Kutesa Kwa Zamu- Ikulu

Samahani kwa mtoa hoja nimekuwa msomaji mzuri hapa ofisini kwangu watu hafanyikazi asubui kabla hawajasoma hapa hii Jambo Forum imekuwa bora kuliko magazeti.

ninaoba nijiunge na nyiye hapa ni wape maoni yangu kama mtaniakikishia usalama wa maisha yangu na familia yangu na kaumri pia kamesogea nimechoka na kunyenyekea watoto wasiyokuwa nanizamu kwa wazazi wao kwa sababu ya madaraka mimi siyo mwana siasa mimi nimesoma ninaelemu nzuri ndiyo sababu wakanipa kazi nipo kwenye nafasi kubwa na mengi machafu ninayo mezani kwangu, jamani simnajua nikiandika kisomi itakuwaje nyiye mnachotaka ni ujumbe ufike ''usiangalie kiswahili changu''nitatoa na ushaidi wa copy kama mtahitaji.

ninaomba samahani niliingia bila kukaribishwa kama mwanaJF MTANZANIA kunikumbusha asante nina kushukuru sasa ninaomba kutoa hoja

Huruma

hivi unajua kama hakuna anayesoma IPPMEDIA.COM wala magazeti ya Tanzania siku hizi?

zaidi ya hayo karibu sana na ujaribu kusoma mada zilizopita na utaona kuwa pamoja na tofauti zetu za kimawazo humu ndani sisi bado ni wamoja kwen ye mengi tuu

NIMEONA "Nyoka" kama wawili humu ndani wananusa nusa....

Mbona tunashinda nao kutwa humu. Wao ni watu kama sisi, msifikiri hawana huruma na nchi hii, jamaa wapo na wanajua kwanini wakuharibie raia mmoja mpiga debe tupu ambaye kura yake ni almost hakuna?

Ni wabongo wangapi wanasoma internet? ni wabongo wangapi wanafanya kazi maofisini? humu wote hatuzidi elf 5 believe me, ambayo ni asilimia 0.0000000.... ya wapiga kura.

Wapiga kura wapo vijijini, na ukitaka kujua hawaelewi nini kinaendelea angalia walivyopiga kura kwenye UDIWANI.

Na wale wa mjini walio wengi angalia walivyojitokeza kumlaki JK kuwa kashinda uenyekiti ambao alikuwa anagombea pekee yake!

Hapo ndio utajua nini kinaendelea TZ. Hapa tunatayarisha kizazi cha mwaka 2025 ambacho ndio kitaondoa CCM madarakani au kukimegua CCM vipande vipande!

Anyway GROUND WORK ni muhimu... Tujitahidini!
 
FD,

Maneno yako ni mazito na machungu lakini ni ya ukweli.

Kitu kimoja natahadharisha though wale wanaofurahia umaarufu wa ccm vijijini ni hili. Hali za maisha ya watu vijijini zinadumaa na hiyo si sign nzuri. Watu wa vijijini wakiendelea kuwa nyuma hivi na kuwa marginalized like this matokeo yake ni mabaya.

Angalia vita vya ndani vilivyotokea kwa majirani zetu Rwanda, Congo, Burundi, Uganda, nk kisha ujibu maswali haya. Hivi hao rebels walianzia mijini au vijijini? Ilikuwaje rahisi kwa rebel leaders kupata wafuasi?

Jibu rahisi ni kuwa, makundi yote hayo yalijengeka vijijini ambapo watu wengi wamekwisha kata tamaa. Kama ccm itaendelea kushinda kwa kutumia nguvu ya watu walioko vijijini at the same time ikitumia mabilioni kujenga majengo ya BoT huku hao wapiga kura wake wakifa kwa njaa na magonjwa yanayotibiwa, basi ccm itabidi ijilaumu yenyewe siku hao wajinga wa vijijini wakichoka na maisha.

hili pia litauma masikioni mwa wengi ila ni ukweli.
 
ahhhh, now i get it ! i see people getting sympathetic now ! GREAT !

Kuna wakati fulani hali ya siasa nchini haikuwa safi na hiyo lazima tukubali, na pale kipindi kile watu walikuwa wakishangilia sana, LAKINI SIDHANI KAMA WALIJUA LONG TERM OUTCOMES ZAKE !

lakini anyway, tuweni pamoja, tukosoe pale viongozi wanapohitaji kukosolewa, tunapongeze pale wanapostahili !

Shukrani !
 
FD,

Maneno yako ni mazito na machungu lakini ni ya ukweli.

Kitu kimoja natahadharisha though wale wanaofurahia umaarufu wa ccm vijijini ni hili. Hali za maisha ya watu vijijini zinadumaa na hiyo si sign nzuri. Watu wa vijijini wakiendelea kuwa nyuma hivi na kuwa marginalized like this matokeo yake ni mabaya.

Angalia vita vya ndani vilivyotokea kwa majirani zetu Rwanda, Congo, Burundi, Uganda, nk kisha ujibu maswali haya. Hivi hao rebels walianzia mijini au vijijini? Ilikuwaje rahisi kwa rebel leaders kupata wafuasi?

