Ninasikitika sana kwamba nilisaidia kutoa Virodine kwa wagonjwa Lugalo hospitali na ziliwafanya kuharisha sana among other side effects including deaths. Virodine zinafanana sana na dawa za kienyeji na aliyesimamia hii study ni Dr Balele na ilimlipa sana!!! Hata ilipokuja kuwa kashfa baada ya wizara kukataa kwamba haijatoa kibali hata costech vilevile Balele alihamishiwa Makao Makuu ya Jeshi kuwa Director of Medical Services badala ya kuwa Doctor incharge Lugalo hospital na Director kurudishwa Lugalo!!! Sijui hii ilikuwa demotion au promotion?
Huu mradi wa Virodine baada ya kukataliwa kwa ethical issues aliuchukua General Mboma akijua anaongoza askari wasiojua kitu na akatengeneza pesa sana kwa kushirikiana na Balele! Mungu aturehemu waTz wengi walikufa nawafahamu lakini nani atawasemea??? Jwtz ni chombo kinachoogopwa kama supreme na ndio maana askari wetu hawana wanachojua zaidi ya kuelekeza silaha mbele tu. Bado tunacrem tu!! Ofisa wa Tz hana tofauti na askari wa Kenya tu hapa jirani, tuombe Mungu isizuke vita tu tutamalizana wenyewe kabla ya adui!
Nawakilisha wakuu! yapo mengi jeshini ila nani ana ujasiri wa kusema???
Na huyo Dr. Balele si ndio mkuu wa Mkoa Shinyanga sasa, au sio?
Mbona Tanzania tunaishi kana kwamba ndio tunaingia century ya 19?
Utafiti wa namna hii, sio huko jeshini tu, au hata kwenye magereza kwa wafungwa; hauwezi kuruhusiwa popote pale. Hii ni kukiuka haki za kibinadam. Mwanajeshi ni binaadam kama walivyo wengine, na analindwa na sheria na mikataba ya kimataifa inayokataza mambo kama haya. Hii ni aibu. Na sio kweli kabisa kwamba wahusika hawawezi kufikishwa mbele ya sheria. Ni kukosa tu wasimamizi; kama taasisi zetu zinazotetea haki za binaada. Kama kweli ushahidi upo, sioni tatizo lolote la kupeleka kesi hiyo mahakamani.