Kutengeneza dawa ya kuku ya kutibu magonjwa yote kwa mitishamba

Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?
Hii itakua Newcastle au mdondo
 
mi nami nishare uzoefu wangu....pilipili kichaa ni kiboko chukua pilipili zitwange halafu changanya na maji iwe kali sana wape wanywe umekomesha magonjwa yote. ili wanywe vzur wafungie halafu wawekee chakula kikavu mf pumba mpaka saa nane hvi then wape maji hayo yenye pilipili. mwaka 2014 kijijin kwetu ulizuka ugonjwa kuku wote walikufa isipokuwa kwangu tu mpaka wakasema mi mchawi kumbe nliwapa dawa hyo baada ya kusoma jarida mtandaon
Mkuu hii pilipili kichaa inatibu ugonjwa gani
 
Yapata wiki sasa nahangaika na tatizo la Kuku kuvimba macho na kuwa vipofu kabisaa mpaka sasa ni Kuku 22 ndio wamepatwa na tatizo hilo, nimewahamisha banda kabisa ili wasichangamane na Kuku wengine wakaleta maafa zaidi nimeshajaribu kutumia antibiotics mbali mbali kama Piperazine citrate, sevin , Akheri powder kuwatibu lakini wapi yaani tatizo liko palepale kinachoniumiza zaidi hawa Kuku walishaanza kutaga na wengine ndio wanaelekea kuanza kutaga.
Kama kuna wataalamu humu naomba msaada wa cha kufanya maana mambo yanakua magumu sasa,hii ndio biashara pekee ambayo hakika haikuwahi kuniangusha sasa kama nitaanguka kwenye hii Nayo miti yote itakua inateleza kwangu hivyo chini nitaanguka
Jaribu kuchukua alovere Na umuwekee jichoni au dawa yamacho yabinadamu ko nusu wape dawa yamacho yabinadamu nusu uwape alovera uangalie ikwapi inaufanisi mkubwa
 
naongezea
chukua majani mabichi ya mwarobani yaanike kivulini au kibarazani (yasikauke kwa jua) then uje uyatwange then chanyanya kwenye chakula chao ..majani hayo yana antibaotic nyingi.

nyingine ni majani ya mti wa mlingalinga yafanye kama ulivyofanya mwarobaini ,hayo yana vitamin nyingi sana kuzidi ya kwenye aminototal
Ahsante sana
 
Back
Top Bottom