Kutengeneza dawa ya kuku ya kutibu magonjwa yote kwa mitishamba

Kuna mabwawa ya kisasa yakuhamishika na mtoto sio rahisi kutumbukia,na linahamishika sehemu yeyote ile.ukiitaji kuyaona ni pm namba yako.na vifaranga nitakupatia pia vya sato
mkuu kama unaweza kutusaidia hayo mabwawa hata kwa picha tu hapa ingekuwa njema sana!
Ni wengi tuna mawazo hayo ila changamoto kama hizo!
Tusaidie mkuu tufaidi wote kama hutojali
 
Mm sio mzoefu sana, ila Hilo tatizo kwa kumbukumbu yangu ni kama upungufu wa vitamin A......na hasa huwapata Kuku wakiwa bado wadogo kati ya wiki nne na kuendelea. Unawapa majani!? Uliwapatia mult-vitamin
Mkuu Kuku wangu waliougua ni wakubwa na nimehangaika nao kweli Jana niliamua kuwachinja wote 22 hakukua na namna
 
Mkuu Kuku wangu waliougua ni wakubwa na nimehangaika nao kweli Jana niliamua kuwachinja wote 22 hakukua na namna
Pole Sana Kwakuchukua uamuzi mgumu lakini hapo utakuwa kama umekimbia tatizo haujasovu tatizo ulitakiwa ufuatilie TIBA hadi Uone mwisho wake Na baada ya hapo Ungekuwa umejifunza kitu kikubwa sana Kwa maana ya TIBA SAHIHI Na ungekuwa mzoefu kukuwengine wasinge KUPA tabu.
 
Haya mambo yanachanganya Mkuu yaani ukilala hupati usingizi maana unawawaza kesho asubuhi nikiwakuta wamekufa itakuaje!! Nikaona ili kuwaokoa wale wengi waliobaki bora niwachinje hawa wachache ili nami niepuke hasara bora kuwauza nyama,ila shukrani sana kwa neno lako next time nitafuatilia hadi nione mwisho wa tatizo
 
Wapake mafuta ya Samli ya ng'ombe kwenye macho. kisha changanya Samli na Pumba au mahindi. Hyo nayo ni nzuri kwa ndui.
 
mkuu kama unaweza kutusaidia hayo mabwawa hata kwa picha tu hapa ingekuwa njema sana!
Ni wengi tuna mawazo hayo ila changamoto kama hizo!
Tusaidie mkuu tufaidi wote kama hutojali
Najaribu kuweka picha inakataa.nitumie namba yako nikutumie uyaone.na maelezo yake
 
Wapake mafuta ya Samli ya ng'ombe kwenye macho. kisha changanya Samli na Pumba au mahindi. Hyo nayo ni nzuri kwa ndui.
Kwa tiba ya ugonjwa wa ndui iliyomujarabu tumia vdonge vya PEN V.chukua vidonge 5 na weka kwenye maji ya Lita 1 wape wanywe ck nzma yakiisha ongeza.
Nawaambieni ndan ya ck 3 mtanipa majibu.
 
hata mimi nafuga kuku waliwahi kuugua huo ugonjwa cha muhimu ni watenganishe na kuku wazima,kisha wakwangue hayo madude ukishafanya hivo chukua maji ya vuguvugu uliyochanganya na chumvi paka mle ulimowakwangua ukimaliza hapo wapake dawa inaitwa ocucycline fanya hivo kwa mda wa week mbili utaniambiaa
Hio atumie vidonge vya pen v.hio ndo kiboko take.ndan ya ck 3 tu utaleta mrejesho
 
Niliwahi kuhudhuria hilo darasa la ufugaji wa samaki,sema mpaka Leo naona kuna ugumu kwangu kuyafanyia kazi mafunzo Yale hasa ninapofikiria kujenga Fish pond hapa nyumbani wakati nna watoto wadogo,naongopa kusababisha kilio Mkuu, wishing you Good luck katika mradi wako mpya
Mbona kuhusu pond nayo ni rahisi tu. Unaweza zungushia mabanzi au wire mesh kote na mlango kabisa, hapo mtoto haingii.
 
ForumsKilimo, Ufugaji na Uvuvi

Kutengeneza dawa ya kuku ya kutibu magonjwa yote kwa miti shamba.
Watch Thread
1234
  1. donata fredyMember
    #1
    Aug 3, 2016

    MADAWA YA ASILI YA KUKU:
    Madawa haya yanatokana na mimea na yanasaidia ktk jinga na kutibu pia. Dawa hizi tunazipata ktk sehemu za mimea yaani; majani, magome, mbegu, Maua na matunda. Umuhimu wake ni kama ifuatavyo:
    hupatikana kwa urahisi, rahisi kutumia, gharama nafuu, zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.

    Pia unaweza ukawe tengeneza unga wake na kuchanganya kwenye pumba za Kuku tazama hatua

    Hapa kwenye mlonge ni pazuri zaidi mmea huu unaitwa mmea Wa maajabu Duniani ni safi sana kwa binadamu naomba niwape kidogo. Chuma majani mateke yaanike ndani ili virutubisho visiondolewe na jua majani yakikauka yasage au twanga chekecha kupata unga
    Pia watafiti wengine wanasema unaweza ukatumia shubiri mwitu kama ifuatavyo:

    Shubiri Mwitu (Aloe vera):
    Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.

