeshwa ‘magunia ya misumari’ ya bei ya juu ya chakula, mfumuko wa bei wa kutisha, elimu duni, maisha duni, ufisadi wa kutisha na matatizo lukuki yanayosababishwa na panya (CCM) hawa wasiokuwa na haya! Kizazi kizima cha CCM kinakaribia kuzama na kusahaulika kabisa katika ardhi ya Tanzania.

It’s a matter of time before CCM dynasty comes to an end, and that’s when magambas will apprehend the significance and power of the people. Desolately, CCM have been ignoring and looking down their noses at common Tanzanians for many years. Time has now come when citizens can no longer endure CCM’s tyranny and corrupt rule. Everybody is tired of living like a slave on a land endowed with an assortment of natural wealth which only benefits minority fisadis and a few elites in power while majority Tanzanians lead very miserable lives.

What comes around goes around. Let CCM go to hell for good because they have absolutely failed to uplift the living standards of millions of Tanzanians at the expense of a few fisadis whose gargantuan stomachs never fill up! And no one should be blamed for the hatred and grudge that majority people hold against CCM and their crooked government except fisadis themselves who, horrifically, decided to gnaw the cassava-made boat by which they were sailing!
 
muswada huo unalenga pia kuviimarisha zaidi vyama vya siasa...

Sasa upinzani mnacho lalamika ni kitu gani sasa... Kama mswada wenyewe ukipita unaenda kuimarisha vyama vya siasa?
 
Rubbish! Ushahidi mwingine wa Bunge UOZO/DHAIFU udikteta na udhalimu utakithiri nchini chini ya huyu dikteta na dhalimu ambaye ni janga kubwa la Taifa.
Kuna dikteta zaidi ya yule alienyofowa kipengele cha ukomo wa uongozi na akaweka kipya hakuna mwanachama kwenda mahakamani kuhoji ukihoji unafukuzwa chama!
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom