Kutengwa kwa wafuasi wa katoliki S/wanga, Ukweli umebaki pale pale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutengwa kwa wafuasi wa katoliki S/wanga, Ukweli umebaki pale pale

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Aikaotana, Dec 25, 2010.

 1. A

  Aikaotana Senior Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ile kauli eti tatizo ni mgombea wa CCM kuuelezea utatu katika hali ya kisiasa ndio iliyofanya waumini waliomuunga mkono watengwe proved not correct, ni propaganda tu za kanisa!

  Ukweli unabaki palepale kwamba waumini wa kanisa katoliki Sumbawanga kama ilivyokuwa kwa nchi nzima walikataa maagizo ya kanisa ya kumnyima kura mgombea Ubunge wa CCM (Muislamu)na kumpa wa Chadema(mkristo), soma article ya mwanachi between the lines leo tarehe 25/12


   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  JK amesema kuna UDINI, tuweke wazi tatizo tujadili huenda likakwisha...

  Mficha maradhi mauti itamuumbwa, iko Tanzania itaumbuliwa na maradhi ya UDINi
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyo mwislamu ana nini mpaka awafukuzishe watu kanisani? Mbona hatujaona sehemu ambako waislamu wamegombea na kushinda wakristo wakifukuzwa kanisani? Watu wengine hamna vitu vingine vya kufanya mpaka mlete vitu visvyo na maana?
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama udini upo JK atuambie uko maeneo gani kuliko kutoa kauli za jumla jumla na kuziacha hewani bila kufafanua!
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Maeneo si ndiyo kama hayo hapo juu chagua mtu wa dini yako tu...au ulifikiri ni siri siri imefichuka
   
 6. A

  Aikaotana Senior Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  specifically s wanga ndio mfano wa udini ulioasisiwa na kanisa uchaguzi uliopita, hujui? halafu hao hao wanaibuka na kusema hakuna udini watu wa ajabu hawa!
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo jk kachaguliwa kwa sababu ya dini yake na pia waislamu wengine wamechaguliwa kwa sababu ya dini zao? Sasa kama ndio hivyo wanacholalamikia ni nini hasa?
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Dec 25, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama JK angejua siri asingeuma maneno kwamba kuna udini tu kaachia hapo, ila ushetani uitwao kadhi na oic anaona sio udini!
   
 9. T

  Topical JF-Expert Member

  #9
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kadhi na oic haitakuwepo bana maaskofu hawataki siku wakikubali itakuwepo

  Udini upo ndio maana wanaofaidi nao wanapinga

  mawaziri 33 vs 17 vipi utakubali udini upo ingekuwa oppsite udini ungekuwepo ok.

  Mna bahati JK anawaogopa sana maaskofu...
   
 10. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #10
  Dec 25, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Umekuja huku tena kuhesabu vizibo vya mawaziri waislam na wakristo tutolee udini wako tena ukome kabisa.
   
 11. A

  Aikaotana Senior Member

  #11
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hujui! we unaishi nchi gani? nenda ofisi zote za umma na taasisi za umma, utaukuta huko umeota mizizi
   
 12. A

  Aikaotana Senior Member

  #12
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunajua kwa nini hamtaki kukiri udini upo kwa sababu unawanufaisha
   
 13. A

  Aikaotana Senior Member

  #13
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  crap , kaishiwa hoja huyu
   
 14. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #14
  Dec 25, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha watengwe tu. Kanisa katoliki lina misingi yake ambayo ukitaka kuwa member lazima ufuate. Sharti ktk al queda ni kuua watu wakati katika RC ni upendo na kuheshimu utatu mtakatifu. Mbona sijasikia Mpanda Maaskofu wamefukuza mtu kwa kuchagua wapagan wa kiislam au mbona sijasikia Bukoba mjini askofu wamefukuza muumini?

  Achana na scapegoat kushindwa kwa CCM ni kwa sababu ya ufisadi na incompetence.
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wapi utakaponikataza ndio na enjoy uhuru wetu kwenye katiba yetu...labda hiyo mpya ndio itunyime...udini ni tofauti na ukweli

  eti ukome, hiyo lugha ya walokole ...uhuru mkuu...usihofu kusikia ukweli udini upo
   
 16. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #16
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 3,620
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Usidanganye watu. Maelezo sahihi ni kama yalivyotolewa katika gazeti la mwananchi:

  Waumini RC Rukwa 'wakiri' kukashifu

  Saturday, 25 December 2010
  Na Geofrey Nyang'oro, Sumbawanga

  KUTENGWA kwa waumini wa Kanisa Katoliki wilayani Sumbawanga ambao walitengwa mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kunaweza kuhusishwa na masuala ya kisiasa, lakini imebainika kuwa walinajisi kanisa katika kusherehekea ushindi wa kisiasa, Mwananchi inakuthibitishia.

  Habari za kutengwa kwa waumini hao zilihusishwa sana na purukushani za uchaguzi mkuu na ilidaiwa kuwa walitengwa na kanisa kutokana na kujihusisha na chama tawala cha CCM, lakini Mwananchi ilifanya utafiti na kubaini kuwa waliofungiwa wengi wamegundua kosa lao na sasa wanalijutia
  .

  Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Sumbawanga mkoani Rukwa umebaini kuwepo kwa vitendo vya kukashifu imani ya Kikristo vilivyofanywa na baadhi ya waumini hao wakati wa kampeni na baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 31.

  Mwananchi imebaini kuwa waumini hao walitengeneza jeneza na ndani yake wakaweka mgomba na sanamu ya kanisa na msalaba wake na baadaye kulizika jeneza hilo.

  Tukio hilo lilifanyika katika kijiji cha Chelenganya kilicho umbali unaokadiriwa kuwa ni zaidi ya kilometa 20 kutoka yalipo makao makuu ya Manispaa ya Sumbawanga.

  Muumini mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alilimbia gazeti hili kijijini hapo kuwa siku ya tukio baadhi ya waumini walitengeneza jeneza na kuweka mgomba ndani yake pamoja na sanamu ya kanisa na msalaba baadaye kufanya ibada ya mazishi, kitu ambacho kinaonekana kuwa ni kuikashifu imani ya Kikristo.


  Alisema kibaya zaidi ni kitendo cha waumini hao kuingia kanisani wakiwa na jeneza hilo na kuendesha ibada ya mazishi kabla ya kwenda kulizika jeneza hilo.

  Alisema mgomba ulitumika kama ishara ya kumzika mgombea wa Chadema, Norbet Yasebo wakati waliweka msalaba na kanisa kama ishara ya vilitabiriwa kama mazishi ya kanisa hilo ambalo inadaiwa kuwa lilikuwa likimuungano mgombea huyo wa chama cha upinzani.


  Lakini waumini hao sasa wanajutia kitendo chao.


  Wanajitetea kuwa walifanya hivyo bila kujua kuwa walikuwa wakifanya kosa kubwa kwa kanisa lao; walifikiri wapo kwenye shamra shamra za kusherehekea ushindi wa mgombea wao.

  "Hatukujua kama hili tulilokuwa tukilifanya ni kosa, bali tulikuwa tukisherehekea ushindi wa mgombea wetu ambaye alishinda katika uchaguzi huu," alisema mmoja wa waumini hao waliotengwa kijijini hapo huku akitaka jina lake lisiandikwe gazetini.

  Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Sumbawanga, Charles Kabanga alithibitisha kuwepo kwa waumini wa kanisa hilo waliotoa kashfa kwa kanisa na mapadri wao wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31.


  Kabanga, ambaye naye ni miongoni mwa waumini wa kanisa hilo waliotengwa kutokana na madai ya kuhusika katika vitendo hivyo, alisema wakati wa kampeni aliwashuhudia baadhi ya Wakristu wakitoa kashfa kwa mapadiri hao kwa madai kuwa wanamkashifu mgombea wao wakati wao pia wana mapungufu yao.

  Alisema waumini hao, ambao wengi ni wajumbe wa CCM, waliwataka mapadri kuwaachia suala la kisiasa na kwamba wandelea na kazi yao ya kuhubiri neno la Mungu.

  "Wanaosema mimi nilihusika na kitendo cha kuwakashifu na kuwatukana mapadri wangu wananionea," alisema Kabanga.


  "Kilichotokea ni kwamba nilikuta baadhi ya wajumbe CCM ambao pia ni waumini wa kanisa hilo wakisema mapadri wanamkashifu mgombea wetu kuwa ana tabia mbaya wakati wao wana mapungufu mengi," alisema Kabanga akiwanukuu waumini wenzake.

  "Ndipo nilipoanza kuwatetea mapadiri wangu na kuwaambia watu hao waache kuzungumza hayo kwa kuwa sote ni wakirstu swa Kanisa Katoliki na hao ni mapadiri wetu ambao hutupatia huduma za kiroho. Niliwaambia kuwa hata wakisema hivyo leo, padri ni padri na ataendelea kuwahudumia," alisema Kabanga.

  Alisema katika mkutano huo aliwaomba waumini wenzake kuacha kuwakashifu mapadiri, badala yake kuendelea kufuata misingi ya imani ya kanisa hilo huku wakisikiliza mafundisho yao na kuacha kufauata matendo wanaoyofikiri yapo kinyume na mwenendo na maadili ya mapadri hao.

  Kuhusu suala la mgombea wa CCM kukufuru utatu mtakatifu, yaani Mungu, mwana na roho, Kabanga alikanusha kuwepo na kitendo hicho na kueleza kuwa kauli zake zilitafsiriwa vibaya.


  "Alichosema mgombea wetu ni kuhamasisha wanachama na wapenzi wake kuchugua mafiga matatu, mafiga matatu ambayo ni rais, mbunge na diwani na si vinginevyo," alisema Kabanga.

  "Hata hivyo sisi kama chama tulimwita mgombea wetu na kumsihi kuacha kutumia maneno ambayo yanagusa imani kwenye kampeni zake," alisema Kabanga.

  Kuhusu kutengwa kwake, Kabanga alisema uamuzi huo unamuuma na kumkosesha amani katika maisha yake ya sasa.


  "Hata ninapokuwa njiani nikitembea, najisikia vibaya kwa jinsi waumini wenzangu wanavyoniangalia na jinsi wanavyozungumzia kuwa nimetengwa na kanisa," alisema.

  Naye Chiritina Ninde, ambaye pia ametengwa na kanisa hilo, aliimbia Mwananchi kuwa mgombea wa chama hicho katika kampeni zake aliwataka wapiga kura kuchagua mafiga matatu ambayo ni rais, mbunge na diwani akirejea maandiko ya kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia kuwa kuna nafsi tatu ambazo ni Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu ambazo Kikristo hutafsiriwa kuwa ni kitu kimoja.


  Ninde, ambaye haruhusiwi kushiriki ibada, kupokea sakaramenti na huduma nyingine za kiroho zinazotolewa na kanisa hilo kutokana na kutengwa, anasema adhabu hiyo inamuumiza sana.


  "Inauma sana mtu kutengwa na jumuiya uliyokuwa ukishiriki nayo katika kila kitu leo siruhusiwa kushiriki ibada wala kuhudhuria mazishi ya ndugu wala jamaa yangu ambaye kanisa litahusika... kwakweli hadi sasa sielewi cha kufanya," alisema huku akionyesha barua aliyokabidhiwa na kanisa la hilo Parokia ya Kirstu Mfalme Desemba 17.

  "Mimi nimezaliwa na kudumu katika imani ya kanisa katoliki hadi sasa. Sijawahi kusikia tukio kama hilo tangu kuzaliwa kwangu na wala sikutegemea kama ingefikia siku nikatengwa na kanisa."

  Baadhi ya waumini walilimbia gazeti hili kuwa chanzo cha mgogoro huo ni kitendo cha kanisa hilo kutoa elimu ya uraia wakati wa kampeni, likihamasisha waumini wake kuchagua viongozi bora.


  Lakini elimu hiyo ilichukuliwa na wanachama wa CCM kuwa ililenga kumsaidia mgombea wa Chadema ambaye ni Mkristo.

  "Kila mara mapadri walitumia muda mwingi kuhamasisha waumini kuchagua viongozi bora huku wakitoa sifa za mtu anayefaa kuwa kiongozi. Lakini sifa hizo zilionekana kumhusu mgombea wa Chadema jambo lililowafanya waumini hao kutafisiri kuwa mapadiri wanaipendelea Chadema," alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Joseph.

  Akizungumzia hilo, Wakili wa kiaskofu wa kanisa hilo mjini Sumbawanga, Padri Modest Katonto alisema kanisa lilikuwa likitimiza wajibu wake wa kutoa elimu ya uraia kwa waumini wake kuhusu uchaguzi na wala halikupendelea chama chochote.

  "Katika kipindi hicho kanisa lilitoa elimu ya uraia kwa waumini wake sambamba na kukemea vitendo na mwenendo mbovu, na wala halikupendelea chama chochote cha siasa. Madai ya baadhi yao kuwa tulipendelea chama ni uzushi na uongo," alisema Katonto.


  Alisisitiza kuwa kanisa litaendela kufundisha waumini wake juu ya kuwajibika katika kutenda mema.

  Katika uchaguzi wa mwaka huu, mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Aeshy Hilaly aliibuka mshindi dhidi ya Yamsebo wa Chadema ambaye pia walikumbana kwenye kura za maoni ndani ya CCM kabla ya kuhamia upinzani.

  Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa Kanisa Katoliki Sumbawanga lilitangaza kuwatenga waumini wake wapatao 27 na kuwasimamisha waumini wengine zaidi ya 400 kwa madai ya kulikashifu kanisa na kukufuru.


  Padri Katonto alitaja makosa yaliyolilazimu kanisa kufikia hatua hiyo kuwa ni pamoja na baadhi ya waumini kukufuru matumizi ya msalaba na kanisa kwa kutengeneza sanamu ya vitu hivyo na kuvizika.

