Kutishiwa kwa Zitto na Mageuzi ya lazima kwa TISS

Unaweza kuwa na asilimia fulani za ukweli kuhusu hiyo TISS .
Lakini umeandika kwa muhemko kiasi kwamba wewe umekuwa boya kuliko unaowatuhumu.
Mathalani mbinu wanazotumia akili yako ina mbinu moja tu na unadhani kuwa hii taasisi kuwepo kwa mujibu wa sheria nikuwa wazi kwa kila jambo au kufikiri kuwajibika kwa mihimili mingine kwa uwazi zaidi lkn nataka nikwambie kuwa nchi nyingine hizi taasisi ni independent agency yaani haziwajibiki kwa yoyote ziko huru ila zipo kikatiba.
Kwa taarifa yako hata kutunisha msuli kwa adui yako japo huna lengo la kupigana naye ni Mbinu ya kum neutralize hata kum defeat. Sasa chukulia iwe kweli huyo ametishiwa kuuawa na sasa kisaikolojia amevurugwa huoni kama lengo limetimia?
Kama unaowajua ni Tiss mazuzu kama unavyodai na waliingia kwa mgongo wa ujomba na kukosa professionalism hiyo nikukosa weledi wa hao wajomba vinasaba ambavyo umeonesha kuwa navyo kwa ukaribu sana .
Kama wewe ni mkweli uncover ID yako ujulikane weka contact zako hapo nitajua wewe ni jasiri uliyetayari kufia nchi na kile unaamini otherwise ni zuzu tu
Mwisho huenda unasumbuliwa na Wivu maana umeonesha wanajidai na vitambulisho vyao sasa kwanini utamani kufanya mabaya na kupata feva ya ID?
Kwa taarifa yako TISS ina watu wa aina zote mazuzu watashughulika na mazuzu wenzao kila ili kufanikisha. Je hukawahi sikia kuwa kuna wanawake wanfanya ufuska na kutoa papuchi kupata information? Je hao ni malaya?
Ila NIKUPONGEZE kuwa hata wewe ni asset kulingana na mahali unatakiwa kutumika japo IQ yako si lazima iwe kama yule zipo mission hutatumwa maana ni kilaza

Sent using Jamii Forums mobile app
Braza waache tu watoto walopoke humu JF, hawaijui hii taasisi zaidi ya kusoma mitandaoni na kusikia porojo kwa wanasiasa. Intelejensia ya taifa ni dubwana kubwa sana, huwezi kulijua hivi hivi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani mi si mtaalamu sana wa miundo na malengo ya baadhi ya taasisi za serikali hususan TISS, ila ninachojua taasisi za serikali huwa zinaundwa kwa mujibu wa sheria na miongozo kwa maslahi na faida ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Lakini bahati mbaya nilichokiona katika tukio la kutishiwa kuuwawa Mh. Zitto Ni kama vile naona malengo na muundo wa TISS haujapishana na ule muundo na malengo ya kundi au genge la Panya Road ...

Mara zote kundi/genge la kihuni Kama Panya Road hutumia technique zisizo rasmi na za kijima kwa lengo la kuathiri jamii/mtu kwa uwazi bila ya usiri, ili tu kuiogopesha jamii/mtu husika ili waweze kupora mali zao bila ya kupingwa kwa manufaa ya maisha yao ambayo siku zote huwa starehe, ulevi, uzinzi na uesherati ...

TISS is shallow wengi wa vijana wanaoajiriwa na idara nyeti kama hiyo hata darasani walikua hawaperform vizuri wana passmark za kawaida tu unategemea Hawa watu watakua intelligent kiasi Cha kujua matokeo ya wanachokifanya???

Wengi wamewekwa na wajomba zao na mashemeji zao tunawafahamu vizuri tu wao na familia zao na mpaka walivyoingizwa humo ... hakuna intelligent hapo ni upupu mtupu ... tunawajua tunakaa nao kwenye mabaa na vilinge vya kahawa kila siku wengine tumecheza nao mitaani wengi wao ni maboya tu hawana lolote ...

Intellijensia wanayoijua wao ni kuonyesha vitambulisho vya kazi zao kwenye mabaa na ma night klabu na ma hotelini ili waogopeke tu na watu au kuwatishia matrafiki barabarani na vitambulisho vyao na Kisha kujiona Kama nchi ndio yao kumbe ni ujinga na USHAMBA tu wanaoufanya tena kinyume na maadili ya taaluma zao ...

Unawezaje kumtishia mtu kumuua waziwazi hali yakua unafanya kazi kwa mujibu wa sheria Mxieuszzzz!!!

Hi TISS tunayo iongelea hata interpretation ya CCTV footage zinawashinda, bado wanatumia intelligence technique za kizamani kabisa za miaka ya 70 na 80 ambazo wenzetu walisha badilisha kutokana na maendeleo ya elimu na technolojia ...

Leo hi technique hizo wanahasau kua zimepitwa na wakati na wananchi wa miaka ya 70 na 80 sio wananchi wa miaka ya 90 kuja juu ... Hali imebadilika vijana wadogo wanna uelewa mpana kutokana na maendeleo ya elimu na utandawazi

Usishangae leo hii ukakutana na mtoto mdogo wa form two anajua kucheza na akili za watu au vitu vinavyo athiri jamii inayozunguuka kwa kubonyeza kitufe kimoja tu katika computer yake kupitia game anayocheza kuliko yule mkurugenzi wa kitengo ...

Hiyo ndio hali halisi ... Kwa kifupi TISS inahitaji mabadiliko makubwa ikiwemo kupadilisha mifumo ya njia mbalimbali za ki intelijensia husasan jinsi ya kucheza na akili za watu, kwakweli njia mnazo tumia na vijana mnao watuma kutekeleza njia hizo Ni Kama maboya tu yasiyo endana na upeo wa mambo mliyo wakabidhi ...


Sent using Jamii Forums mobile app

Umezungumza kishabiki sana.

Wewe una uhakika gani kama ni TISS ndo wanahusika kumtishia Zitto Kabwe?
 
Kuhukumu taasisi nzima na kuita jina la maudhi yaani kuita taasisi nyeti PANYA ROAD sio busara kwa tukio labda kafanya afisa mmoja tu.

Tubadilike kama watanzania hii taasisi ina heshima yake na ndio roho ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Taasisi yoyote ni Watu ,kama Taasisi inakuwa na Matendo ya Kihuni kwa Watu wake unataka Watu watafsiri vipi ?.
 
Mara zote kundi/genge la kihuni Kama Panya Road hutumia technique zisizo rasmi na za kijima kwa lengo la kuathiri jamii/mtu kwa uwazi bila ya usiri, ili tu kuiogopesha jamii/mtu husika ili waweze kupora mali zao bila ya kupingwa kwa manufaa ya maisha yao ambayo siku zote huwa starehe, ulevi, uzinzi na uesherati ...

Jiulize lengo la mpuuzi yule wa hiyo TISS Kama si Panya Road lilikua ni Nini??

Ukifahamu lengo lake (ambalo halihitaji intelijensia ya kwenda darasani kusomea) oanisha na maneno hayo juu, then utaelewa kwa nini nimewafananisha na Panya Road

Sent using Jamii Forums mobile app

Huu ni uzushi mwingine.

Yaani unchoongea ni hadithi za kutoka kwenye kile kijiwe chenu cha pale nyuma ya soko la Kisutu.
 
Wakuu Jana Zito Zuber Kabwe Alikuja Na Tuhuma Nzito Sana Kuhusu Kutishiwa Usalama Wake Na Anasema Kwamba Ni Afisa Usalama Na Mpaka Akafikia Mahali Kumwandikia Barua Spika Wa Bunge Kulalamikia Hiko Kitendo.
......
Mimi Kama Mdau Wa Ukweli Na Uwazi, Niombe Kwamba Bunge Lote Nje Mpaka Ndani Lina Cctv Camera, Itafutwe Cctv footage Ya Jana Inayoonyesha Kipindi Zito anatoka Bungeni Na Hapo Ndipo Tutaona Huyo Afisa Usalama Anaedai Alimtishia Ataonekana.

Naomba Kuwasilisha Wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yericko bana?

Kwanza unatakiwa kuwalipa Jamiiforums kwa kutumia jukwaa lao kutangaza biashara yako. Kwa mtu muungwana lazima kwanza angelipia kabla ya kuanza kutangaza biashara.

Pili, Siku hizi kila mtu anadai ametishiwa na TISS wakati hao TISS wa kweli hawajulikani na hata ofisi zao huwezi kuingia bila ruhusa maalum.

Baada ya kesi yake mahakamani kukosa nguvu ya kisiasa kwa sasa ameenda bungeni kutafuta kiki nyingine ya kisiasa kupitia TISS.

Aliyekuambia TISS hawajulikani ni nani? Je ni ofisi gani unaweza kuingia tu bila ruhusa, hiyo itakuwa ni ofisi au soko?
 
Yericko mkuu hivi unamuamini Zito kweli kwenye hilo saga? Zito anaumwa kisaikolojia anaishi kwa mawazo sana MTU kama huyo hata ukimuangalia tu anahisi unataka kumfanyia kitu kibaya. Bahati mbaya zaidi mkiambiwa kitu na MTU wa upande wenu akili zenu mnaziweka kwenye freezer kabisa, think deep mkuu.
Lissu alipo sema ananawindwa hamkuamini, akatwangwa risasi hamkuamini, akanusurika hamkuamini, akapelekwa kutibiwa hamkuamini,...........sasa hivi mnamwita mtoro!!
 
Wewe Yericko hata Kesho Waziri akitekwa utaandika na kusema nunua kitabu changu Cha ujasusi wa Kidola, Leo jumanne ofa.

Yaani eti hicho kitabu kimebeba mambo yajayo na Kiko flexible kinabadilika kutokana na matukio

Be serious on issues, sio Kila kitu biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninashangaa kuona madai ya zito yanaaminika bila kufanyiwa uchunguzi ili hali inaeleweka zito ni muongo na mzushi.ndugu zangu hebu tuwe na busara

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna jambo lolote toka kwa lisu,zito, fatuma na Mbowe bavicha wanaweza kuhoji.Na hao jamaa wanajua akili za wafuas wao.

Nokia ya kitochi yuzingi jamii foramu
 
Kwanini Jiwe anahaha na hana amani kabisa licha ya:

1. Kuweka spika wake bungeni.

2. Kuzuia bunge LIVE isipokuwa yeye yuko LIVE muda wote.

3. Kupiga marufuku mikutano ya siasa kinyume na katiba isipokuwa kwa CCM.

4. Kuteka, kuua na kufunga kila mkosoaji.

5. Kudhibiti blogs, vyombo vya habari, mitandao na majukwaa huru.

6. Kuzindua mpaka miradi koko.

BADO WATU HAWAKUELEWI TU !!!!
jamaa anadai nui yeye pekee hapa tanzania anaye weza tatua changamoto zilizopo. aktoka madarakani ndo bas tena
 
Zito anatafuta kiki kwa nguvu zote kwa sababu anajua Mbowe yupo gerezani hivyo makeke ya chadema yamepungua. Anajua kabisa alifanya kosa kuingia vikao visivyo muhusu na kufanya fujo, pia anajua hayo aliyoanzisha hayana ushahidi wowote. Huyu apuuzwe tu maisha yaendelee.
Kwa lisu mlisema hivihivi mwisho wake mmemimijia risasi 30 na yeye alilalamika kama anavolalamika zito na mkamjibu kama mnavomjibu zito na sio mtaishia kuminina risasi kama ilivokua kwa lisu..
 
Hata Rais John Pombe Magufuli naona siku hizi kabadilika kidogo...

Nyakati za nyuma ilikuwa akisikia habari kama hizi, haraka anajitokeza kwenye kamera za TV amefura na kufokafoka hovyo.....

Aone na asikie Tundu Lissu anamponda? Asikie Zitto anaponda?.....Aaaaah, alikuwa havumilii huyu msukuma.....

Kwa sasa naona kamwachia Job Ndugai kushika hatamu....
 
Back
Top Bottom