Kutoa na Kutotoa Namba ya Simu kwa Wanawake

Nakuuliza mtoa mada, nijibu then na mimi ntakujibu, Je huwa mnajisikiaje mnapokutana na mwanamke, ukaongea nae dakika mbili tu na hapo hapo unaomba namba? lengo huwa nini?

Kichwani kwa wanaume wengi duniani, kuomba namba ya simu ni kutaka kuendeleza uhusiano ambapo lengo lake kuu huwa ni Mapenzi.
 
Kichwani kwa wanaume wengi duniani, kuomba namba ya simu ni kutaka kuendeleza uhusiano ambapo lengo lake kuu huwa ni Mapenzi.

Hapo nimekuelewa ina nadhani ungesema lengo kuu ni kufanya 'NGONO' inge sound poa sana. Kumbe ndo mana baadhi ya watu husema kuwa wanaume wengi wanafanya maamuzi yako kwa kutumia viungo vyao vya uzazi na sio ubongo
 
Inatemea hizo dakika mbili mlikuwa na mazungumzo gani pia tupo ulimwengu wa utandawazi na utafutaji hivyo ukiwa upo limited na idadi kadhaa ya marafiki maana yake hutopata fursa nyingine za ziada hivyo ni sahihi kutoa namba hata kama umeongea nae dakika 2 na ndio maana huwa kuna business card wakati mwingine, unachotakiwa kujua unapotoa namba kuna mambo kadhaa lazima ufikirie kama alivyochangia boss hivyo basi kwa kuwa wewe ni mtu mzima basi kama atakuja na issue ya tongozo utajua nini cha kumjibu japokuwa anaweza akakupigia simu akaja na vitu positive
 
Last edited by a moderator:
Mimi siku zote huwa maongezi dakika 2 halafu naomba namba. Akinipa huwa nahisi ni binti mstaarabu asiye na muda wa kupoteza, baada ya hapo tunapanga muda ambao wote tutakuwa free kwa mazungumzo zaidi. Akikataa kutoa au akitoa namba feki huwa namhisi ni mtu anayefanya mambo yake bila kuzingatia muda na huenda hana shughuli yoyote. (yupo yupo tu)
 
Inawezekana nahitaji kuzungumza nawe siku nyingne hivyo utapewa namba, pengine nina haraka zangu muda huo hlf unanikera(hapa nakupa namba kiustaarabu ila utapiga hadi uzimie, simu haitopokelewa)
 
Niliwasikia akina dada wakiambizana kwamba, wao wakiombwa namaba za simu hutoa za waume/wachumba wao ili kuepuka usumbufu.
Hii inamaana gani?
 
mwanamke akitoa namba mara zote ni kwamba yuko interested na ww katika yale mambo aliyosema The Boss,kwa mimi huwa nikinyimwa namba ya simu huwa ninajua kunakitu katika mazungumzo hakikwenda vzr kwahy nimeshindwa kumfanya huyo dada aone ni mtu ambaye angepeenda kuendelea kuwasiliana na mm kwa swala lolote lile kama alivyosema mkuu hapo.
 
Last edited by a moderator:
Sitoi namba yangu kwa mtu niliyefahamiana naye kwa muda mfupi hvyo, labda iwe ni kwa mazingira ya kikaz...

na nakunyima namba ya sim yangu huku nakwambia live kuwa cwez kumpa namba mtu nisiyemfaham, kama ni mstaarab anaelewa, kama cyo anakuponda coz kuna wanaume hawapend kweli kushindwa......................................
 
Kuna kitu kinaitwa business card. Sasa hapo unaweza kupata namba ya mwanamke hata hujasema nae kabisa.
 
kuna wengine akikupa namba ndo 'amekubali' tongozo

kuna wengine anakupa namba kama njia ya 'kukufukuza kwa haraka' ukipiga hapokei

kuna wengine anakupa namba 'ili muwasiliane zaidi' kabla ya kukubali tongozo

kuna wengine anakupa namba kikazi zaidi,kiofisi au kibiashara zaidi,hataki mapenzi\

kuna wengine 'uarafiki tu wa kawaida'...
Na wengine akumege vocha na M-PESA/TIGO PESA kwanza kabla ya kukumwaga kama hakutaki.
 
Back
Top Bottom