Kuteua Madokta na Maprofesa hakuleti tija kiutendaji

Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,270
2,000
Binafsi huwa najiuliza, hivi dhana nzima ya kujaza madokta na maprofesa kwenye safu yake ya uongozi kunaleta tija gani?
Je, hao wana utaalamu wa kutosha kufanya kile wanachotakiwa kufanya? Au ni waaminifu katika utendaji wao?
Isitoshe wengi ya hao wanaoteuliwa wametolewa kwenye taasisi za elimu ya juu hususani vyuo vikuu.
Ukiangalia idadi ya madokta na maprofesa wanaohitajika katika vyuo vikuu Tanzania ni kubwa mno.
Binafsi nawafahamu waalimu wa chuo kikuu walioteuliwa kuongoza taasisi mbalimbali. Na wengi wamebobea katika nyanja ambazo utaalamu wao unahitajika kwa hali na mali hususani kwenye kufundisha na kufanya utafuti.
Muda wa kufanya tafiti na kuandika machapisho hawataupata tena.

Ni rai yangu kuwa JPM aachane na hii kasumba. Watu anaowahitaji sana sana ni watendaji ambao sio lazima wawe na elimu ya kutisha kama hawa watu.
Hawa watu wanahitajika vyuoni mwetu ambapo kuna uhaba mkubwa wa walimu na watafiti.
 
kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,094

you have a point ila sidhani rais kama atawamaliza maprof.
 
eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,610

Acha JPM avitoe hivi vibabu, vinafanya shule iwe ngumu kazi kufelisha watoto, hukusikia sakata la degree za chupi? bora aviondoe tupate wahadhiri vijana wenye weledi, ukienda kenya kuna maprofesa wana miaka thelathini tu, tunahitaji UDSM mpya yenye wahadhiri wenye fikra mpya, hawa walioteuliwa wakirudi 2020 wanakuta vijana walishalisimika maofisini.
 
Bado Tanzania inawahitaji.
Huwezi kusema watolewe ilihali vyuo vyetu vinafundishwa na watu wa masters.
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,637
2,000
Ni kweli utendaji na uadilifu haupimwi kwa kuwa Profesa. Wapo maprofesa wavivu na mafisadi wa kutosha nchini.
Wengi husomea ufisadi wengi ni wezi wa kalamu hutumia usomi wao kuiba kijanja pasipo kujulikana,kwa kifupi wanaojiita wasomi Tanzania hawana uchungu na rasilimali za Taifa wengi wapo kwa masilahi binafsi na michepuko yao,Maprofesa wa Tanzania ni tofauti na maprofesa wa Nchi zingine,mfano jaribu kuangalia Tabia ya Lipumba,kapuya,Tibaijuka,mbilinyi na yule PhD aliyenunua mabehewa feki na kuandaa mchakato wa Reli kwenda Airport.
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
10,979
2,000
Acha aendelee kuteua tu huoni UCHUMI UNAVYOPAA, UTALII JUU, HUDUMA ZA AFYA KAMA ULAYA, MAJI BWERERE HADI VIJIJINI, UCHUMI WA MWANANCHI MMOJA MMOJA UNAKUWA KWA KASI?
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,637
2,000
Acha JPM avitoe hivi vibabu, vinafanya shule iwe ngumu kazi kufelisha watoto, hukusikia sakata la degree za chupi? bora aviondoe tupate wahadhiri vijana wenye weledi, ukienda kenya kuna maprofesa wana miaka thelathini tu, tunahitaji UDSM mpya yenye wahadhiri wenye fikra mpya, hawa walioteuliwa wakirudi 2020 wanakuta vijana walishalisimika maofisini.
Ni kweli hayo ndiyo mapungufu yao wengi wamekuwa wakifanya vioja huko vyuoni
 
ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,637
2,000
Acha aendelee kuteua tu huoni UCHUMI UNAVYOPAA, UTALII JUU, HUDUMA ZA AFYA KAMA ULAYA, MAJI BWERERE HADI VIJIJINI, UCHUMI WA MWANANCHI MMOJA MMOJA UNAKUWA KWA KASI?
Uchumi unakuwa vp wakati mzunguko wa pesa hakuna? Hata thamani ya dola dhidi ya shilingi bado inazidi kupaa.
 
