Kuteua Madokta na Maprofesa hakuleti tija kiutendaji

Binafsi huwa najiuliza, hivi dhana nzima ya kujaza madokta na maprofesa kwenye safu yake ya uongozi kunaleta tija gani?
Je, hao wana utaalamu wa kutosha kufanya kile wanachotakiwa kufanya? Au ni waaminifu katika utendaji wao?
Isitoshe wengi ya hao wanaoteuliwa wametolewa kwenye taasisi za elimu ya juu hususani vyuo vikuu.
Ukiangalia idadi ya madokta na maprofesa wanaohitajika katika vyuo vikuu Tanzania ni kubwa mno.
Binafsi nawafahamu waalimu wa chuo kikuu walioteuliwa kuongoza taasisi mbalimbali. Na wengi wamebobea katika nyanja ambazo utaalamu wao unahitajika kwa hali na mali hususani kwenye kufundisha na kufanya utafuti.
Muda wa kufanya tafiti na kuandika machapisho hawataupata tena.

Ni rai yangu kuwa JPM aachane na hii kasumba. Watu anaowahitaji sana sana ni watendaji ambao sio lazima wawe na elimu ya kutisha kama hawa watu.
Hawa watu wanahitajika vyuoni mwetu ambapo kuna uhaba mkubwa wa walimu na watafiti.
Ni kweli. Ndio maana chadema Mwenyekiti form six ziro. Wabunge kama Lema, Sugu, Prof. Jay, Mnyika, Kubenea, kutaja wachache elimu yao ni magumashi kwasababu hawataki wasomi.
 
Marekani na Uingereza ni vinara kwa elimu lakini wanajua udhaifu wa hawa watu ndiyo maana hawa wateui kwenye uongozi wao ni wataalamu tu.
 
Madokta na Maprofesa ninaowaamini ni wa kutoka Ulaya, Asia na Middle East ( hasa Israel ) tu pekee ila wa huku Afrika hasa hapa kwetu Tanzania nadhani hata Mimi mwenye Elimu yangu ya kutukuka kabisa ya darasa la Saba ( 7 ) ninawazidi kwa mambo mengi / vitu vingi.
Kwahio unakubaliana na mimi kuwa hawa watu wanatakiwa kurudi vyuoni?
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nadhani mtu akiitwa Professa au Dokta
maana yake 'ana elimu kubwa sana'
au anajua 'maambo meengi sana'

Kumbe ni tofauti.....
Actually proffesa au mtu mwenye PhD ni yule ambae
kwenye taaluma yake fulani amesoma zaidi au kufanya tafiti zaidi

Hii ina maana mtu mfano kasomea udaktari wa mifugo
akija kuwa professa sanasana anakuwa ana specialize na kitu kimoja tu
kwenye masuala ya afya ya mifugo
tena wala sio afya ya mifugo kwa ujumla....
labda Phd yake inahusu nutrition only..

Sasa mtu huyu kweli unakuja kumpa uwaziri wa Afya si unamuonea?

masuala ya management uzoefu ni kuhimu zaidi
na sio tu kila mwenye Phd basi ni manager
Au amesomea mambo ya Adminstration.

Mfano Msajili wa hazina unapeleka mtu mwenye Phd.

Hiyo ni misallocation ya resources.
 
Karibu kwa mchango wako mkuu.

Mara nyingi sisi Waafrika(na hasa Watanzania) tunapenda kuonyesha kuwa tuna elimu badala ya kuthibitisha tumeelimika! Hata humu JF ukimpa mtu hoja ya nguvu badala ya kukujibu anakimbilia kuulizia CV yako!

Sasa hizi mamlaka za uteuzi nazo zinarudia hayo hayo. Kuonyesha kuwa serikali imejaa wasomi!
 
Kufika kileleni kwenye ajira sio elimu, umuhimu wa elimu ni necessary industrial or sectarian knowledge inayokusaidia kufanya maamuzi sahihi.

Muhimu ya yote kufika katika senior position ni uelewe kupitia experience ya majukumu ya wengine, kuwa umeshafanya kazi kuanzia kwenye operation and middle management na mafanikio ya kazi yako yanaweza pimwa kwa CV kabla ya kufikiriwa kwenda kwenye strategic positions. Vinginevyo utashindwa simamia mkakati bila ya hizo experience.

