Kutoka Bungeni: Maswali ya Papo Kwa Papo kwa Waziri Mkuu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,571
Wababodi,

Kila nipatapo nafasi, huja mjini Dodoma na kujivinjari viwanja vya Bunge. Ndivyo nilivyofanya asubuhi hii ya leo, hivyo nitawaletea maswali ya papo kwa papo live toka hapa viwanja vya bunge, karibuni.

Ikumbukwe kwa wiki mbili zilizopita, kipindi hiki hakikuwepo kutokana na PM Pinda kupata udhuru.

Maswali yameanza. Kwa kawaida swali la kwanza hutoka kwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, ila asubuhi hii, Mhe. Mbowe hayupo.

Swali la 1: lilihusu UWEKEZAJI HOLELA
Jibu: Kuna wawekezaji wazuri na wabaya tutaendelea kuwatathimini kuwabaini wawekezaji wakweli na wawekezaji uchwala ndipo tujue hatua za kuchukua.

Swali la 2: Toka kwa Mhe. Mohamed Nyaa, linahusu Tanzania kujitolea katika ulinzi wa amani, ila Tanzania tunanyimwa fungu la malipo.

Jibu
: Ni kweli, lakini sasa tutatumia fursa hizo vizuri amemshukuru Migiro kusaidia na Wamarekani wamejitolea kutufunza.

Swali la 3. Toka kwa Mhe. Mwigulu Mchemba, ameuliza kuhusu sheria ya manunuzi ndio chanzo cha ufisadi na huduma za kiwango cha chini na kupaisha bei, amelink na direct sourcing kuokoa zaidi mapato.
Jibu: Inategemea uaminifu wa wahusika, watendaji sio waaminifu wana collude na suppliers kupaisha bei ili kupata cha juu!.
La nyongeza, watendaji hao wa makosa ya manunuzi tuwaingize kwenye kosa la wahujuu uchumi.
Jibu. Ni wazo zuri, ila inategemea uwezo wa kuwabaini kutoka na usiri uliopo.

Swali la 4: Toka kwa Mhe. Rajab Mbaruk na linahusu uwezo wa serikali yetu kukabiliana na maafa mbalimbali kama kuzama kwa boti hivi karibuni.
Jibu: Usimamizi wa kuzuia majanga hatuko makini!. Pande zote mbili zitazingatia viwango, lazima tukubali kulikuwa na laxity.
la nyongeza: Kwa vile jibu lako limethibitisha kuna uzembe upande wa Sumatra, jee utachukua hatua gani kwa uzembe wa SUMATRA,
Jibu: yaliyopita si ndwele, tugange yajayo. Tunasubiria taarifa ya uchunguzi ya SMZ na tutachukua hatua stahiki.

Swali la 5: Toka kwa Mhe. Tundu Lissu. Kwa mujibu wa katiba ya JMT, nini maofisa waandamizi wa serikali hawapaswi kuwa wabunge. Baada ya wabunge kuteuliwa kushika nafasi za maofisa waandamizi wa serikali, walipaswa kujiuzulu ubunge, kwa nini mpaka sasa, maofisa waandamizi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa bado wako bungeni?.
Jibu: Sina uhakika na hili, mwanasheria mkuu yupo atalishughulikia. "Vingunge wenzio wanaofahamu madudu haya, watalishughulikia hili na ikibidi kauli ya serikali kuhusu hili, italetwa bungeni kulifafanua"-Pinda.

Swali la 6: Toka kwa Mhe. Marriam Msabaha kuhusu watoto wa mitaani.
Jibu: Watoto wa mitaani ni tatizo la jamii na ni changamoto, jitihada zipo ila idadi inaongezeka kila kukicha, jitihada zinaendelea.

Swali la 7: Kutoka kwa Susan lymo, kwanini serikali imeondoa kipengele cha dini kwenye hojaji za sensa?.
Jibu: Hatupangi maendeleo kwa kuzingatia vigezo vya dini, kiserikali tumeona halina tija ili kuepuka kigogoro ya nani wengi.
La nyongeza, matumizi ya waalimu kutokana na uaminifu.
Jibu. Sensa inatoa fursa kwa walimu, hivyo sasa wametoa fursa kwa watanzania wenye sifa ambao hawana kazi.

Swali la 8: toka kwa Mhe. Peter Serukamba. Serikali ilifuta ushuru kwa wafanya biashara ndogo ndogo na badala yake serikali iliahidi kutoa fedha za ruzuku kufidia kutotoza ushuru kwa biashara ndogo ndogo, jee fedha hizo za ruzuku zinapelekwa wapi?. Kwa nini wafanyabiashara ndogo ndogo wanaendelea kutozwa ushuru?.
Jibu. Serikali itatoa kauli rasmi kusisizia msisitizo.
la Nyongeza, jee serikali inatoa kauli gani kwa Meya wa Kigoma kuendelea kutoza ushuru huu?.
Jibu. Kwa vile Mhe. Serukamba ni mjumbe wa baraza la madiwani, hivyo anajua kinachoendelea, ila tutalifuatilia na kutoa taarifa rasmi.

Maswali yamekwisha.

MY Take.
Mengi ya maswali ni maswali mepesi mepesi yasiyo na burning issues, na mengine yakiwa ni leading questions ambayo hayana impact wala serious relevance!. Kwa upande wange kipindi cha maswali na majibu cha leo, kilikuwa na swali moja tuu la msingi, lile la Mhe. Tundu Lissu na angalau kidogo swali la Mhe. Mchemba na kidogo zaidi swali la Serukamba akijaribu kumtundika mtu msalabani kwa mlango wa nyuma.

Kwa msiofahamu, hata kuuliza maswali nayo ni fani inayohitaji kichwa, uwezo na kujipanga, wengi wa waheshimiwa wabunge wetu ni weupe mno upstairs, hivyo kuishia kuuliza maswali laini laini kama maini na mepesi mepesi kama upepo huku wakitegemea kupata majibu magumu!

Asanteni,

Pasco.
 
SWALI LA KWANZA: UWEKEZAJI HOLELA
JIBU: Kuna wawekezaji wazuri na wabaya.

Swali la pili toka kwa Mohamed Nyaa, linahusu Tanzania kujitolea katika ulinzi wa amani, ila Tanzania tunanyimwa fungu la malipo.

Jibu: Ni kweli, lakini sasa tutatumia fursa hizo vizuri amemshukuru Migiro kusaidia na Wamarekani wamejitolea kutufunza.
 
Wababodi,

Kila nipatapo nafasi, huja mjini Dodoma na kujivinjari viwanja vya Bunge. Ndivyo nilivyofanya asubuhi hii ya leo, hivyo nitawaletea maswali ya papo kwa papo live toka hapa viwanja vya bunge, karibuni.

Ikumbukwe kwa wiki mbili zilizopita, kipindi hiki hakikuwepo kutokana na PM Pinda kupata udhuru.

Maswali yameanza. Mbowe hayupo.

Tuhabarishe mambo mengine yaliojiri Dodoma, kama ni bunge tunaangalia live kupitia tv.
 
Swali la 3. Toka kwa Mchemba, ameuliza kuhusu sheria ya manunuzi ndio chanzo cha ufisadi na huduma za kiwango cha chini na kupaisha bei, amelink na direct sourcing kuokoa zaidi mapato.
Jibu: Inategemea uaminifu wa wahusika, watendaji sio waaminifu wana collude na suppliers kupaisha bei ili kupata cha juu!.
 
La nyongeza, watendaji hao wa makosa ya manunuzi tuwaingize kwenye kosa la wahujuu uchumi.
Jibu. Ni wazo zuri, ila inategemea uwezo wa kuwabaini kutoka na usiri uliopo.
 
Swali la 4. Uwezo wa serikali yetu kukabiliana na maafa toka kwa Rajab Mbaruku.
Jibu: Usimamizi wa kuzuia majanga hatuko makini!. Pande zote mbili zitazingatia viwango, lazima tukubali kulikuwa na laxity,
 
la nyongeza, utachukua hatua gani kwa uzembe wa SUMATRA,

jibu, : yaliyo[ita si ndwele, tunasubirio taarifa ya uchunguzi tutachukua hatua stahiki.
 
Sali la 5: Tundu Lissu.
Kwanini watendaji waandamizi wa serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa kuwa wabunge,
Jibu: Sina uhakika na hili, mwanasheria mkuu yupo atalishughulikia.
 
"Vingunge wenzio wanaofahamu madudu haya, watalishughulikia hili na ikibidi kauli ya serikali kuhusu hili, italetwa bungeni kulifafanua"-Pinda.
 
Swali la 6 toka kwa Marriam Msabaha kuhusu watoto wa mitaani.
Jibu: Watoto wa mitaani ni tatizo la jamii na ni changamoto, jitihada zipo ila idadi inaongezeka kila kukicha, jitihada zinaendelea.
 
Swali la 7: Kutoka kwa Susan lymo, kwanini serikali imeondoa kipengele cha dini kwenye hojaji za sensa?.
Jibu: Hatupangi maendeleo kwa kuzingatia vigezo vya dini, kiserikali tumeona halina tija ili kuepuka kigogoro ya nani wengi.
 
La nyongeza, matumizi ya waalimu kutokana na uaminifu.
Jibu. Seansa inatoa fursa kwa walimu, hivyo sasa wametoa fursa kwa watanzania wenye sifa ambao hawana kazi.
 
`Swali la 8 toka kwa Peter Serukamba. fedha za kufidia kutotoza ushuru kwa biashara ndogo ndogo zinapelekwa wapi maanana haifikishwi kubnakohusika, wafanyabiashara ndogo ndogo wanaendelea kutozwa ushuru!
Jibu. Serikali itatoa kauli rasimi kusisizia msisitizo

Maswali ya,ekwisha.
 
Waziri Mkuu ,MIZENGO PINDA amesema Siyo mgomo uliosababisha baadhi ya Walimu kutochukuliwa katika zoezi la sensa.
Waziri mkuu amesema hoja iliyotumika ni kuyapa fursa makundi yote (Walimu, wanafunzi walihitimu shule na whitimu wa vyuo vikuu ambao hawana kazi) kutumia fursa hiyo.
 
Back
Top Bottom