donata fredy
Member
- Jul 22, 2016
- 45
- 84
MADAWA YA ASILI YA KUKU:
Madawa haya yanatokana na mimea na yanasaidia ktk jinga na kutibu pia. Dawa hizi tunazipata ktk sehemu za mimea yaani; majani, magome, mbegu, Maua na matunda. Umuhimu wake ni kama ifuatavyo: hupatikana kwa urahisi, rahisi kutumia, gharama nafuu, zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.
Pia unaweza ukawe tengeneza unga wake na kuchanganya kwenye pumba za kuku tazama hatua.
Hapa kwenye mlonge ni pazuri zaidi mmea huu unaitwa mmea Wa maajabu Duniani ni safi sana kwa binadamu naomba niwape kidogo. Chuma majani mateke yaanike ndani ili virutubisho visiondolewe na jua majani yakikauka yasage au twanga chekecha kupata unga. Pia watafiti wengine wanasema unaweza ukatumia shubiri mwitu kama ifuatavyo:
Shubiri Mwitu (Aloe vera):
Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.
Mchanganyiko huu unaweza kutibu: Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla kwa kinga. Homa ya matumbo (Typhoid). Mafua (Coryza). Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Mlonje): Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine.
Mlonge hutibu:
Pia katika Dawa hiyo ya jani la mpapai unaweza ukatwanga ukachanganya na pumba kile kisamvu chake weka kiasi ambacho Kuku watamaliza siku hiyo hiyo( chakula)
Mafua. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Homa ya matumbo Ini.
Pilipili Kichaaondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).
Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai
Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi. - Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.
Kutumia (kwa kinga) Kupambana na magonjwa ya kuku: Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi.
Njia nyingine ya kutumia Mpapai
Kuandaa na Kutumia Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.
Chukua jani moja la Shubiri mwitu lenye ukubwa wa kati. Likate katika vipande vidogo vidogo. Loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi cha lita mbili. Kuku utumia maji haya kunywa yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi unapobadilisha.
Kutumia Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku zote. Hii inafanya kazi ya kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali. Badilisha maji hayo kabla hayajaanza kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingine. Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla ya kuwawekea dawa nyingine.