Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,102
- 53,357
Binafsi huwa najiuliza, hivi dhana nzima ya kujaza madokta na maprofesa kwenye safu yake ya uongozi kunaleta tija gani?
Je, hao wana utaalamu wa kutosha kufanya kile wanachotakiwa kufanya? Au ni waaminifu katika utendaji wao?
Isitoshe wengi ya hao wanaoteuliwa wametolewa kwenye taasisi za elimu ya juu hususani vyuo vikuu.
Ukiangalia idadi ya madokta na maprofesa wanaohitajika katika vyuo vikuu Tanzania ni kubwa mno.
Binafsi nawafahamu waalimu wa chuo kikuu walioteuliwa kuongoza taasisi mbalimbali. Na wengi wamebobea katika nyanja ambazo utaalamu wao unahitajika kwa hali na mali hususani kwenye kufundisha na kufanya utafuti.
Muda wa kufanya tafiti na kuandika machapisho hawataupata tena.
Ni rai yangu kuwa JPM aachane na hii kasumba. Watu anaowahitaji sana sana ni watendaji ambao sio lazima wawe na elimu ya kutisha kama hawa watu.
Hawa watu wanahitajika vyuoni mwetu ambapo kuna uhaba mkubwa wa walimu na watafiti.