    Mchanganyiko huu unaweza kutibu: Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla kwa kinga. Homa ya matumbo (Typhoid). Mafua (Coryza). Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).

    Mlonje): Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine.

    Mlonge hutibu:
    Pia katika Dawa hiyo ya jani la mpapai unaweza ukatwanga ukachanganya na pumba kile kisamvu chake weka kiasi ambacho Kuku watamaliza siku hiyo hiyo( chakula)
    Mafua. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Homa ya matumbo Ini.

    Pilipili Kichaaondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).

    Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai
    Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi. - Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.

    Kutumia (kwa kinga) Kupambana na magonjwa ya kuku: Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi.

    Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.

    Chukua jani moja la Shubiri mwitu lenye ukubwa wa kati. Likate katika vipande vidogo vidogo. Loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi cha lita mbili. Kuku utumia maji haya kunywa yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi unapobadilisha.

    Kutumia Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku zote. Hii inafanya kazi ya kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali. Badilisha maji hayo kabla hayajaanza kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingine. Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla ya kuwawekea dawa nyingine.

    Report
    Like- 11 people likes+ QuoteReply
  2. G
    gungeleJF-Expert Member
    #2
    Aug 4, 2016

    nmekusoma mkuu

    Report
    Like+ QuoteReply
  3. Lugoba InvestmentSenior Member
    #3
    Aug 13, 2016

    Nilichotaka nimepata

    Report
    Like+ QuoteReply
  4. Frank WanjiruJF-Expert Member
    #4
    Aug 13, 2016

    Asante kwa Elimu Mkuu.

    Report
    Like+ QuoteReply
  5. black sniperJF-Expert Member
    #5
    Aug 13, 2016

    Ahsante

    Report
    Like+ QuoteReply
  6. KataviPlatinum Member
    #6
    Aug 13, 2016

    Nitaifanyia kazi hii

    Report
    Like+ QuoteReply
  7. MPEMESenior Member
    #7
    Aug 14, 2016

    Asante kwa somo lako
    Yaani namalizia kupost haya maneno naenda kuponda majani ya mpapai

    Report
    Like- 1 people like+ QuoteReply
  8. KIKAZIJF-Expert Member
    #8
    Aug 14, 2016

    Asante sana Mdau kwa nondo nzuri

    Report
    Like+ QuoteReply
  9. W
    WamalinyiJF-Expert Member
    #9
    Aug 14, 2016

    nzur sana

    Report
    Like+ QuoteReply
  10. W
    WamalinyiJF-Expert Member
    #10
    Aug 28, 2016

    MADAWA YA ASILI YA KUKU:
    Madawa haya yanatokana na mimea na yanasaidia ktk jinga na kutibu pia. Dawa hizi tunazipata ktk sehemu za mimea yaani; majani, magome, mbegu, Maua na matunda. Umuhimu wake ni kama ifuatavyo:
    hupatikana kwa urahisi, rahisi kutumia, gharama nafuu, zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.
    Pia unaweza ukawe tengeneza unga wake na kuchanganya kwenye pumba za Kuku tazama hatua
    Hapa kwenye mlonge ni pazuri zaidi mmea huu unaitwa mmea Wa maajabu Duniani ni safi sana kwa binadamu naomba niwape kidogo
    Chuma majani mateke yaanike ndani ili virutubisho visiondolewe na jua majani yakikauka yasage au twanga chekecha kupata unga
    Pia watafiti wengine wanasema unaweza ukatumia shubiri mwitu kama ifuatavyo:
    Shubiri Mwitu (Aloe vera):Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12. Mchanganyiko huu unaweza kutibu:Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla kwa kinga.Homa ya matumbo (Typhoid).Mafua (Coryza).Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
    Mlonje): Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mlonge hutibu:
    Pia katika Dawa hiyo ya jani la mpapai unaweza ukatwanga ukachanganya na pumba kile kisamvu chake weka kiasi ambacho Kuku watamaliza siku hiyo hiyo( chakula)
    Mafua. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Homa ya matumbo Ini.
    Pilipili Kichaaondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).
    Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi. - Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.
    Kutumia (kwa kinga) Kupambana na magonjwa ya kuku: Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi. Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.
    Chukua jani moja la Shubiri mwitu lenye ukubwa wa kati. Likate katika vipande vidogo vidogo. Loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi cha lita mbili. Kuku utumia maji haya kunywa yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi unapobadilisha. Kutumia Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku zote. Hii inafanya kazi ya kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali. Badilisha maji hayo kabla hayajaanza kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingine. Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla ya kuwawekea dawa nyingine.
    Click to expand...
    Mkuu nisaidie kote nimeekewa ila,Isiyotumika mwanga maana yake nn

    Report
    Like- 1 people like+ QuoteReply
  11. ARMs14Senior Member
    #11
    Aug 28, 2016

    Report
    Like+ QuoteReply
  12. NanoliJF-Expert Member
    #12
    Aug 28, 2016

    Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
    Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
    Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?

    Report
    Like+ QuoteReply
  13. ivunyaJF-Expert Member
    #13
    Aug 28, 2016

    Asante kwa somo, ili kupunguza kero kwenda kwa majirani kuchuma majani ya papai Inabidi niupande hapa home kwa matibabu ya kuku.

    Report
    Like- 1 people like+ QuoteReply
  14. Miss NatafutaJF-Expert Member
    #14
    Aug 28, 2016

    Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
    Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
    Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?
    Click to expand...
    kuhusu mafua wape piriton ni dawa nzuri sana kwa kuku

    Report
    Like- 1 people like+ QuoteReply
  15. EvarmJF-Expert Member
    #15
    Sep 2, 2016

    Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
    Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
    Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?
    Click to expand...
    Hata dawa za tiba kwa binadamu, ukiwapa kuku wanapona bila ya Shida.

    Report
    Like- 4 people likes+ QuoteReply
  16. PdidyJF-Expert Member
    #16
    Sep 2, 2016

    Hata dawa za tiba kwa binadamu, ukiwapa kuku wanapona bila ya Shida.
    Eg argumentin

    Report
    Like+ QuoteReply
  17. N
    nezytheeMember
    #17
    Sep 3, 2016

    Mkuu nisaidie kote nimeekewa ila,Isiyotumika mwanga maana yake nn
    ukiwaekea kuku hayo maji/dawa na wakashindwa kuimalza kwa siku husika,imwage ili kesho uweke nyingne

    Report
    Like- 1 people like+ QuoteReply
  18. ARMs14Senior Member
    #18
    Oct 8, 2016

    Wakuu Leo naomba nami niongezee kitu hasa kwenye dawa za kuku wa kienyeji.ni cku nyingi sana nimefuatilia dawa ya alovera nimegundua ni dawa sahihi ila alovera iliyonipa mafanikio siyo ile chungu la ni ile isiyo chungu mara nyingi iinapatikana porini.nimeijaribu mara nyingi kwa kuku wagonjwa imenipa mafanikio naombeni nanyi muijaribu. Nami baada ya kugundua nimepanda kwa hom.Picha yake hii hapa chini.

    Attached Files:Report
    Like- 1 people like+ QuoteReply
  19. W
    WamalinyiJF-Expert Member
    #19
    Oct 8, 2016

    sawa

    Report
    Like+ QuoteReply
  20. K
    KajoleJF-Expert Member
    #20
    Oct 8, 2016

    mi nami nishare uzoefu wangu....pilipili kichaa ni kiboko chukua pilipili zitwange halafu changanya na maji iwe kali sana wape wanywe umekomesha magonjwa yote. ili wanywe vzur wafungie halafu wawekee chakula kikavu mf pumba mpaka saa nane hvi then wape maji hayo yenye pilipili. mwaka 2014 kijijin kwetu ulizuka ugonjwa kuku wote walikufa isipokuwa kwangu tu mpaka wakasema mi mchawi kumbe nliwapa dawa hyo baada ya kusoma jarida mtandaon

    Report
    Like- 2 people likes+ QuoteReply
59 more messages...
1234
    • ForumsKilimo, Ufugaji na Uvuvi

      • WHO ARE WE?
        JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic. You are always welcome!
        Read more...
      • WHERE ARE WE?
        We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually. For anything related to this site please Contact us.
        Contact Us Now...
      • DISCLAIMER
        JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..
        Read more...
      • FORUM RULES
        JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you. You MUST read them and comply accordingly
        Read more...
      • PRIVACY POLICY
        We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one. Read our Privacy Policy.
        Proceed here...
 
Yapata wiki sasa nahangaika na tatizo la Kuku kuvimba macho na kuwa vipofu kabisaa mpaka sasa ni Kuku 22 ndio wamepatwa na tatizo hilo, nimewahamisha banda kabisa ili wasichangamane na Kuku wengine wakaleta maafa zaidi nimeshajaribu kutumia antibiotics mbali mbali kama Piperazine citrate, sevin , Akheri powder kuwatibu lakini wapi yaani tatizo liko palepale kinachoniumiza zaidi hawa Kuku walishaanza kutaga na wengine ndio wanaelekea kuanza kutaga.
Kama kuna wataalamu humu naomba msaada wa cha kufanya maana mambo yanakua magumu sasa,hii ndio biashara pekee ambayo hakika haikuwahi kuniangusha sasa kama nitaanguka kwenye hii Nayo miti yote itakua inateleza kwangu hivyo chini nitaanguka
Kwa ufahamu wangu....kuju wangu wamewahi kupata hiyo shida.....nilisoma soma kwenye articles nyingi nikafahamishwa kuwa wamekosa vitamins baadhi kwenye mwili....solution ilikuwa kuwapa majani ya aina nyingi kwasababu yana vitamins...eg majani ya papai,mchicha,cabbage,nyanya,viazi,etc...majani yote ambayo kuku hula...baada ya wiki niliona tofauti....na sasa wamepona kabisa!
 
Shukrani kwa elimu hii
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom