Kuteuliwa Maua Daftari huko Zanzibar kuna maana gani kwa vijana ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,366
217,411
Mkongwe Maua Daftari ameteuliwa kuwa Kamishna wa Maadili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , uteuzi huo umetangazwa na Rais wa Nchi hiyo Dkt Hussein Mwinyi .

Sina shaka na Maua Daftari , lakini ninajiuliza , hivi hakuna vijana wanaoweza kufanya kazi hizi za umma ? Hivi ni lazima tuendelee kuzungusha hawa vikongwe wa Tangu Nyerere kwenye kila Taasisi ? mbona yeye Hussein aliaminiwa akiwa kijana , kwanini anashindwa kuwaamini vijana wenzake , au ana roho mbaya ?

Nawalilia sana Vijana wasomi wa Tanzania ambao nafasi zenu zimezibwa na vikongwe , tegemeo lenu ni Mungu pekee

Nawatakia IDD njema
 
Hivi CHADEMA kupambana ili halima na wenzake waondolewe ateuliwe Joyce Mukya unamaana gani kwako wewe BAWACHA?
 
Waswahili wanasema utu uzima dawa. Labda kaona vijana wengi hawaendani na sera zake.
 
Ujumbe ni kuwa vijana wanakwama mifano hai ipo Kwa akina saa mbaya na konda boy,na mifano mingine ya waliopoteza Imani Kwa mamlakazao za teuzi pamoja na uungwaji mkono na raia wa kawaida japo Bado wengi wao Bado wanasitiriwa na mamlaka zao za teuzi ,ila muda ukifika wasiwaze hata kufikiria Tena.
 
Mkongwe Maua Daftari ameteuliwa kuwa Kamishna wa Maadili wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , uteuzi huo umetangazwa na Rais wa Nchi hiyo Dr Hussein Mwinyi .

Sina shaka na Maua Daftari , lakini ninajiuliza , hivi hakuna vijana wanaoweza kufanya kazi hizi za umma ? Hivi ni lazima tuendelee kuzungusha hawa vikongwe wa Tangu Nyerere kwenye kila Taasisi ? mbona yeye Hussein aliaminiwa akiwa kijana , kwanini anashindwa kuwaamini vijana wenzake , au ana roho mbaya ?

Nawalilia sana Vijana wasomi wa Tanzania ambao nafasi zenu zimezibwa na vikongwe , tegemeo lenu ni Mungu pekee

Nawatakia IDD njema
Akina Maua hawawezi kucheza bongo muvi wala bongo fleva hivyo acha wachape kazi na vijana watawezeshwa kwenye bongo muvi ziwapite Holiwudi ziangaliwe duniani kote.
 
Back
Top Bottom