Kutengeneza dawa ya kuku ya kutibu magonjwa yote kwa mitishamba

donata fredy

donata fredy

Member
Joined
Jul 22, 2016
Messages
45
Points
125
donata fredy

donata fredy

Member
Joined Jul 22, 2016
45 125
MADAWA YA ASILI YA KUKU:
Madawa haya yanatokana na mimea na yanasaidia ktk jinga na kutibu pia. Dawa hizi tunazipata ktk sehemu za mimea yaani; majani, magome, mbegu, Maua na matunda. Umuhimu wake ni kama ifuatavyo:
hupatikana kwa urahisi, rahisi kutumia, gharama nafuu, zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.

Pia unaweza ukawe tengeneza unga wake na kuchanganya kwenye pumba za Kuku tazama hatua

Hapa kwenye mlonge ni pazuri zaidi mmea huu unaitwa mmea Wa maajabu Duniani ni safi sana kwa binadamu naomba niwape kidogo. Chuma majani mateke yaanike ndani ili virutubisho visiondolewe na jua majani yakikauka yasage au twanga chekecha kupata unga
Pia watafiti wengine wanasema unaweza ukatumia shubiri mwitu kama ifuatavyo:

Shubiri Mwitu (Aloe vera):
Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12.

Mchanganyiko huu unaweza kutibu: Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla kwa kinga. Homa ya matumbo (Typhoid). Mafua (Coryza). Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).

Mlonje): Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine.

Mlonge hutibu:
Pia katika Dawa hiyo ya jani la mpapai unaweza ukatwanga ukachanganya na pumba kile kisamvu chake weka kiasi ambacho Kuku watamaliza siku hiyo hiyo( chakula)
Mafua. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Homa ya matumbo Ini.

Pilipili Kichaa:pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).

Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai
Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi. - Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.

Kutumia (kwa kinga) Kupambana na magonjwa ya kuku: Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi.

Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.

Chukua jani moja la Shubiri mwitu lenye ukubwa wa kati. Likate katika vipande vidogo vidogo. Loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi cha lita mbili. Kuku utumia maji haya kunywa yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi unapobadilisha.

Kutumia Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku zote. Hii inafanya kazi ya kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali. Badilisha maji hayo kabla hayajaanza kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingine. Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla ya kuwawekea dawa nyingine.
 
Lugoba Investment

Lugoba Investment

Senior Member
Joined
Dec 5, 2013
Messages
180
Points
250
Lugoba Investment

Lugoba Investment

Senior Member
Joined Dec 5, 2013
180 250
Nilichotaka nimepata
 
MPEME

MPEME

Senior Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
149
Points
225
MPEME

MPEME

Senior Member
Joined Mar 25, 2014
149 225
Asante kwa somo lako
Yaani namalizia kupost haya maneno naenda kuponda majani ya mpapai
 
KIKAZI

KIKAZI

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Messages
1,067
Points
2,000
KIKAZI

KIKAZI

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2014
1,067 2,000
Asante sana Mdau kwa nondo nzuri
 
W

Wamalinyi

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2016
Messages
241
Points
250
W

Wamalinyi

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2016
241 250
MADAWA YA ASILI YA KUKU:
Madawa haya yanatokana na mimea na yanasaidia ktk jinga na kutibu pia. Dawa hizi tunazipata ktk sehemu za mimea yaani; majani, magome, mbegu, Maua na matunda. Umuhimu wake ni kama ifuatavyo:
hupatikana kwa urahisi, rahisi kutumia, gharama nafuu, zinatibu vizuri na HAZINA MADHARA.
Pia unaweza ukawe tengeneza unga wake na kuchanganya kwenye pumba za Kuku tazama hatua
Hapa kwenye mlonge ni pazuri zaidi mmea huu unaitwa mmea Wa maajabu Duniani ni safi sana kwa binadamu naomba niwape kidogo
Chuma majani mateke yaanike ndani ili virutubisho visiondolewe na jua majani yakikauka yasage au twanga chekecha kupata unga
Pia watafiti wengine wanasema unaweza ukatumia shubiri mwitu kama ifuatavyo:
Shubiri Mwitu (Aloe vera):Chukua majani 3-5 makubwa, katakata na loweka ndani ya maji lita 10 kwa masaa 12 hadi 16. Wape kuku kwa siku 5 - 7. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine baada ya masaa 12. Mchanganyiko huu unaweza kutibu:Kideri/Mdondo (Mdonde/Chikwemba/Kitoga/Chinoya/Sotoka) - inyweshwe kabla kwa kinga.Homa ya matumbo (Typhoid).Mafua (Coryza).Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera).
Mlonje): Ina vitamini A na C. Chukua majani ujazo wa mikono miwili (gao mbili). Kisha yapondeponde na kuyaweka katika lita 10 za maji na iache kwa masaa 12-16, chuja na wape kuku. Isiyotumika mwaga na tengeneza nyingine. Mlonge hutibu:
Pia katika Dawa hiyo ya jani la mpapai unaweza ukatwanga ukachanganya na pumba kile kisamvu chake weka kiasi ambacho Kuku watamaliza siku hiyo hiyo( chakula)
Mafua. Kideri - inyweshwe kabla kwa kukinga Kipindupindu cha kuku (Fowl Cholera). Homa ya matumbo Ini.
Pilipili Kichaa:pondaponda kiasi kisha changanya na maji na wawekee kuku wawe wanakunywa kwa muda wao. Inasemekana inasaidia kutibu mdonde (lakini mapema kabla maradhi kuingia).
Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapai Kuandaa Pata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha lita mbili na nusu. Kutumia (kwa tiba) - Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewe maji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi. - Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike.
Kutumia (kwa kinga) Kupambana na magonjwa ya kuku: Jinsi ya kutibu na kuchanja - Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi. Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha lita 1. Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2. Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wachache, andaa chakula wanachoweza kumaliza kwa siku moja ili kisibakie na kuharibika kabla hawajakimaliza.
Chukua jani moja la Shubiri mwitu lenye ukubwa wa kati. Likate katika vipande vidogo vidogo. Loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi cha lita mbili. Kuku utumia maji haya kunywa yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi unapobadilisha. Kutumia Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku zote. Hii inafanya kazi ya kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali. Badilisha maji hayo kabla hayajaanza kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingine. Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla ya kuwawekea dawa nyingine.
Mkuu nisaidie kote nimeekewa ila,Isiyotumika mwanga maana yake nn
 
Nanoli

Nanoli

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2015
Messages
3,482
Points
2,000
Nanoli

Nanoli

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2015
3,482 2,000
Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?
 
ivunya

ivunya

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
1,532
Points
2,000
ivunya

ivunya

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
1,532 2,000
Asante kwa somo, ili kupunguza kero kwenda kwa majirani kuchuma majani ya papai Inabidi niupande hapa home kwa matibabu ya kuku.
 
Miss Natafuta

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Messages
22,290
Points
2,000
Miss Natafuta

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2015
22,290 2,000
Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?
kuhusu mafua wape piriton ni dawa nzuri sana kwa kuku
 
Evarm

Evarm

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Messages
1,559
Points
1,500
Evarm

Evarm

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2010
1,559 1,500
Asante sana kutupatia utaalam tiba mbadala...
Sasa kuku wangu wamepatwa na ugonjwa wa kizunguzungu, kushusha mabawa, kuvimba macho na mafua. Nimeshatumia dawa nyingi tu lakini bila bila,. nikawa nawaza hizi tiba za asili kwakua Kuna nilipitia pitia kusoma kitabu flani nikaambiwa haya matatizo kwa kuku hayana tiba, bali yana Kinga...
Sasa wewe kwa kutumia tiba asili unaweza nisaidia tatizo hili?
Hata dawa za tiba kwa binadamu, ukiwapa kuku wanapona bila ya Shida.
 
ARMs14

ARMs14

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2014
Messages
248
Points
250
ARMs14

ARMs14

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2014
248 250
Wakuu Leo naomba nami niongezee kitu hasa kwenye dawa za kuku wa kienyeji.ni cku nyingi sana nimefuatilia dawa ya alovera nimegundua ni dawa sahihi ila alovera iliyonipa mafanikio siyo ile chungu la ni ile isiyo chungu mara nyingi iinapatikana porini.nimeijaribu mara nyingi kwa kuku wagonjwa imenipa mafanikio naombeni nanyi muijaribu. Nami baada ya kugundua nimepanda kwa hom.Picha yake hii hapa chini.
 
Attachments:

Kajole

Kajole

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
1,562
Points
2,000
Kajole

Kajole

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
1,562 2,000
mi nami nishare uzoefu wangu....pilipili kichaa ni kiboko chukua pilipili zitwange halafu changanya na maji iwe kali sana wape wanywe umekomesha magonjwa yote. ili wanywe vzur wafungie halafu wawekee chakula kikavu mf pumba mpaka saa nane hvi then wape maji hayo yenye pilipili. mwaka 2014 kijijin kwetu ulizuka ugonjwa kuku wote walikufa isipokuwa kwangu tu mpaka wakasema mi mchawi kumbe nliwapa dawa hyo baada ya kusoma jarida mtandaon
 
Forum statistics

Threads 1,304,151
Members 501,282
Posts 31,504,691
Top