Kutoka Bungeni: Mbunge Mageni adai kuna ufisadi kwenye Halmashauri

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Sumve (CCM), Kasalali Mageni ameitaka Serikali kushughulika na ufisadi katika ngazi ya halmashauri na Wilaya alikodai kuwa bado kuna shida.

Mageni ameeleza hayo leo Jumatano Februari 3, 2021 katika mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli ya ufunguzi wa Bunge la 12.

Amesema katika ngazi za juu Serikali imefanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini katika maeneo ya chini akitolea mfano halmashauri na Wilaya kazi kubwa inahitajika.

Amebainisha kuwa kwenye halmashauri na Wilaya fedha nyingi za matumizi zinapelekwa lakini hazitumiki inavyotakiwa na kwamba bado kuna miradi hewa, usimamizi mbovu wa fedha na fedha nyingi kupotea.

“Hata ubora wa majengo na miradi inayosimamiwa na Halmashauri haujafikia viwango vinavyotakiwa. Tamisemi inatakiwa kuangalia halmashauri kwa jicho la pili,” amesema
 
Ukweli ndio huo. Halmashauri pamoja na Mh. Rais kuwaweka chini yaku bado kuna madudu ya kutisha. Nadhani kuna makosa yalifanyika kwa Rais kuwateua Wakurugenzi.

Matokeo yake ni kila mtu kiwaogopa si Mkui wa Wilaya wala Mkuu wa Mkoa. Na kwa jinsi walivyotumika kwenye uchaguzi basi ndio kabisa wamekuwa wafalme kwani wana siri kubwa za wanasiasa ikiwemo wabunge.

Nilibahatika kutembelea Morogoro mjini kwa wiki moja nikashangaa kukuta barabara za mji zina mashimo ya kutisha tena karibu zote na hata nilizoambiwa zimejengwa karibuni nazo zina mashimo ya kutisha.

Wanfukia mashimo kila baada ya miezi minne lakini bado haisaidii. Hizi ndio halmashauri zetu na leo baada ya upinzani kuondoka ndio wamewaachia kodi za majengo na mabango basi ndio itakuwa shida kubwa. Jafo kwa kweli halmashauri zimemshinda kama zilivyomshinda Pinda kabla hajawa Wazir Mkuu.
 
Mambo mengine ni hisia tuu. Wanaiba nini huko bhana? Tunapeleka bei gani hadi tuwasakizie misala kila siku? Halmashauri zenye hela ni za Dar tuu, kwingineko choka mbaya hadi viongozi wake
 
Back
Top Bottom