daniel_mollel
Member
- Sep 30, 2011
- 66
- 13
Mwalimu alipokabidhi nchi kwa Mwinyi, aliendelea kuwa mwenyekiti wa chama hadi mwanzoni mwa miaka ya 90. Jambo hili likitokea halitakuwa jipya...! Kuongoza chama kinachounda serikali kuna manufaa yake. Kwanza unakuwa na nguvu kubwa dhidi ya serikali, kwa maana ya kusimamia ilani ya uchaguzi. Jambo hili litakuwa na ugumu kupita ingawa likitafsiriwa kihalisia linaweza kupita. Nia ya makundi yanayovutana kuhusiana na swala hili ndiyo hasa tatizo kubwa. Upande mmoja kunawanaotaka kurithisha wenzao kwa maslahi yao..!, upande wa pili ni wale wanaoona kuwa wanaonewa. Kuliweka jambo hili sawa hadi lipite ni kazi kubwa kama ilivyo kazi kubwa kulipinga lisipite. Upande utakaoshinda ndio utakaoshinda pia katika mpambano wa kusimamisha mgombea urais wa CCM. Ukishinda upande ulioko nje ya utawala, makubwa zaidi yatafuata. Hatutashangaa kuona yaliyotokea ANC. Nafikiri ni swala la wakati tu, muda ukifika majibu yatatojitokeza yenyewe bila kutafutwa.