Kuteremshwa(kushuswa)kwa mishahara, inakubalika kisheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuteremshwa(kushuswa)kwa mishahara, inakubalika kisheria?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Remmy, Jul 17, 2012.

 1. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Tafadhali wanasheria tunaomba msaada hapa.
  Kuna jambo limetokea kwa ngazi moja ya ajira serikali kuu. Awali ngazi hii ilikuwa ya kimadaraka zaidi hivyo MISHAHARA ilikuwa mikubwa kulinganisha na kazi zingine. Ilipofika mwaka 2003 ngazi hii ilirudishwa kuwa Kama utumishi wa kawaida ila sijui ni bahati mbaya au njema hawakushusha ngazi ya mshahara. Hivyo mpaka 2008 watu waliajiriwa kwa mshahara mkubwa.
  Sasa imekuja barua ya kuwashusha MISHAHARA wafanyakazi hawa toka ngazi ya TGS F mpaka E, ni tofauti ya shilingi 200,000,hii itaanza kwa mwezi huu wa Saba.

  SWALI LANGU: hii iko sahihi KISHERIA? Au niseme sheria inasemaje?

  Note: wafanyakazi hawa wamekopa kwenye mabenki kwa mshahara ule wa awali, wakikatwa watakuwa na negative kwenye account zao.
   
 2. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wako sahihi. Na wale waliolipwa kimakosa walitakiwa warudishe hizo pesa kwa kukatwa kidogokidogo. TGSF inaanzia shillingi ngapi mkuu?
   
 3. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,012
  Likes Received: 3,197
  Trophy Points: 280
  Mi nikafikiri kuteremshwa kwa aya.
   
 4. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  mi naona serikari haiko sahihi.Kilichotakiwa kufanyika ni kuacha kufanya nyongeza ya mshahara mpaka hapo wenzao walioanza na TGSF watakapowafikia la sivyo wawapeleke kwenye majukumu yanayoendena na mishahara wanayopokea sasa
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kimsingi MISHAHARA hiyo iligota, haipandi mpaka sasa walipoamua kuwashusha.
  Sasa can they go to court agaist govt?
   
 6. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mmmm.....
  Mkataba wa ulisema ngazi hiyo? Kosa ni Lao.
  Unatakaje nikitaja pesa.
   
 7. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mshahara uliotolewa kutokana na sheria halali ya wakati huo hauwezi kupunguzwa hata kama mhusika ameshushwa cheo!
   
 8. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Barua toka kwa katibu mkuu utumishi za kushusha mshahara zimewafikia.
  Je wanaweza kwenda mahakamani?
   
 9. A

  ARDEAN Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Nitaanza kwa kusema kwamba kilichofanyika sio sahihi. Kabla hatujaenda kwenye vifungu vya sheria Civil Service Act, 2003 na pengine Employment and Labour Relations Act, 2004 ili kuona kama Mwajiri anayo mandate ya kushusha mshahara wa mwajiriwa, tujiulize haya:

  Kwamba, ajira ni mkataba/ makubaliano kati ya mwajiri na mwajiriwa. Mwajiri alipotangaza kazi alitoa sifa na pengine masharti ya ajira. Mwajiriwa akaona kuwa anazo sifa, akaomba kazi hiyo. Akasahiliwa na kufaulu. Baada ya hapo, bila shaka alipewa barua ya kufaulu kwake na kuonyesha kuwa amekubaliwa kuajiriwa. Barua hiyo ndio inatoa masharti ya ajira ikiwemo malipo (yaani mshahara). Kwa stage hii, muomba kazi halazimishwi au halazimiki kuajiriwa. Anaangalia masharti ya ajira yenyewe lakini kikubwa anaangalia mshahara (How much do you offer me). Hiki ni kigezo kikubwa sana cha mtu kukubali kuajiriwa. Inawezekana kuwa wakati wa ajira hii, mtu alishwahi kupata offer nyingine mahali pengine. Kwa kulinganisha mishahara ya sehemu mbili tofauti, bilashaka unachagua sehemeu iliyonona kidogo. Mtu huyu (Mwajiri) akikubadilikia kesho na kutoa mshahara tofauti atakuwa amekuumiza na kukupotezea opportunities za mahali pengine.

  Hivyo basi, kwa mantiki hiyo, Mwajiriwa hawezi kukurupuka na akasema leo nashusha msharahara wako bila kukushirikisha na wewe ukatoa idhini au maoni yako. Akifanya hivyo, atakuwa amevunja mkataba wa ajira na atakuwa amekiuka sheria na hata katiba ya nchi. Mwajiriwa hana budi kuchukua hatua.
   
 10. C

  Cartoons Senior Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  that's true.
   
 11. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160

  Asante sana mkuu kwa mawazo.
  This is silly government.
   
 12. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  hapa panahitaji wataalamu wa masuala ya sheria za kazi ili waweze kuwasaidia
   
 13. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakikatwa wasihesabiwe wakati wa sensa
   
 14. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Wameamua kutokufanya kazi kwa ufanisi. Na watatoa huduma kwa ulegevu tena kwa malipo.
   
Loading...