Jibu rahisi ni kuwa, makundi yote hayo yalijengeka vijijini ambapo watu wengi wamekwisha kata tamaa. Kama ccm itaendelea kushinda kwa kutumia nguvu ya watu walioko vijijini at the same time ikitumia mabilioni kujenga majengo ya BoT huku hao wapiga kura wake wakifa kwa njaa na magonjwa yanayotibiwa, basi ccm itabidi ijilaumu yenyewe siku hao wajinga wa vijijini wakichoka na maisha.
hili pia litauma masikioni mwa wengi ila ni ukweli.

watu waliochelewa kupata teknolojia thats how you refer them to as ??
no, no ! please rephrase that !
 
NIMEONA "Nyoka" kama wawili humu ndani wananusa nusa....

Mmmmhhhhh!!!! hapa siku hizi ndipo wanaposhinda usalama wa taifa, tatizo tu kwao ni vihiyo wa technologia hii mpya.

Walijifanya wana uwezo wa kumkamata mtu wa great stuff, lakini wapi, wametoka kapa.
 
huruma alikuja kubeep nini ?

NO!

huruma yuko verious na alichosema.

So far nimeona makubwa. Kaa mkao wa kula utapata mambo muda sio mrefu. So far ameongezewa protection ya hali ya juu kabisa kwenye system zake zote za mawasiliano na atatuma chochote labda MOSAD tu ndio wanaweza kumtrace.
 
Hivi usalama wa taifa wakishinda hapa, ina maana wanataka kukamata watu "wanaopinga" serikali au wanasoma tuu ili kurahisisha kazi zao za data collection nakujua wananchi wanaonaje utendaji wa serikali?

Alafu Mwafrika wa kike vita vya Rwanda, Burundi, na Uganda vilikuwa vya ukabila zaidi na uchu wa madaraka sio wananchi kuchoka(as far as I know)
 
Endelea kujifariji na hiyo generalization.
Swali la kujiuliza ni kuwa, ilikuwaje rahisi hivyo kurecruit watu wengi hivyo na wakapigana for that long. Watu wenye life na things going in their lives huwa hawakubali kupigana hovyo bila sababu ya msingi.

Fuatilia hata USA uone kuwa baada ya vita ya Iraq, Jeshi limepata kazi sana kupata watu wanaojiunga na imebaki kuwa namba kubwa ya wanaojiunga jeshi USA ni blacks, Latinos au poor whites. Jiulize ni kwanini kisha uone how easy it is kupata wanajeshi kama watu wamekuwa masikini wa kutupwa!
 
It is a pit in many places of the world that ignorant people in the rural villages are always exploited for political gains! Many politicians in the world have achieved gains through such ignorant people!

Remember politics is dirty game! To realize true justice- it is immoral to exploit poor and ignorant people!
 
CHIEF HURUMA.
Karibu sana JF hapa JF kwani ndio sehemu pekee ya kutoa dukuduku lako lakini kumbuka usije toa vitu ambavyo huna ushahidi navyo we need very clear and crucial evidence kwenye hoja yako na kama you think kuna kitu kinatokea just tell us then watu wafanyia utafiti.
Thank you once again for joining JF
 
Jamaa amenitumia PM anasema kesho asubuhi sana ataweka vitu vya ajabu hapa, ila ana wasiwasi kama JF haitafungwa; nami nimemhakikishia kuwa JF ni immortal kama alivyokuwa Mzee Punch!
 
Jamaa amenitumia PM anasema kesho asubuhi sana ataweka vitu vya ajabu hapa, ila ana wasiwasi kama JF haitafungwa; nami nimemhakikishia kuwa JF ni immortal kama alivyokuwa Mzee Punch!

Umenikumbusha mbali sana Kitila,
For sure JF ni moto wa kuotea mbali. Mkuu huruma mwaga mavituuuuzi!
 
Jamaa amenitumia PM anasema kesho asubuhi sana ataweka vitu vya ajabu hapa, ila ana wasiwasi kama JF haitafungwa; nami nimemhakikishia kuwa JF ni immortal kama alivyokuwa Mzee Punch!

Basi bwana kama ni mpaka kesho, nami kwa leo na-log out hadi hiyo kesho, manake hapa leo nilikuwa nasubiri huruma ya huyo Huruma. Natumaini kesho Huruma atatuonea huruma na hatatushindisha njaa.
 
HAO WATU WA IKULU WALIOCHOKA WAKO WENGI...TATIZO WATU WA IKULU WALIOSOMEA KAZI HADI ISRAEL et AL..wameachwa njia panda ,wajinga wajinga waliokuwa ma informer ucwara wasio na elimu ya intelegensia wamepewa sehemu nyeti...wakati kazi hawajui...tarajieni kupata habari nyingi kutoka kwa WATU WENYE UCHUNGU NA NCHI YAO....

kama alivyosema mmoja hapa HURUMA na wenzako kuficha identity hadi kwa mkeo/yeyote ni muhimu...usiamini compyuta za hapoi ofisini kwani ITY manager anauwezo wa kujua anachofanya kila mmoja wenu ..au akaangalia badaye kupitia server....ni muhimu kuwa na laptop usiyoitumia kazini...na zaidi jivinjari internet cafe za uswazi kwa raha zako...karibuni wajameni...

wataalamu wa IT hapa wapo watakuwa mara kwa mara wanatoa ushauri ili kuwalinda members wasipoteze source.
 
kitila kama vitu ni vikali sana arushe kwa walio ulaya au america kwa sasa kupitia PM wavimwage..au kwenye cafes ..nafikiri umempa ushauri maridhawa......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom