Kutojengwa kwa Reli ya Kati ni Mkakati wa Malori ya Wazee? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutojengwa kwa Reli ya Kati ni Mkakati wa Malori ya Wazee?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Apr 26, 2012.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hivi karibuni tulisikia Riziki ana malory kadhaa, na zaidi ya hapo tunaona na waziri wa utalii naye yumo kwenye biashara hiyo, sasa tukiwa na watu namna hiyo kweli ipo siku serikali wakapitisha sera ya kweli ya kunyanyua au kukarabati reli ya kati na nyinginezo? au ndio itakuwa ni biashara kama kawaida mpaka ndani ya baraza la mawaziri na wengineo, na kumtupilia mbali mluguru, mgogo, nyamwezi , sukumas, jita, kerewe, haya, nyambo, bazinza nk na matatizo ya reli. na zaidi ya hapo hivi karibuni wakati wa davos ambao raisi alihudhuria na kushriki mdahalo , alimsikia pm aka waziri mkuu wa kenya akisema ili kufufua uchumi ni lazima wajenge/tujenge reli na kupunguza kuziumiza hizi bara bara na mizigo mikubwa matokeo yake barabara kuharibika muda si mrefu baada ya kutengenezwa. ndio maana uchumi wa tanzania upo mifukoni mwa watu, kwani hela inayoingia au kutumiwa inaenda kwao, wakati serikli matumizi trillioni 3, mapato ni 1 trillion. na wachumi wetu? wanaona kwa kuwa hizi trillioni 3 zimeingia miongoni mwao na kujenga mahekalu nk basi uchumiunakuwa kwa kasi saana, wakati serkali haiwezi kujitosheleza hata kwa karatasi za kuandikia nyaraka, kulipa mishahara kwa wakati., kutoa nyongeza za mishahara n.k n.k
   
 2. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Naam! Wengi tuliowapa dhamana wamejikita kwenye biashara ya usafirishaji wa malori
   
 3. r

  rohrer Member

  #3
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwl . Nyerere aliwahi kusema 'kupanga ni kuchagua'. Huyo waziri mwenye dhamana amechaguliwa na wahanga wa hiyo reli duni.
   
 4. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,491
  Trophy Points: 280
  .. Pana ukweli hapa. Mifumo mibovu kama hii tuliyo nayo inawanufaisha sana baadhi ya watu. Ndio maana inaaminikia kuwa wakati wa vita, watu wanapata ukwasi wa kutisha!
   
 5. A

  Adili JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2012
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 1,996
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Waziri alisema malori yake yanampatia $20,000 kila mwezi - fikiria ni wangapi serikarini na wafanya biashara wakubwa wana miradi aina hiyo. Reli ya kati sahau maana hata Kagame amewasihi mpaka akachoka. Haiwezi kujengwa kwa sababu itaharibu vitumbua vya walioshikilia utamu.

   
 6. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kwa sekta ya Reli Tanzania ni ya mwisho kabisa
   
 7. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha, inakera na inauma. Tusibaki walalamikaji tu basi tuchukue hatua ya kuwanyofoa vibaka hawa.
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,740
  Likes Received: 6,016
  Trophy Points: 280
  CHADEMA waliwaambia wakipata ridhaa ya wananchi watajenga reli za kisasa wananchi waweze kuishi Mwanza na kufanya kazi Dar es Salaam. Haya sasa tusubiri hakuna rangi tutaacha kuona kutoka kwa magamba. Duniani kote reli ni usafiri wa uhakika kwa mizigo na abiria.

  Marekani, Uchina, na India pamoja na maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia waliyofikia ikiwa ni pamoja na kuwa na maviwanda makubwa ya magari bado wanafanya tafiti na kuwekeza mno kwenye reli. Sisi makapuku hata kile kidogo tulicho nacho tunakimalizia kabisa.
   
 9. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli Riz1 ana milori zaidi ya 150,mumemsikia maige naye ana yake japo nadhani idadi aliyosema siyo ya kweli.Naona suluhisho la kisiasa halisaidii.Tukodi SNIPERS wadondoshe mmoja mmoja mafisadi wote hata wakuu wa majeshi wanao shirikiana nao,mwisho tumalizie na mkuu wa kaya.Tulipo fikishana ni kubaya.No retreat no surrender on their acts.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mawazo finyu.
   
 11. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Serikali hii dhalimu haina huruma na jinsi wananchi wanavyosumbuka na ndio maana hawataki kabisa kukarabati reli zote hapa nchini. Kama reli hizi zingekarabatiwa bidhaa zingesafirishwa kwa bei nafuu kuliko sasa wanapotumia malori na hivyo mfumuko wa bei ungepungua na kuwapunguzia makali ya maisha wananchi!! Sasa kama viongozi kwa kupitia watoto wao na washirika wao wana mamia ya malori je unategemea kweli watakuwa na kipaumbele cha kukarabati reli? Maendeleo ya nchi hii yatapatikana pale tu tutakapompata Kagame wetu lakini sio tukiwa na hawa wezi!!
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Wakuu ukosefu wa reli inayofanya kazi kwa ufanisi ni hujuma kubwa katika uchumi wa nchi yetu. Huu ni ufisadi ambao ni calculated na mtu wa kawaida huwezi kuuona. Reli haifanyi kazi ili malori yapate biashara ya kubeba shehena. Kwa upande wa pili nchi inatumia pesa nyingi sana katika kujenga barabara za lami lakini barabara hizo zinaharibiwa na malori yanayobeba shehena kupita uwezo wake. Ingekuwa reli inafanya vizuri mizigo ingekuwa inapita kwenye reli na barabara zetu zingedumu; lakini kwa hali ya sasa nchi itakuwa inajenga barabara na baada ya muda mfupi zinakufa kwa kuzidiwa na shehena za malori. Investment kwenye barabara inahujumiwa.
   
 13. F

  Fofader JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Hili ni tatizo kubwa Tanzania. Decision makers hata law makers wanafanya maamuzi makubwa wakiwa na personal/corporate interest bila kudeclare kabla kama inavyotakiwa. Kazi kwelikweli!!
   
 14. a

  adolay JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Hili la kuwatoa mmoja mmoja naliunga mkono kwa 100%. Hakuna kuzunguuka hapa.

  Ni wazi kutokana na ufisadi wao baba, mama kaka na ndugu zetu wengi wanapoteza maisha kwa wingi kwa matatizo mbalimbali ambayo chanzo chake ni huu ufisadi.

  Si vibaya kuwauwa hawa maana wao wanauwa wengi indirectly- kukosa matibabu, usafiri mbovu(ajari), elimu duni nk

  Tuwauwe hawa kuharakisha mageuzi ya kweli, inchi hii yetu sote.
   
 15. A

  August JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  hapa ni biashara tatu zinakwenda kwa tatizo moja, biashara ya kwanza ni ya ma lori ya uchukuzi ambao wanaua wewe huwezi maana mtajiwako mdogo, biashara nyingine ni ujenzi wa hizo barabara usio isha.biashara ya tatu ni ya kukuza mitaji yao ili usiwafikie milele na milele, wao wanavyo amini.
   
 16. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Yote kwa yote...miaka 50 ya UHURU hakuna lolote la faida kwa mlala hoi!! Hongereni MAGAMBA kutufikisha hapa...lol
   
Loading...