Sabayi
JF-Expert Member
- Dec 4, 2010
- 2,310
- 991
Gazeti la Mwanahalisi lilikuwa linamilikiwa na Saed Kubenea lilifungiwa miezi kadhaa iliyopita kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi iosipokuwa tu uchochezi kufuatana na barua aliyoandikiwa na idara ya Maelezo.
Barua haikueleza ni uchochezi upi isipokuwa tu inaaminika kutokana na habari gazeti lilikuwa likiandika kuhusiana na kutekwa na kuteswa Ulimboka.
Mwanahalisi lilianza kufanikiwa kupata undani wa wa kutekwa na kuteswa kwa mwanaharakati huyo kwani kidole kilianza kuonyesha Ikulu kwa maana afisa mmoja wa usalama (TISS) ndiye mhusika mkuu.
Baada ya kufungiwa Jujwaa la Wahariri (TEF) lilimuona Kubenea ni mkosaji kwa kuandika habari zile na lilimtaka akubali kosa kwa kuandika habari ambazo wengi wa wajumbe wa TEF katika kikao kimoja waliona ni za majungu na wengine hata kudiriki kusema Kubenea alikuwa anakwenda kinyume cha maadili ya uandishi.
TEF ilimtaka Kubenea ashirikiane na Jukwaa hilo ili kumuombea kwa serikali gazeti lifunguliwe mradi tu kwanza akubali hilo kosa lake.
Kubenea aliipuuza TEF kutokana na msimamo wake huo wa ajabu na alikuwa anasusia vikao vyake.
Sasa hili la Kibanda limetokea ni kama lile lile la Dr Ulimboka ikizingatiwa ile pattern ya tukio. Sasa sijui TEF watawapinga wote wale watakaokuwa wanaandika habari kwa undani za kuteswa kwa Kibanda kama habari hizo zinaonyeshea kidole wahusika ambayo inaaminika ni wale wale waliomfanyia unyama Ulimboka?
Kwa maneno mengine ni kwamba iwapo wahariri watagundua ukweli kuhusu kuteswa kwa Kibanda watatakiwa kufunga midomo yao?
Kwa mtazamo wangu naona Kubenea amewaumbua sana TEF.
Nawasilisha
Umejidhirisha kuwa Great thinker
Kubenea aliandika ukweli mtu kwenye ile Makala lakini serikali imemfungia kwa ukweli wake