Kutoka Bungeni: Makato 15% HESLB Yako Kisheria

Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,126
1,837
Habari wadau,

Leo Bungeni ishu ya Makato kichomi kwa mtumishi mnyonge aliesomeshwa na Serikali yalijadiliwa ambapo mbunge(simkumbuki jina) aliuliza " Serikali ina mpango gani wa kuyashusha makato hayo ambayo yalikuwa 8% na kuwa 15% ishu ambayo inawapa ugumu kiuchumi watumishi na wengine kukosa hata nauli za kwenda makazini"

Waziri Prof: Ndalichako alijibu "makato yapo kisheria,wadau walihusishwa na sheria kuvadilishwa,hivyo serikali ya wanyonge haina mpango wa kubadilisha makato haya"

NO Madaraja (vyeo),
NO Mabadiliko ya Mshahara,
NO Annual Incriment (July),
Matibabu,Nauli Kulipwa after 1+ year,
Makando kando mengine ya Utumishi

Mtumishi tafuta source nyingine ya Income, muda ni mali, umri unakwenda, hili jukwaa linaishi, Usije kulaumu hukushauliwa,
Ushauri ni hili Bandiko...
 
Tuko kwe right truck
Tembea kifua mbereee
Ipo siku itakuwa "wrong truck" then utapewa siasa za watendaji kumuangusha,kheri kuaminishwa mambo yanaenda na huku una observe reality,sio hv anavyofanya jiwe,nguvu kubwa inatumika kuaminisha umma tupo kwenye right truck...
 
Haya ya miradi ya matrilion ndani ya muda mfupi huenda ndio chanzo cha yote haya maana inabidi serikali itukamue ile kupata fedha za kuendesha shughuli nyingine kama kutoa mikopo ya elimu ya juu, n.k.

Narudia, hii miradi yote ikiwemo kuhamia Dodoma wanaweza kuikamilisha hata kwa kulazimisha lakini wanachi tutakuwa hoi bin taabani na sekta nyingi zitaathirika.
 
Habari wadau,

Leo Bungeni ishu ya Makato kichomi kwa mtumishi mnyonge aliesomeshwa na Serikali yalijadiliwa ambapo mbunge(simkumbuki jina) aliuliza " Serikali ina mpango gani wa kuyashusha makato hayo ambayo yalikuwa 8% na kuwa 15% ishu ambayo inawapa ugumu kiuchumi watumishi na wengine kukosa hata nauli za kwenda makazini"

Waziri Prof: Ndalichako alijibu "makato yapo kisheria,wadau walihusishwa na sheria kuvadilishwa,hivyo serikali ya wanyonge haina mpango wa kubadilisha makato haya"

NO Madaraja (vyeo),
NO Mabadiliko ya Mshahara,
NO Annual Incriment (July),
Matibabu,Nauli Kulipwa after 1+ year,
Makando kando mengine ya Utumishi

Mtumishi tafuta source nyingine ya Income, muda ni mali, umri unakwenda, hili jukwaa linaishi, Usije kulaumu hukushauliwa,
Ushauri ni hili Bandiko...
Lipeni mikopo na wenzenu wapate kusoma
 
Ipo siku itakuwa "wrong truck" then utapewa siasa za watendaji kumuangusha,kheri kuaminishwa mambo yanaenda na huku una observe reality,sio hv anavyofanya jiwe,nguvu kubwa inatumika kuaminisha umma tupo kwenye right truck...
Kuna siku nimesikitika sana.

Nilikua nazungumza na afisa elimu flani.
Akanieleza juu ya upungufu wa madawati(viti na meza) kwenye idara yake ya elimu Sekondari (wilaya nzima).
Alisema upungufu wa madawati ni zaidi ya 95%, yeye kama mtalaamu alipoandika ripoti ya kueleza mamlaka juu ya upungufu huo alifatwa na Mkurugenzi na kuhojiwa kwanini anaandika kuna upungufu? Akaambiwa aandike hakuna upungufu hata 1% kwakua akiandika kuna upungufu mhe. Fulani ataleta shida sana na kuna watu watafukuzwa.

Kingine cha kusikitisha alisema katika vikao vyao afisa elimu-shule za msingi alisema wana upungufu mkubwa wa walimu wa shule ya msingi, akaitwa abadilishe ripoti zake aandike hakuna upungufu maana italeta shida.

Nilichoelewa katika yale mazungumzo ni kwamba nchi yetu hatuna uhalisia wa takwimu, hatuko serious na maendeleo wala hakuna mtawala yuko serious kuokoa elimu wala kizazi cha Tanzania.
Kila mtu apambane na hali yake tu
 
Juzi ndugai wa kope bandia na genge lake wamepitisha sheria inayozuia kutoa takwimu kinzani na za serikali
 
Vizuri si umesikia hata mchina ameanza kuteka viwanja na mashirika ya nchi kisa madeni
Ndio lkn sheria yao walibadilisha angani, na hapa natembelea magoti. Na isubiri mwakani panapo majaliwa ya uhai kwa hamu sana
 
Utamaliza tu mkuu sisi wengine tulikopa benki mambo yalibana na benki nao si unajua ila tulifunga mikanda
 
Kuna wengine wanasema wakatwe ili wengine wakopeshwe? Lakini kwa ukaribu tunasikia kuna wanafunzi wamekosa mikopo wakati serikali inakata 15%!
Aidha kama 15% imekuja ili wengine wakopeshwe je na mabepari wakibadili masharti na kupandisha makato ili nchi zingine zipate mikopo kama ndiyo sababu ya baadhi ya wachangiaji tutafika kama nchi?

Hii15% imewaletea baadh ya watumishi hasa wanaovuta pesa kidogo jumlisha mikopo basi ile asilimia ambayo benki ilimwachia, inachukuliwa yote kwenye 15% basi maisha ni kulia na kusaga meno!

Na hao wadau ni akina nani au ni wakopeshaji tu na siyo wakopaji?

Wengine wana mikataba ya 8% lakini hana wa15% ni shida kwetu kulinda mapatano!!!!!​
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom