Kutojitambua Kwa Watanzania ndo chanzo cha Umasikini

Kinaeleweka

Senior Member
Nov 10, 2014
145
104
Ndugu zanguni wasomaji,tuna kila sababu ya kuzidi kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa kutupa uzima na uhai mpaka Leo hii tunapoelekea mwishoni mwa mwaka.

Nimekuwa nikifuatilia mambo mbalimbali wayafanyayo viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kusimamia rasilimali za hii nchi na kutuletea maendeleo.

Pia,nimefuatilia malalamiko mbalimbali ya Watanzania pale viongozi waliowapa dhamana,wanapoiba au kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Nimegundua kuwa KUTOJITAMBUA Kwa Watanzania ndo tatizo la umasikini na kudidimia Kwa maendeleo ya hili taifa kutokana na sababu kubwa 2 zifuatazo:

1.Watanzania wengi hawafahamu umuhimu wa Ushiriki wao katika mambo mbalimbali yanayowahusu kama vile kupiga kura,kuhudhuria vikao au mikutano mbalimbali ya kimaendeleo n.k.

2.Wanaofaham au wenye uelewa wa ushiriki wao ktk mambo ya msingi pia wanapuuzia kutoshiriki kwa visingizio visivyo na tija.Kwa mfano kijana msomi wa chuo,na wengine hata kazi hawana lakini kutumia nusu saa kwenda kupiga kura hawataki,bali utamwona anaangalia movie au anashinda kuchati tu na cm.Lakini utamsikia/wasikia kuuchukia sana mafisadi kama vile wizi uliofanyika ktk akaunti ya Tegeta Escrow.

Swali! Tutauumalizaje au kuwaondoaje wezi wa hii nchi bila kwenda kupiga kura na kuwatoa madarakani?

3.Uvivu ndo adui Mkubwa sana wa maendeleo ya taifa lolote lile.Watanzania wengi ni wavivu sana,si tu kufanya kazi bali hata ktk kufikiri.Niliwahi kupita mtaa wa shauri moyo,Kariakoo na kuwasikia Waarabu wanaisifia Tanzania na kuiita "Heaven of Arabs" .Kuna rafiki yao m'bongo aliwauliza kwann Tz wanaiita hivyo na mwarabu 1 akamjibu Kwa kusema ukitaka kutoka kimaisha fasta ishi Tanzania kwani fursa ni nyingi sana na Watanzania hawajui kuzitumia.

MAONI

Kutojitambua ni tatizo kubwa sana Kwa Watanzania bila kujali ni Profesa au mhitimu wa shule ya msingi,lakini kama ukishindwa kutumia haki yako ya kufanya jambo la maendeleo ,"You are Hopeless" Mpigania haki za binadamu na hasa wamarekani weusi, Martin Luther King aliwahi kusema kuwa "Stupid are those people who knows what to do, but yet they remain silent"
Tukatae kuendelea kutumika na mafisadi na hasa mama na dada zetu.

Mwisho wa ufisadi wa hii nchi utaisha pale tu mimi na wewe tutakapoenda kupiga kura na hasa kuanzia uchaguzi wa serikali za mtaa na kuchagua upinzani.Tusiwaachie Viongozi wachache kwani hawawezi kufanya lolote bila ushiriki wetu wote.

Lakini,tabia yetu ya Watanzania ya uvivu na kupenda "shortcut" ndo mwendelezo wa ufisadi.

"Exposure" ni shida sana Kwa Watanzania,ukilinganisha na mataifa yanayotuzunguka ndo maana tunashindwa kujitambua kama tunafursa au la? Tuwe na tabia ya kutembea na hasa nchi za nje au hata jirani kujifunza wanafanya nn kwani tunaona wao kuzidi kuja kwetu tu.

Ukombozi wa hii nchi ni kutokana na Watanzania wenyewe na tusitegemee wazungu,licha ya kuonyesha kwa hisia kuuchukia ufisadi Kwa kukatisha misaada na mikopo ya kimaendeleo ya taifa hili.Aibu kwa Watanzania.

Nawakilisha hoja tafadhali
 
Umenena ukweli mdau...wengi wetu tumechelewa sana kuamka kifikra...tuanze sasa.

Mapinduz ya kifikra (mawazo chanya endelevu) yanahitajika kuanzia kila mtu binafs ili kujenga jamii yenye uelewa.
 
Back
Top Bottom