Kuto kujua taratibu ndiyo sababu ya mahusiano / ndoa kuvunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuto kujua taratibu ndiyo sababu ya mahusiano / ndoa kuvunjika

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Anyisile Obheli, Aug 25, 2010.

 1. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndoa nyingi zina matatizo kwa kuwa wengi wetu wa wanandoa tumeingia na zile tabia zetu za ujana, pasi na kujua kuwa ndoa ni mlango mwingine ambao ili uweze kupita na kumudu sheria zake ni lazima ulazimike kukua kimawazo na kiakili
  pia uweze kuvua baadhi ya mavazi ya umimi na kuyavaa mavazi ya sisi yaani wawili
  kuna haja ya kubadirika tu uingiapo kwenye mlango huu wa nyumba inayoitwa ndoa na humo utakutana na mavazi mengine mazuri aina ya uvumilivu, utii, heshima, adabu, na kujifanya mjinga mwelevu.
  Mavazi ya ujuaji mwingi kwenye ndoa hayatakiwi kabisa, na kama unaona kuwa bado unayahitaji na yanakufaa basi ni vema ukaendelea kwanza kuyavaa ili ukijaingia humo usilete usumbufu kwa mweza wako, kwani huchafua sana utu wa mtu, maana hakuna sifa mbaya ya kuitwa aliachika akaolewa tena, aliacha akaoa tena.
  Kama unaona duka lako linahitaji wateja wengi, basi ni wakati mzuri wa kuwahudumia kwanza mpaka utosheke na ndipo uingie katika ndoa maana humo mteja ni mmoja tu, wala hahitaji kupanga foleni kutaka kuhudumiwa, nasema haya kwa waume na wake.
   
 2. D

  Dick JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  This is the ideal situation, practically ni tofauti mkuu.
   
 3. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  What are u talking about???? Life must be built on principles some of which may appear tough. We unataka mambo rahisirahisi tu. Unapoamua kuoa/kuolewa lazima kuna vitu vya kuacha. Usipoviacha huwezi kuwa na ndoa imara. No wonder devorce rate is increasing maana kuna watu wanataka kula keki halafu waendelee kuwa nayo
   
 4. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi mwanaume humuoa mwanamke akitegemea kuwa atabaki hivyohivyo na sio kubadilika, wakati mwanamke humkubali mwanaume akitarajia kuwa yule mwanaume atabadilika na kuachana na vitendo visivyompendeza anavyofanya. Lakini mara nyingi pia haya huwa tofauti kabisa...!
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu Anyisile,
  Naomba ruhusa yako niiprint hii thread nimpelekee wife wangu hard copy ili awe anaisoma mara kwa mara.
  Tafadhali.
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hujamwandikisha uraia wa JF bado...............wacha uchoyo bana!
   
 7. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Wengi wanatenda bila kufikiri na pia na ukawa na umimi katika ndoa ni moja wapo ya mahusiano mengi kutokufika mbali nakumbuka nikiwa kanisani padri alisema dhumuni hasa la ndoa ni kumfanya mumeo au mkeo awe mtakatifu watoto ni matokeo lini kitu cha muhimu ni kumfanya mwenzako awe mtakatifu.
   
 8. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uwe huru tu wala haina neno, umuhimu mkubwa wa jf kwangu ni kujifunza,
  kwa kile ukionacho kinakufaa kwa thread kutumia we tumia tu hahaaaahaaa
   
 9. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hii inatokana na watu ama wanandoa wenyewe kuingia humo bila kuwa na uelewa wa ni wapi wanatoka na wapi
  wanakwenda, ndoa ni kama chombo cha moto, ambacho kwa bahati mbaya huendeshwa na madereva wawili,
  ambao kila mmoja ana ujuzi wa chuo tofauti na mwenziye,
  kuna haja ya kila mmoja kujua sheria za barabara hiyo ambayo hicho chombo ndoa hutumia kwa kupita, ili kuweza kuweza
  kutoa nafasi kwa madereva hao kuweza kuimudu vilivyo,
   
 10. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisa mkuu!!! kama bado hujaamua kuacha baadhi ya vitu unavovipenda ni bora uwepo uwepo kwanza aisee.
  tusikimbilie vitu ambavyo bado hatujajitolea kuvimudu ipasavyo.:thumb:
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sawasawa kabisa kiukweli kitu ndoa kinahitaji miili iliyopoa ili kuimwagilia na kuistawisha,
  lakini miili ambayo bado ni moto kwa mambo ya tamaa, hiyo haiwezi kabisa ndoa,
  kila leo lawama na kusutana hakuishi, maana kabla hujaingia kwenye huo mlango wa ndoa
  lazima ukubali na kusaini mkataba wa kufunga mapazia yako ya madirisha ya tamaa na kukubari kuwa uko tayari kuwa kipofu kwa yaliyo nje ya ndoa bali unaona sana kwa yale ya ndani ya ndoa yako
   
 12. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  ni mtazamo huo pia nao waweza kusaidia
  ongeza bidii yako tu
   
 13. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #13
  Aug 26, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Anyisile, Hayo yote yanajulikana, utekelezaji ndo unasumbua
   
 14. g

  gnasha Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachomfanya mtu ashindwe kutekeleza ni nini hasa? Maana sidhani kama kuna sababu ya msingi
   
 15. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  sababu ya msingi ipo na hata ukisoma sana hiyo thread kwa makini utakuta ndani kuna baadhi ya vitu vunavyopaswa kuviangalia
  ili vikusaidie mala uingiapo huo mlango wa ndoa, nadhani pengine umeisoma kwa haraka sana,
  maana kubwa la maelezo yaliyopo humo ni jinsi gani watu/wanandoa/ wameziharibu na kuzivunja ndoa zao kwa kukiuka taratibu
   
 16. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  i salute you boss.
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana mpendwa ni somo fupi lakini limebeba ujumbe mzito ..ubalikiwe na bwana
   
 18. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  asante kwa kulisoma na kulielewa vile ulivyolielewa, barikiwa pia
   
Loading...