Kutoka alama 'Jembe na Nyundo' hadi kuwa alama ya 'Jiwe'"

RockCarnegie

JF-Expert Member
Jan 17, 2019
963
1,927
Habani wana JF

Toka enzi za TANu kabla na baada Uhuru wa Tanganyika hadi kuzaliwa kwa CCM, chama hiki kimekuwa kikijinasibu kuwa ni chama cha kutetea maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi wa nchi hii!

Tangu Serikali ya awamu ya Rais Magufuli maarufu a.k.a Jiwe iingie madarakani Wakulima Tanzania wamakuwa wakilalamika jinsi serikali ilivyowafukarisha kwa kuharibu bei na masoko ya mazao yao! Mfano wakulima wa korosho, pamba, kahawa, ufuta, mbaazi, choroko na mazao mengine mengi yameanguka kwa kukosa masoko.

Hivi karibuni mawaziri wa kilimo na viwanda naa biashara wamesikika wakiwaambia wakulima kuuza mazao yao popote wanapotaka baada ya miaka mitano ya kuwalazimisha wakulima kuuza mazao yao kwenye vya ushirika walivyovifisilisi wao wenyewe kwa ufisadi!

Wanunuzi wa mazao wametaifishwa mali zao wakilazimishwa kutumia vyama vya ushirika kununua mazao ya wakulima. Sasa wakulima wanaambiwa wajijitafutie wanunuzi mazao yao baada ya wanunuzi kukimbia ukatili wa serikali ya Jiwe!

Jembe limegeuka kutoka kuwa alana ya ukombozi wa maisha ya wakulima hadi kuwa zana ya kuchimba kaburi la uchumi wao.

Wafanyakazi wa umma ni mwaka wa tano sasa hakuna nyongeza ya mishahara na Rais wakati kuvunja bunge alisisitiza waziwazi kuwa waendelee kufunga mikanda kwani SGR, Stigler na mandege yako njiani kuja kuwakomboa kiuchumi!

Nyundo iliyokuwa alama ya ushujaa na thamani ya wafanyakazi kulijenga taifa sasa inawatwanga wafanyakazi wa Tanganyika na Zamzibar na kuwazika kwenye kaburi umasikini na uoga uliokithiri!

Jembe na Nyundo ni alama mfilisi inayotumiwa na CCM kuwahadaa Wakulima na Wafanyakazi Tanzania! Ili kuendelea kuwanyonya!

Tunapoelekea uchaguzi mkuu 2020, ni wajibu wa Wakulima na Wafanyakazi kuukataa Ubeberu Jiwe. Vinginevyo mjiandae kumusujudia miaka mingine mitano ijayo!
 
Siku utakapofukuzwa kazi, utashangaa utakapoishi bila hiyo kazi

Sikuutakapoanza kutumia kipaji chako,utashangaa utakapoweza kuishi bila kuitegemea hiyo degree yako

Siku utakapo anza kutumia ubunifu wa taaluma yako, ndipo utakapokuja kugundua kuwa,unaweza kuishi bila hata kutegemea kupandishwa cheyo

Hayo unayodhani huyawezi, ni Kwa sababu tu kuna mahali umejishikiza,

Tumiaeni Elimu zenu kujikomboa, mnatumia elimu kutegemea mishahara? Kutegemea kuajiliwa? Kutegemea vyeo?

Kazi kushinda mitandaoni kupiga kelele zisizo saidia, mtakufa maskini wajinga ninyi!

Na Wana siasa muache kucheza na Nafaka zetu na vilimo vyetu
 
Heri yako tajiri unayeshinda mitandaoni kutetea watawala!
Heri yako tajiri unayetegemewa na kila mtanzania katika kula yake!
Heri yako wewe mkulima hodari usiye hitaji sera bora za kustawisha kilimo chako!
Nasubiri keki unazogawa kwa washinda mitandaoni ambao kula yao inakutegemea wewe!
Ila ninamashaka kuwa ni walewale waimba pambio za kusifu na kuabudu Lumumba bk7, ni haki yako kwa kuwa fungu ulilochagua ndiyo hilo!
 
Wewe ndio wale mkifundishwa somo leo, kulielewa ni Hadi zipite siku moja Hadi mbili ndio unaelewa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom