Kutishiwa bunduki!

EMM_411

Member
Mar 24, 2011
27
7
Nina jirani yangu ambaye nyumba zetu zinatazamana tunaishi pamoja maeneo ya Bunju, leo jioni nilimtuma mwanangu akamfungulie ndama ambaye alikua amefungwa nyuma ya uzio wa nyumba yetu. kwa bahati mbaya hakumkuta ndama, ndama huyu alikuwa amekimbilia kwa jirani yangu. Mtoto wangu akaenda kumfuatilia ndama huyo na kumkuta yupo kwa jirani yangu akila majani (sio akiiba), wakati kijana akiendelea kumtoa ndama kwa jirani yangu huyu, jirani aliwasili na gari lake na kumkuta kijana wangu akiwa kwake huku akiwa na ndama yule. Jirani alimuhoji kijana wangu kwanini ndama alikuwa kwake, kijana alijaribu kumuelewesha jirani yangu huyu mwenye jabza bila maelewano, ndipo alipomwambia samahani ndama alifungua, jirani kwa jazba akamwambia kijana wangu "NITAKUPIGA RISASI,NIMEKATAZA NG'OMBE KUJA KWANGU" hakuishia hapo bali alitoa Bastola yake na kumwelekezea kijana wangu huku akimwambia "NITAKUUA" Sasa mimi nilikuwa naomba kuuliza kisheria, Je jirani yangu ana haki ya kumtishia mwanangu Bunduki? Je ni hatua zipi za kisheria napaswa kumchukulia jirani yangu huyu?
Nawasilisha!
 
Huyo jirani hafai. Nadhan anaishi maisha ya upweke kama waishivyo baadhi ya nchi za ulaya. Lakn pia nadhan kosa hilo alilofanya jiran limeshawahi waweka watu wakubwa nchini hapa ndani. Pole sana. Mimi ningeenda polisi kutoa taarifa angalau
 
Pole kwa tukio. Report tukio polisi. Kama ni bunduki ya halali au isiyo, huyo jirani yako kwa kitendo alichokifanya kinamwondolea sifa ya kumiliki silaha ya moto. Sikiliza polisi watasema nini, kisha peleka stori yako kwa mbunge, radio na hata magazetini. Najua kuna upande wa pili wa habari hii, haijalishi mazingira, habari hii ni ya kuripoti kwenye vyombo husika.
 
Report polisi mkuu, anaweza kusambaratisha vichwa vya watu huyo jirani yako.
 
Huyo limbukeni wa kutumia bastola,inavyoonekana itakuwa sio ya halali na kama nihali itabidi apimwe akali kwanza ndo aendelee kuwa nayo, kamshaki afutiwe umiliki na ikibidi dai fidia ya mwanao kufundishwa uoga. Usipo mripoti polisi siku nyingine hata tishia atawauwa kweli!
 
Huyo limbukeni wa kutumia bastola,inavyoonekana itakuwa sio ya halali na kama nihalali itabidi apimwe akali kwanza ndo aendelee kuwa nayo, kamshitaki afutiwe umiliki na ikibidi dai fidia ya mwanao kufundishwa uoga. Usipo mripoti polisi siku nyingine hata tishia atawauwa kweli!
 
Back
Top Bottom