Bavaria

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
48,270
2,000
Wengi husomea ufisadi wengi ni wezi wa kalamu hutumia usomi wao kuiba kijanja pasipo kujulikana,kwa kifupi wanaojiita wasomi Tanzania hawana uchungu na rasilimali za Taifa wengi wapo kwa masilahi binafsi na michepuko yao,Maprofesa wa Tanzania ni tofauti na maprofesa wa Nchi zingine,mfano jaribu kuangalia Tabia ya Lipumba,kapuya,Tibaijuka,mbilinyi na yule PhD aliyenunua mabehewa feki na kuandaa mchakato wa Reli kwenda Airport.
Ndo maana nasema waende vyuoni wakafundishe. Na watu wa masters ndo wawe watendaji.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,842
2,000
Binafsi huwa najiuliza, hivi dhana nzima ya kujaza madokta na maprofesa kwenye safu yake ya uongozi kunaleta tija gani?
Je, hao wana utaalamu wa kutosha kufanya kile wanachotakiwa kufanya? Au ni waaminifu katika utendaji wao?
Isitoshe wengi ya hao wanaoteuliwa wametolewa kwenye taasisi za elimu ya juu hususani vyuo vikuu.
Ukiangalia idadi ya madokta na maprofesa wanaohitajika katika vyuo vikuu Tanzania ni kubwa mno.
Binafsi nawafahamu waalimu wa chuo kikuu walioteuliwa kuongoza taasisi mbalimbali. Na wengi wamebobea katika nyanja ambazo utaalamu wao unahitajika kwa hali na mali hususani kwenye kufundisha na kufanya utafuti.
Muda wa kufanya tafiti na kuandika machapisho hawataupata tena.

Ni rai yangu kuwa JPM aachane na hii kasumba. Watu anaowahitaji sana sana ni watendaji ambao sio lazima wawe na elimu ya kutisha kama hawa watu.
Hawa watu wanahitajika vyuoni mwetu ambapo kuna uhaba mkubwa wa walimu na watafiti.
Madokta na Maprofesa ninaowaamini ni wa kutoka Ulaya, Asia na Middle East ( hasa Israel ) tu pekee ila wa huku Afrika hasa hapa kwetu Tanzania nadhani hata Mimi mwenye Elimu yangu ya kutukuka kabisa ya darasa la Saba ( 7 ) ninawazidi kwa mambo mengi / vitu vingi.
 
Blood of Jesus

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
1,220
2,000
Hawa maprof & ma dr ni mizigo serikalini (kiutendaji) ; hata huko mavyuoni wako hovyo tu. Binafsi sijaona mchango chanya wa kutosha wa hawa wasomi wetu. Kuna sehemu tulikosea (Tz kama nchi) kama kuna kalaana flani. - bado hatujaweza kula mema ya nchi!

La msingi nadhani ni KUTUBU na kumrudia Mungu.
 
mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,203
2,000
Mkuu amekariri kanda ya ziwa wamezoea kujisifia elimu ambayo wala hawawezi kuitumia, bora akae kijiweni kapiga suti na kujiita profesa hata kama hazalishi kuliko kuingia mtaani kufanya umachinga na ukulima uzalishe mali, watu hawa wamejaa sifa ya kujiita mimi ni fulani wala haina tija yoyote kwa taifa na ndio maana hata waziri wa viwanda ni msomi lakini ameshindwa kuandaa mazingira ya kiwanda hata kimoja amebaki kutoa povu tu kuwa wao wanaanda mazingira lakini viwanda vijengwe na wengine mazingira yenyewe hayaonekani zaidi ya kuongea tu, kama ishu ya Dangote alitoka povu sana eti sungura anajengwa sijui wapi huko, twiga inazalisha, simba anaunguruma ovyo kabisa alijidai haoni impact ya Dangote kufunga, usomi wa kukariri ni janga kwa taifa.
 
Dr. Msafiri

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
471
250
Ufanisi wa hawa wasomi wazamivu kikazi ili kusogeza mbele maendeleo ya Taifa yatathibitisha Viwango vya elimu Tanzania!
Vinginevyo mh!
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
40,330
2,000
Nilipokuwa mdogo nilikuwa nadhani mtu akiitwa Professa au Dokta
maana yake 'ana elimu kubwa sana'
au anajua 'maambo meengi sana'

Kumbe ni tofauti.....
Actually proffesa au mtu mwenye PhD ni yule ambae
kwenye taaluma yake fulani amesoma zaidi au kufanya tafiti zaidi

Hii ina maana mtu mfano kasomea udaktari wa mifugo
akija kuwa professa sanasana anakuwa ana specialize na kitu kimoja tu
kwenye masuala ya afya ya mifugo
tena wala sio afya ya mifugo kwa ujumla....
labda Phd yake inahusu nutrition only..

Sasa mtu huyu kweli unakuja kumpa uwaziri wa Afya si unamuonea?

masuala ya management uzoefu ni kuhimu zaidi
na sio tu kila mwenye Phd basi ni manager
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom