Kutoka Bungeni muda huu: Wabunge wailalamikia Takukuru kuwasumbua majimboni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka Bungeni muda huu: Wabunge wailalamikia Takukuru kuwasumbua majimboni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Faru Kabula, Jul 12, 2010.

 1. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,631
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Wakati kipindi cha maswali na majibu kikiendelea sasa hivi, Spika wa bunge Bw. SS alisitisha maswali kwa muda na kutoa kauli kwamba amekua akipokea malalamiko kupitia ujumbe kutoka kwa wabunge kwamba wanasumbuliwa na TAKUKURU huko majimboni. Bwana SS akauliza, "sasa mbunge wa sasa anatekeleza ahadi zake alizotoa 2005, anagawa vyerehani, halafu TAKUKURU wanamsumbua, tunaomba baada ya maswali na majibu mwanasheria mkuu atoe ufafanuzi", alisema SS huku wabunge wakishangilia kwa nguvu.

  Katika tukio lingine, spika amemzuia Naibu waziri wa Fedha, Omary Yusuf Mzee kumuita yeye (SS) kuwa ni Naibu Spika badala ya Spika. "Naona hii ni mara ya pili unaniita naibu spika" alisema SS na kumfanya Yusuf Mzee kuomba msamaha huku wabunge wakifa mbavu.

  Tukio lingine pia lilimhusu SS, pale alipomtaka waziri mmoja kukaa vizuri kwenye kiti, kwani waziri huyo alikuwa amekizungusha kabisa kiti chake kiasi cha kumpa mgongo spika na akawa anapiga stori na mtu wa nyuma yake huku bunge likiendelea na maswali na majibu. "Naona umezungusha kabisa kiti chako kiasi cha kunipa mgongo, ni vyema watu wote wakawa wananitaza spika. Tena umekalia kiti cha waziri wa maendeleo ya jamii" alisema SS na kusababisha kicheko kutoka kwa wabunge.
   
 2. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Asante kwa updates. wengine TV tunaziona usiku na asubuhi na wkend peke yaka
   
 3. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,631
  Likes Received: 2,871
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nipo mzigoni, ila boss amechomoka kidogo nikawasha ka TV na kulogin JF !
   
 4. D

  Dina JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nafikiri argument kubwa ya TAKUKURU, kama nilivyosikia Hosea akifanya mahojiano na Clouds FM, ni kuwa huyo mheshimiwa mbunge, alikuwa wapi siku zote akaanze kutoa misaada hiyo leo? (hata wewe mwananchi wa kawaida jiulize, three months from election month!). hata mimi kwa maoni yangu, hiyo ni rushwa tu wala spika asitetee ujinga...
   
 5. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  that is typical rushwa, hivi kazi ya mbunge ni kuahidi na kugawa cherehani? kweli hii nchi imeishiwa viongozi wa ukweli
   
 6. telele

  telele Member

  #6
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapo SS anatetea uozo, na siajabu anatetea anayoyafanya yeye kwenye jimbo lake anajihami kabla ya hatari. kuna mambo wanafanya hawa waheshimiwa majimboni kwao ni ajabu kabisa, kama huku umasaini kwetu, hawa wabunge waliopo madarakani wanarudi siku za weekend na kuwachinjia wamasai wenzetu ng`ombe kadhaa na kugawa masanduku ya bia kwa wenyeviti wa vijiji wawagawie wananchi wao, sasa huko ni kutekeleza ahadi jamani? TAKUKURU wakipiga picha matukio hayo na kuwahoji wananchi nani ametoa ng`ombe hao na bia hizo, mbunge analalama eti anaingiliwa wananchi wake kuhojiwa. hizo ni dalili za kutokubalika. TAKUKURU fanyeni kazi yenu msimuogope huyo SS. kama viwango vyenyewe ndio hivyo, basi ameshajichokea huyo
   
 7. D

  Dina JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nafikiri argument kubwa ya TAKUKURU, kama nilivyosikia Hosea akifanya mahojiano na Clouds FM, ni kuwa huyo mheshimiwa mbunge, alikuwa wapi siku zote akaanze kutoa misaada hiyo leo? (hata wewe mwananchi wa kawaida jiulize, three months from election month!). hata mimi kwa maoni yangu, hiyo ni rushwa tu wala spika asitetee ujinga...
   
 8. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hiyo anayotaka kufanya SS kwa lugha ya kitaalamu inaitwa "INTIMIDATION THREAT"... by just that statement TAKUKURU itakuwa kwa namna moja au nyingine imeingiliwa uhuru wake hasa ukizingatia ni chombo kikubwa (BUNGE) ndo linaongelea mambo hayo....

  It is so sad
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,544
  Likes Received: 18,175
  Trophy Points: 280
  SS pia ni jeuri, kiburi na mbishi fulani. Sheria ya gharama za uchaguzi tumeipigia kelele sana, wao wakaipitisha, na sasa ndio wanafungua macho kujua kuwa ni msumeno unakata mbele na nyuma kama upanga wa makali kuwili.

  Hosea alifafanua vizuri kuhusu hili, siku alipozungumza live na Clouds radio. Alisema sheria hiyo inakataza kufanya aina yoyote ya wema kuelekea uchaguzi, ila amesema kutimiza ahadi kunaruhusiwa kwa shurti, lazima mbunge ambaye hakutekeleza ahadi kipindi chote kilichopita, lazima airidhishe Takukuru, kwa nini hakutekeleza ahadi hizo kipindi chote cha nyuma, pili athibitishe huo uwezo wa kutekeleza ahadi hizo sasa, ameupata wapi ambapo huko nyuma hakuwa nao. Tena Hosea akaonya na kuwatahadharisha wabunge, 'tusionane wabaya', akasema wale wabunge ama wakombea wanacheleweza kutimiza ahadi zao kwa makusudi ili wazitimize karibu na uchaguzi, vijana wake, watakufa nao.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  sita kweli ni mfamaji, naonna haishi kutapatapa. tutaona mengi mwaka huu
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Watu wote tuliilalamikia sana hii sheria, mimi naona inaweza kuwa break through ya kuingiza wabunge wa kweli msimu huu!!!
  Maana naona kwama vijana wa Hosea watakuwa wakali kama nyigu namna hii, wabunge uozo wote hawatarudi, na inaweza ikaleta wabunge wa kweli (ikiwamo na wa upinzani).

  Unaweza kuta hii sheria ikawatafuna kwa staili ya msumeno tukajikuta na hung parliament!!
  Ngoja tuongeze pop corn tuone!!
   
 12. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ebu waache izo childsh game!1
  thats rushwa.
  final
   
 13. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #13
  Jul 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Wakiona vipi basi waifute tena hiyo Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kurudisha ile ya TAKRIMA!
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jul 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naomba ndugu Gabu kama Mwanasheria Mkuu akitoa ufafanuzi utupashe habari amesemaje!
   
 15. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Standing by ndg Gabu!!
   
 16. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Bunge siku hizi = zekomedi
  Spika SS = masanja!
   
 17. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Ahaaa, kumbe imefika zamu yake na yeye ( Bw Hosea) kuwawashia moto eeeeeh???? Si ndio hawa hawa walitaka kumwaga ka-ugali kake pale walipotaka kumchiomoa mzima mzima kutoka kwenye ka-ofisi kake kenye kiyoyozi kwa kisa cha TAKUKURU kutokuwa na meno ya kuumia mafuisadi papa? Haya bwana, ngoja tuone tamthilia itaendeleaje. Ila kama kuna mbunge anafanya madudu, wewe hosea kamata hata kama wakirudi watamwaga ka-ugali, potelea mbali utakuwa umeondoka kishuja na wewe umeondoka na wa kwako na umeandika historia kwamba angalau ulijaribu kuwaguza akina mafisadi papa japo, papa hawa si wakubwa saaana, ila haidhuru, kula nao sahani moja bro!
   
 18. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #18
  Jul 12, 2010
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hahaha!! Tatizo la wabunge wetu wanatunga/kupitisha vitu ambavyo hata hawavijui kabisa...sasa Sitta alitegemea atoe vyerehani halafuTAKUKURU wamwangalie tu???Sheria hii ya Gharama za Uchaguzi ni wao walioipitisha na PCCB ni enforcement agency tu, kwaiyo kama ina tatizo waibadili wao wenyewe.
  Nasikia A.G kawapa ukweli wao...
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Spika mara hii umesahau kuwa sheria hii mlitunga ninyi wenyewe juzi tu, elewa kuwa TAKUKURU wanatekeleza sheria mliyoitunga kwa jazba na kusainiwa kwa mbwembwe. Bila kujali malalamiko kutoka kwa wadau kuhusu mapungufu ya sheria hiyo. Sasa mnalia nini. Kumbuka,

  You dont have to cry on a self inflicted injury or volenti non fit injuria
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Hili ndo tatizo kubwa la watunga sheria wetu, wakiwa wanatunga sheria hawaangalii mbali wanaangalia mwisho wa pua, sheria hii haina hata miezi sita imeshafanyiwa marekebisho mara moja ( kufuatia ugunduzi wa Mh. Slaa), sasa malalamiko yameanza tena itabidi ibadilishwe hata mwaka haujaisha.

  Kuweni serious jukumu mlilopewa na wananchi ni kubwa sana sio kukaa kwenye viti na kuzunguka badala ya kusikiliza na kutafakari mijadala kwa faida wa wananchi waliowapa kura ( na hata waliowanyima) amkeni mtajikuta mmetunga sheria kuwa kusiwe na bunge kama mambo yenyewe ndo haya.
   
Loading...