Sisi tunadhani mtu akiwa na Phd ndio kamaliza. Unless ya management or hrm sidhani kama wengine wanaweza ruka to the top bila ya experience at lower levels decision making ndio maana uishia kuwa washauri tu wengi wao kwa sababu za kukosa management experience.
 
Tatizo ni mfumo mzima wa elimu ya nchi yetu ndio unawafanya hawa maprof na Ma Dr waonekane hawana mchango katika maendeleo ya nchi.

Kwa mfano wa kwanza hata tafiti wanazofanya baadhi yao zina kuwa kwa ajili ya manufaa ya wafadhili wanaotoa pesa sio nchi yetu. Hazileti manufaa ya moja kwa moja kwa jamii . Unakuta mtu anafanya utafiti wa kwanini twiga wanapenda kuongozana na swala. Utafiti wa masuala muhimu kama namna ya kuwasaidia wamachinga wajiendeleze hadi kuwa sekta rasmi sijui kama upo.

Mfano wa pili hata maProf na maDr waliowahi kupewa nafasi za kuongoza taasisi hapa nchini hawakufanya vizuri sana kiutendaji. Badala yake unakuta kiongozi ambaye hana PhD anaongoza vizuri sana ukilinganishwa na hao wasomi. Ukiangalia wizara kama kilimo ina ma-Dr wengi sana lakini angalia utendaji wa sekta ya kilimo hapa nchini.

Mfano wa tatu, kuna maProf na maDr ambao walijitahidi kufanya utafiti mzuri. Lakini walipojaribu kushauri serikalini tafiti zao zilidharauliwa hadi wakakata tamaa. Basi wakaona umri unaenda bora wakaingie katika siasa au ajira nyingine nje ya nchi ili wajijenge kiuchumi.
 
Binafsi huwa najiuliza, hivi dhana nzima ya kujaza madokta na maprofesa kwenye safu yake ya uongozi kunaleta tija gani?
Je, hao wana utaalamu wa kutosha kufanya kile wanachotakiwa kufanya? Au ni waaminifu katika utendaji wao?
Isitoshe wengi ya hao wanaoteuliwa wametolewa kwenye taasisi za elimu ya juu hususani vyuo vikuu.
Ukiangalia idadi ya madokta na maprofesa wanaohitajika katika vyuo vikuu Tanzania ni kubwa mno.
Binafsi nawafahamu waalimu wa chuo kikuu walioteuliwa kuongoza taasisi mbalimbali. Na wengi wamebobea katika nyanja ambazo utaalamu wao unahitajika kwa hali na mali hususani kwenye kufundisha na kufanya utafuti.
Muda wa kufanya tafiti na kuandika machapisho hawataupata tena.

Ni rai yangu kuwa JPM aachane na hii kasumba. Watu anaowahitaji sana sana ni watendaji ambao sio lazima wawe na elimu ya kutisha kama hawa watu.
Hawa watu wanahitajika vyuoni mwetu ambapo kuna uhaba mkubwa wa walimu na watafiti.

Elimu ni muhimu sana katika uongozi, ni kweli huko vyuoni kunahitajika wataalamu lakini pia na huko uraiani wanahitajika pia. Wengi wao wanafanya huko serikalini na pia wanafundisha na hivyo inakuwa na advantage ya kuhusisha experience ya mtaani. kuna viongozi wabovu wachache na ubovu wa kiongozi unaweza usitokane na elimu yake
 
Sisi tunadhani mtu akiwa na Phd ndio kamaliza. Unless ya management or hrm sidhani kama wengine wanaweza ruka to the top bila ya experience at lower levels decision making ndio maana uishia kuwa washauri tu wengi wao kwa sababu za kukosa management experience.
Well said mkuu.
 
Acha JPM avitoe hivi vibabu, vinafanya shule iwe ngumu kazi kufelisha watoto, hukusikia sakata la degree za chupi? bora aviondoe tupate wahadhiri vijana wenye weledi, ukienda kenya kuna maprofesa wana miaka thelathini tu, tunahitaji UDSM mpya yenye wahadhiri wenye fikra mpya, hawa walioteuliwa wakirudi 2020 wanakuta vijana walishalisimika maofisini.
OMG: vibabu vinafelisha-vibabu na degree za chupi-vijana wana weledi hii nimeipenda ingawapo inaukinzani sana hasa hizo mbili za mwisho labda tanzania ina vibabu vikali sana kuliko vijana!!!Tafakuri
 
Back
Top Bottom