  Alitaja makosa mengine kuwa ni kitendo cha baadhi ya waumini kujihusisha na matusi, kejeli na maneno ya uchonganishi kwa viongozi wa kanisa na waumini wenzao.

  Pia baadhi ya wagombea walidaiwa kujifafanisha na Mungu mwenye nafsi tatu, kitendo kinachoonekana kuwa ni kufuru kwa kanisa hilo linaloamini katika utatu mtakatifu.


  Akifafanua kuhusu adhabu hizo, Padri Katonto alithibitisha uamuzi wa kanisa hilo kuwatenga waumini 27.

  Padri Katonto alisema kwa mujibu wa sheria namba 1364 ya Kanisa Katoliki, kosa la waumini hao linawatenga na umoja wa kanisa bila ya kutangaziwa na uongozi wa kanisa.

  Katonto alisema iwapo waumini hao watakwenda kwenye nyumba za ibada, watatakiwa kuondoka na kwamba ibada itasitishwa hadi hapo watakapoondoka na zaidi ikiwa watakufa bila kutubu hawatapata maziko na kanisa.


  Alibainisha kuwa kundi la pili ni waumini waliowekewa pingamizi na kufafanua kuwa kundi hilo linanyimwa huduma za kanisa wakati makosa yake yakiendelea kuchunguzwa hadi hapo itakapobainika kuhusiaka au la.


  Alisema baada ya uchunguzi kukamilika na kubaini watuhumiwa hawakuhusika basi muumini husika anarejeshewa huduma zote za kiroho.

  Hata hivyo alisema waumini waliowekewa pingamizi ambao ni zaidi ya 400 wanaruhusiwa kuendelea kushiriki katika umoja na kanisa na si kama ilivyo kwa waliotengwa.
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ukristo unaweza kutolewa na padre?

  Anatoa nini hasa?

  Ukristo unaondolewaje na mtu? mambo mengine kuchekeshana tu...s/wanga shule hakuna nini?
   
 18. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #18
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Buchanan Uko nje ya maada kabisa, hebu rudi JF- Great thinkers. Wanazungumziwa Wapambe, wahamasishaji, viongozi na wagombea ambao wanapiga propaganda za kuchagua kutokana na dini.

  Hapa hawazungumziwi wachaguaji ambao wao bado hawana udini na ndio maada ya thread hii. Soma between the lines utagundua kuwa huo ndio ujumbe mkuu.

  Jamani sio utani, kwa mnaoshabikia udini hamuelewi madhara yake. TUACHANE NA UDINI, TUZINGATIE MAENDELEO YA NCHI YETU.

  Ukweli ni huu: Nchi abayo ina asilimia 30 wakristo, 35 waislamu na 35 ni dini nyinginezo ikiwa pamoja na zile za asili huwezi kulitenga kundi lolote lile kati ya hayo. Utatuzi wake ni kuweka udini pembeni na kuishi wote kama ndugu kama tulivyoishi huko awali.
   
 19. A

  Aikaotana Senior Member

  #19
  Dec 26, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndio maana nilisema you need to read between lines, Kwanza unajua kwa nini Mwandishi ameandikan neno kukiri kutumia inverted comas?

  pili Mwandishi anaonesha biazness kwa ajili ya imani yake ambapo ameeleza maneno ya hearsay kama anauhakika nayo vile! ukichunguz a habari yake imelenga kulidefend kanisa lakini katika uandishi msomi mzuri utagundua loopholes za ukweli alizoziacha,kwanza kwa nini Mwanachi ilienda kufanya uchunguzi Swanga wakati hii issue ilikuwa imepita!

  Kumbuka pia msimamo wa gazeti hili wakati wa uchaguzi wa kuandika mabaya ya serikali na kuficha mazuri yote au kutoyapa kipaumbele!

  Ukisoma kuna hearsay ya mgomba kuingizwa na kuswaliwa kanisani zina doubt, suala la kutengeneza jeneza na kulibeba ni mambo yaliyozoeleka kwenye siasa , tena vyama vya upinzani ndio vinara wa kutengeneza majeneza ya kuizika CCM.

  Maeneo mengi ya mjini hata kama mgombea wa CCM ni mkristo hatukusikia padri wa maeneo husika akilalamikia wafuasi wa CDM kuizika CCM. bado ukweli unabaki kuwa kanisa LILIMPIGIA KAMPENI WAZIWAZI MGOMBEA WA CHADEMA, WANANCHI (WAKIWEMO WAUMINI WALIOSHAWISHIWA) WALIKATAA NA KUMPIGIA WA CCM, PADRI AKACHUKIA KWA WAUMINI WAKE KUKAIDI AMRI, AKAWATENGA
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Dec 26, 2010
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Umshirikina Mkubwa inavyoonyesha!!!
   
Loading...