Kutoa siri za Nchi nje ya Nchi ni Uhaini. Maofisa Hawa Wametoa Siri, Wakamatwe, Washitakiwe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Kitendo cha taarifa nyeti za mambo binafsi ya ndani kabisa yanayotokea ndani ya nyumba yetu na kupelekwa nje ya nchi na hatimaye kuvujishwa kwenye mitandao ya kijamii zikitokea nje ya nchi, sii jambo jema kwa usalama wa nchi.

Japo baadhi ya taarifa hizi zilikanushwa kuwa sio kweli, but as times goes by sasa documents za serikali zenye detailed personal information za maofisa wa serikali zimewekwa online kutoka nje ya nchi!. Huu ni uthibitisho kuwa huyo mtoa taarifa ni well informed hivyo hata zile taarifa za mwanzo, japo zilikanushwa, lakini zitakuwa zilikuwa ni taarifa za kweli.

Kwa watu wenye uzalendo wa nchi yao, hili sii jambo la kushangilia hata kidogo. Huu ni uhaini!. Haiwezekani mambo ya ndani kwenu tena chumbani kabisa kuja kiibukia hadharani. Hii ni aibu, wakati wa Nyerere mambo haya hayakuwepo kabisa!, hata kuwajua tuu nani ni nani ilikuwa kazi.

Sii wengi wanaofahamu kutoa nje ya nchi siri nyeti za Serikali ni kosa la jinai ya uhaini?. Haiwezekani siri za mambo yetu ya ndani kabisa, mambo ya chumbani kwenye nyumba yetu yakaanikwa kwenye mitandao ya kijamii halafu sisi Watanzania wazalendo tukishangilia na kuchekelea tuu!.
Mara baada ya kuhitimu masomo yangu, ajira yangu ya kwanza ni ajira ya serikalini. Niliajiriwa jeshini, JWTZ Airwing Ukonga. Kisha nikaajiriwa RTD na baadae TBC wakati huo TVT. Moja ya miiko mikuu ya utumishi wa umma ni kosa kwa mtumishi yoyote wa serikali kutoa nje siri za serikali. Ukitoa siri za usalama wa nchi, nje ya nchi ni kosa la uhaini na adhabu yake ni kifo. Kesi ya kwanza ya uhaini nchini Tanzania miaka ya 70 iliyomhusu Michael Kamaliza na kina Bibi Titi Mohammed, ilihusu hili.

Sio kosa kwa mtumishi tuu wa umma kutoa siri za serikali nje, bali ni kosa kisheria kwa mtu yoyote kukutwa na document yoyote ya serikali yenye muhuri siri.

School mate wangu wa Chuo cha Uandishi wa Habari, TSJ, Adam Mwaibabile 'Mwana' (RIP) alihukumiwa kwenda jela miezi 3 kwa kukutwa na barua ya serikali yenye muhuri wa siri.

Taarifa zozote za wateja kwenye taasisi yoyote iwe ya umma au binafsi ni siri, ni confidential information na zinalindwa kisheria. Hivyo ni kosa la jinai kwa mtumishi wa taasisi yoyote kutoa taarifa zozote binafsi za mtu yoyote bila idhini yake.

Hii inahusu taarifa za wagonjwa hospitali, taarifa wateja benki, taarifa za mawasiliano ya simu, emails binafsi za watu, inbox ya mtu, taarifa za usajili wa jambo lolote zikiwemo taarifa za TRA.

Miaka ya nyuma Gazeti la Mtanzania liliwahi kuandika kuwa Mfanyabiashara tajiri kuwa anadaiwa na Benki ya NBC na kuweka kiasi cha deni analodaiwa. Japo ni kweli tajiri huyo alikuwa anadaiwa, lakini kitendo cha ofisa wa NBC kutoa nje siri za deni la mteja ni kosa la jinai, tajiri alimshitaki mmiliki wa gazeti la Mtanzania, na kuishitaki benki ya NBC kwa kutoa siri za deni lake nje. Hata taasisi zinazotangazaga majina na picha za wadeni sugu zinafanya makosa, lakini kwa vile Watanzania hatujui haki zetu kisheria, tunajinyamazia tuu as if it's right. Hata zile picha zote za watuhumiwa zinazopigwa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi au picha zote za watuhumiwa wa kesi mbalimbali zinazopigwa wakiwa ndani vya vyumba vya mahakama, ni kinyume cha sheria na uvunjifu wa haki za binaadamu au haki za watuhumiwa ambao kisheria watuhumiwa wote huhesabika "innocent until proven guilt".

Juzi juzi kwenye sakata la Escrow Benki ya Mkombozi ilitoa taarifa za siri za miamala ya account ya mteja wake James Rugemalila na majina ya watu na viwango vya fedha za sadaka(lawe) alivyowagawia. Hili lilikuwa kosa kwa benki ya Mkombozi ililifanya, ni shauri tuu ya uchanga wa benki hiyo ila bahati yao James Rugemalila, ni Mkatoliki safi, kwake kuishitaki benki ya Mkombozi ambayo ni ya kanisa Katoliki ingekuwa ni kama kulishitaki kanisa, ni kama kujichumia dhambi hivyo akasamehe. Benki ya Stanbic walipoombwa majina na miamala ya wateja wao, ambayo ilitolewa cash na kubebwa kwenye viroba, waligoma katakata.

Hivi sasa kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutangaza vita na wauza madawa ya kulevya, wauzaji wakuu wa madawa hayo wameamua kuendesha kampeni kali ya kumkwamisha kwa kutangaza vita na Makonda kutaka kumuangamiza kwa kutumia silaha zozote halali na haramu, ikiwemo kuwatumia makuwadi na vibaraka wao kueneza taarifa za uongo kumhusu Paul Makonda kwa kumsingizia eti amefoji vyeti, jina lake halisi sio Paul Christia Makonda bali ni Daudi Albert Bashite na kudai kuwa alipata Divisheni Zero Form IV, ndipo akatumia vyeti vya mtu anayeitwa Paul Christian na kujiendeleza kielimu mpaka hapo alipofikia.

Mmoja wa watu hawa ni Mchungaji Gwajima akafikia mahali hadi kusema uongo huu madhabahuni au kwenye mimbari mbele ya Mungu na wanakondoo wake akidai kuwa ana vyeti kabisa vya Daudi Bashite alivyopata Zero na vyeti vya Paul Christian ambavyo ndivyo Pau Makonda anavyovitumia.

Walipoona uongo huu umepuuzwa sasa wamefikia hatua ya kuwarubuni watumishi wa umma wa TRA kutoa nje siri za serikali kwa kupeleka scanned documents zenye classified personal information za serikali nje ya nchi na vyombo husika viko kimya!.

Bila ya kujua ni nani wanaopeleka taarifa za siri za watu nje, you never know ni taarifa gani nyingine zimepelekwa bali hazijatolewa!, leo tunaridhika na ikulu kukanusha tuu simple simple kuwa hiki na kile sii kweli, lakini taarifa kama hizi za scanned copies za TRA hazikanushiki na tunapozichekea, hatujui ni taarifa zipi zitaletwa kesho!, kuna siku zitamwagwa taarifa nyeti za TISS kwenye public domain ndipo watu tuanze kutafutana humu!, and sometimes baadhi ya taarifa za mitandaoni ni very ambarasing kwa viongozi wetu kama ilivyotokea hapa kwenye taarifa hii Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi!

Kulitokea taarifa iliyodaiwa kuvuja kutoka nyumba kubwa kuwa kuna mtu kampiga mkewe!. Hili mbona ni jambo la kawaida sana mke kupigwa kwenye familia za kiafrika!, mimi mwenyewe enzi zile za ujana na ulevi, nimeishatoa vichapo sana tuu na kesho yake pombe zimekutoka,unaomba ms amaha, ila pia kuna type fulani ya wanawake ambao huwa wanatafuta wenyewe hivyo vichapo, kwao ndicho kipimo cha kupendwa!, hivyo wanafanya visa tuu ili wapigwe, na sio siri mama zetu wengi tuu wameisha chezea sana vichapo majumbani! sasa kuna ajabu gani mtu kumpiga mkewe chumbani?.

Kwa nje ya Tanzania, ni kama nyumbani, kuna nyumba kibao, wamama wanapokea vichapo lakini inakuwa ni siri ya ndani, hivyo hata kama kuna kichapo kilitembea ndani ya nyumba fulani, majirani wakajua, hawapaswi kusema chochote, sasa iweje wewe Mtanzania Mzalendo utoe siri za baba yako kumtembezea kichapo mama yako?. Hata kama lengo ni whistle blowing ili kumsaidia mama asiendelee kuchezea kichapo lakini unamdhalilisha baba, mama na familia nzima!.

Uzalendo ni pamoja na kutoanika kibarazani, dirty linen za chumbani, ili tuu watu waone mna linen!. Source ya hizi info ni fron inside toka ndani ya nyumba yetu!. Kisha ikaja taarifa kuwa mama ametishia kujiuzulu. Pia taarifa hii ilikanushwa. Mwanzo wengi wetu tulimuona mtoa taarifa kama kichaa fulani, lakini hizi taarifa za Makonda anazoshuka nazo sasa with documentary evidence, na video footages ni uthibitisho tosha, mtoa taarifa sio kichaa, ana inside informant ndani ya nyumba yetu! na pia ni proof kuwa yote yanayosemwa kumhusu Makonda ni kweli.

Mtu huyu anayetoa siri za nchi yetu huko nje alipo, atafutwe na kushitakiwa kwa uhaini. Hatua ya kwanza ni kumkamata huyo mtoa taarifa awe extradited back to Tanzania, ahojiwe kwa kuutumia utaalamu wa mahojiano ya polisi wetu mpaka ataje wanaompatia taarifa za kutuchafulia mahala patakatifu petu, washughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

Taarifa toka inside nyumba yetu zinamfikia vipi huko? , jee kuna taarifa ngapi sensitive zime leak? . Huu si uhaini tuu kama ule uhaini wa kina Bibi Titi Mohammed na Michael Kamaliza?!

Sasa kuna taarifa ya scanned copies za usajili wa gari binafsi ya Makonda ambayo imeibwa toka savers za TRA. Japo document yenyewe sio classified lakini kitendo cha mtumishi wa TRA kutoa personal information za Makonda ni kosa la jinai la kutoa nje siri za serikali.

Kama watumishi wasio waaminifu wa TRA wameweza kufanya hivi na kuachiwa, what if watumishi wa Immigration nao watafanya hivyo hivyo kwa wao kutoa zile taarifa za siri za DN File la Makonda liloko immigration lenye majina halisi ya Paul Makonda na majina halisi ya wazazi wake yanayoonyesha Paul Makonda alizaliwa kwa majina ya Daudi Albert Bashite, mzazi wake ni Mzee Albert Bashite na sio Makonda? . Hii si ni itakuwa hatari?!.

Kama watu wa TRA wametoa personal info za Makonda na kuachwa bila kuchukuliwa hatua zozote, what if watu wa msajili wa hati nao wata disclose details za affidavits za Makonda wakati anabadili jina na kuonyesha amebadili jina kihalali na kisheria kabisa kutoka jina halisi la Daudi Albert Bashite na kuwa Paul Christian Makonda hivyo kuthibitisha kuwa yote yasemwayo kumhusu Paul Makonda ni kweli kabisa!.

Shule ya Pamba alikosoma nako watoe taarifa kuonyesha Daudi Bashite alisoma Pamba Sec na mitihani ya kidato cha IV alifeli kwa kupata F za masomo yote hivyo kupata Daraja 0?.

Chuo cha Uvuvi Nyegezi nao watoe taarifa zao kuonyesha Paul Christian alijiunga chuo hicho na kuhitimu.
Chuo chá Melani na Muccobs nako kote waonyeshe ni kweli Paul Makonda alipita huko kwa issumed name baada ya kuiba vyeti vya Paul Christian akafoji vyeti hivyo kuwa ni vya kwake, akafanya udanganyifu kujipatia elimu ya juu hadi ajira kisha ndipo akaja kubadili rasmi jina kisheria yaani kwa kutumia mtindo wa putting the cart before the horse!, ila mwisho siku ujanja ni kupata sio kuwahi, na mafanikio ni kuzi make anyhow by getting rich or die trying, the end will always justify the means.

Haya yakifanyika Makonda atakuwa amefanya makosa mengi tuu ya jinai ila kutokana na utendaji wa kazi uliotukuka na kumfanya akubalike sana, utaendelea kukubalika na kuhitajika, na kwa vile Watanzania wana imani sana na rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli na kwa vile Magufuli ana imani sana na Makonda na anampenda sana, hivyo ni assumed, Watanzania wote wana imani na Makonda, hivyo tunashauri japo tuhuma hizi zina kila dalili ya ukweli, ili kumsaidia Makonda abaki salama, Rais Magufuli anaweza kummegea kidogo ile kinga yake ya kutokushitakiwa na kutokuchunguzwa kuhusu kumiliki mali kunakotia shaka, na badala yake akatengua uteuzi wa Paul Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na papo hapo kumteua Daudi Albert Bashite kuwa mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam na hizi kelele zote zitakwisha!.Hata Kikwete aliwahi kuwapenda sana wale mafisadi wa EPA, akawamegea kidogo kinga yake ya kutokushitakiwa, na hawakushitakiwa!.

Sasa watu wenye wivu na mafanikio na maendeleo ya Makonda kwa muda mfupi kumiliki mali nyingi hivyo kumsingizia nyingine ni zawadi kutoka kwa watuhumiwa biashara ya unga, wanachimbua taarifa za malí za makonda na kuzimwaga hadharani ili tuu rais Magufuli akasirike, amfanyie uchunguzi na akithibisha amtumbue Makonda, nawapa pole kuwa wamenoa!.

Waliomnunulia magari, Makonda, wamemnunulia kwa mapenzi yao kwa mkuu wao wa mkoa aendeshe gari zuri hapa mujini na hili sio kosa as long as Makonda ame declare kunakohusika.

Kama kumejitokeza watu kwa ridhaa zao wenyewe wakamletea tujizawadi twa tugari tuwili tutatu na tujiaapatiments pale Viva Towers, tujigorofa tuwili tutatu, na kumgharimia viji vakasheni vya nje ya nchi, hakuna ubaya wowote, kwa mtumishi yoyote wa umma kupokea zawadi yoyote toka popote as long as taratibu za zawadi zimefuatwa ikiwemo kuzi declare na thamani yake na mwisho wa utumishi wake wa umma, zawadi hizo hubaki ni malí ya umma.

Tena kwa Paul Makonda, tangu amezaliwa alitolewa sadaka kwa Mungu na wazazi wake baada ya kuishi muda mrefu bila kuwa aliwahi mtoto, hivyo Makonda ni Mlokole ni mchapa kazi na muadilifu sana. Hizo zawadi zote alizopewa atakuwa amezi declare kule Tume ya Maadili hivyo watu wanahangaika bure tuu na wivu wao! kwa kumuonea kijicho tuu kutokana na mafanikio yake makubwa katika muda mfupi.
Wandugu tuacheni wivu na kufuatilia maisha binafsi ya watu, kila mtu ana malengo yake ya maisha. Wengine malengo yao is to get rich or die trying. Na wewe kama unaupenda utajiri just get rich or die trying na sio kumuonea wivu Makonda na utajiri wake.

Jumatatu Njema.

Paskali
 
Maelezo meeengi point kiduchu kama kapiriton.:(

Kwa hiyo mmekubali sasa kuwa hizo mali zake na hiyo documents ni kweli? Maana waliozitoa kama wakiona uozo na hawana pakusemea wafanye je sasa?

Kikubwa mtuhumiwa adhibitishe mali yake au si yake. Akigoma si zake zitaifishwe tu kwa maslahi ya umma
 
Hata wao mikataba ya madini wanafanya siri

Wakizidiwa kete wanakuja majukwaani na kulalamika eti kwa nini muwekezahi anaenda kuchakata mchanga wa Dhahabu nje.

Hii inaashiria sirini huko kuna ubazazi

Mikoa yenye madini haifaidiki na madini yake,kumejaa vumbi,wananchi hawaelewi,chanzo? Usiri.

Mchakato wa tenda sasa hakuna,huu ulikuwa unaweka uwazi na kuondoa usiri,sasa hata tenda za manunuzi ya ndege wanajua wenyewe,kwa mfano nani anajua alichoongea mwakilishi wa Boieng?
 
Nimeishia kusoma "Hivi sasa kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kutangaza vita na wauza madawa ya kulevya, wauzaji wakuu wa madawa hayo wameamua kuendesha vita kutaka kumuangamiza Makonda wetu kwa kuwatumia makuwadi na vibaraka wao akiwemo kueneza taarifa za uongo kuwa Makonda amefoji vyeti, jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite na alipata Zero, akatumia vyeti vya Paul Christian kujiendeleza kielimu mpaka hapo alipofikia na Mchungaji Gwajima akafikia mahali hadi kusema uongo huu madhabahuni au kwenye mimbari mbele ya Mungu na wanakondoo wake akidai kuwa ana vyeti vya Daudi Bashite alivyopata Zero na vyeti vya Paul Christian ambavyo ndivyo Pau Makonda anavyovitumia."

MPUUZI KABISA WEWE!!!
 
tapatalk_1489984573126.jpeg
 
Back
Top Bottom