Kutenganisha uenyekiti na urais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutenganisha uenyekiti na urais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Oct 17, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sababu ambazo zitamfanya JK asikubali kofia za uenyekiti na uraisi zitenganishwe:

  1. Atakua raisi wa kwanza kuvuliwa kofia hilo. Kwake yeye ataichukulia kama kuonekana dhaifu.

  2. Itampunguzia nguvu na itapunguza hata nguvu zake kama raisi kwani kwa Tanzania chama ni serikali na serikali ni chama.

  3. Adui wa kisiasa anaweza akaukwaa uenyekiti kitu ambacho kitamuweka kwenye hali ngumu.

  4. Mgombea wa uraisi kupitia chama anatokea kwenye vikao na mkutano wa chama. Asipo kuwa mwenyekiti nguvu za kumteua mrithi au kuinfluence matokeo zitapungua.

  Kwa nini itakua busara JK kukubali mabadiliko haya:

  1. Chadema ilishaondoa dhana kuwa mwenyekiti wa uraisi lazima awe mgombea uraisi. Hii itaondoa dhana kwamba raisi lazima awe mwenyekiti.

  2. Itampunguzia mzigo. Anaongoza serikali wakati ambapo kuna matatizo mengi mno. Labda kushughulikia matatizo ya nchi na ya chama kwa wakati mmoja kunampunguzia uwezo wa kuwa tumikia kikamilifu Watanzania. Si rahisi kutumikia mabosi wawili (Wananchi kupitia uraisi na wanachama kupitia CCM).

  3. Itampunguzia lawama. Mwenyekiti akiwa mtu mwingine basi na huyo mwenyeliti atabeba baadhi ya lawama tofauti na sasa ambapo inambidi JK abebe lawama zote.

  4. Japo in the short term anaweza kuona kama ni aibu kwake kuwa raisi aliye ruhusu kofia hizo zitenganishwe in the long run atakuja kuheshimika kwa uamuzi huo.

  Je CCM ifuate njia gani kutenga kofia hizi pasipo migawanyiko zaidi?....

  1. Wanaweza wakakubaliana kuwa atakapo staafu JK basi makofia hayo yata tenganishwa. Hivyo itamaanisha JK atabeba makofia hayo mawili mpaka atakapo maliza yeye na hii inaweza ikawa rahisi zaidi kwake kumezwa kuliko yeye kuvuliwa moja kwa moja.

  2. CCM itumie busara na kupendekeza watu kwenye nafasi ya uenyekiti ambao wana heshimika na kuto kuwa na makundi yani a unifier rather than a divider.

  3. Katiba ya chama ielezee kabisa nini zita kuwa kazi za mwenyekiti wa chama na kuhakikisha haziingiliani na za raisi iwapo raisi atakuwa wa CCM. Yani isije ikawa swala la power struggle kati ya mwenyekiti na raisi.

  4. Ratiba wa uchaguzi wa chama ubadilishwe ili mwenyekiti achaguliwe mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa uraisi. Hii inamaanisha kama mgombea wa CCM atashinda uchaguzi tayari kutakua na mwenyekiti ambae bado ana miaka minne kumaliza muda wake.

  Haya ni maoni yangu tu ila uamuzi ni wa chama. Mimi nadhani si vibaya makofia haya kutenganishwa kwani baadhi ya nchi kama Marekani raisi hana cheo rasmi ndani ya chama. Ila hata CCM ikibaki na mfumo huu huu si vibaya. Cha muhimu ni kuhakikisha kuwa uamuzi ni kwa manufaa ya chama na wananchi badala ya watu wachache wenye uchu wa madaraka. Ninacho muomba tu raisi na mwenyekiti wa CCM ni atafakari na kujiuliza kwa nini swala hili limekua hoja sasa na si wakati mwingine wowote ule?
   
 2. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #2
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Nilisoma mahali kwamba ati Katibu wa Itikadi wa chama cha mampinduzi alisema hata Nyerere alikataa CCM kutenganisha kofia ya U-rais na uenyekiti...nilijisemea moyoni kwamba fikra za vijana wa aina hii ni janga.Anashindwa kuelewa emnzi hizo ilikuwa ni enzi za chama kimoja ambapo ilikuwa ngumu kutenganisha chama na Dola.

   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Maisha ni kwa waliyo hai. Kwa sasa matatizo ya Tanzania hayamuathiri kwa namna yoyote hayati baba wa taifa. Kwa maana hiyo basi ni wakati chama kitambue hakiwezi kubaki milele kuwa cha miaka ya sabini au themanini. Hii conservatism inaumiza chama. Kwa hiyo inashangaza vijana kama nape wanapo shindwa kudai mabadiliko.
   
 4. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,163
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti akiwa dhaifu haijalishi anashika nafasi gani katika chama, inabidi abadilishwe aje mtu mwingine. Ikiwa CCM wameona kuna mapungufu. Wabadili mwenyekiti. Lowassa atawafaa sana kwa CCM ya leo.
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ni kweli jambo hili muhimu sana kwa ustawi wa chama chenyewe na nchi pia kutenganisha kofia hizi. Tatizo la wana ccm wa dizaini ya Nape hawaruhusu fikra zao kupembua mambo badala yake wanabanana na kauli ambazo wanadhani zitamfurahisha mkulu basi!
   
 6. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Ila mimi nahisi Nape mara nyingi anatumiwa kama mouth piece. Ni maneno ya watu wengine kupitia mdomo wake...
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  welcome back mwanafalsafa1

  I missed you dude
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hiyo namba 2 ya mapendekezo ndiyo ngumu kwa ccm,huyo mtu naeheshimika ndani ya ccm ni yupi au asiyekuwa na makundi ni yupi?
  ushauri wa maana kwa ccm ni huu chama kitakufa kifo cha aibu na hamna namna ni kujidanganya tu kuwa kuna mwenye kuepusha hali hii.
  ccm inhitaji mtu jasiri wa kuinywesha sumu ili ife haraka na kuinusuru tanzania kwa sababu tunavyoendelea kusubiria hicho kifo cha kawaida ndivyo kama taifa tunavyoumia viongozi tulioamini ni wenye uchungu na nchi baada ya nyerere wamekuwa ni wanafiki wakubwa,tazama kauli zao,tazama walivyojilimbikizia mali,tazama watoto wao tazama wanavyongangania madaraka.
   
 9. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe, kwa kizazi hiki na hasa mabadiliko ya kisiasa na uwingi watu pamoja na majukumu ni muhimu sana CCM wakatenganisha hizi kofia

  Labda kama wanataka uongozi uwe passive kwa sababu hiyo ndiyo maana tupo hapa tulipo gizani maana hakuna mtu wa kuhoji kwa nguvu toka ndani ya chama mstakabali wa matatizo ya taifa hili.

  Wakitenganisha watakuwa wamefauru sana

  Kwa sasa mi naona tatizo ni katiba labda hairuhusu mabadiliko makubwa kiasi hiki ambayo bado ni pata potea
   
 10. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono 100%. Mara nyingi baadhi ya Watanzania tunafikiri kwa kutumia masaburi na tunafikiri kuwa Watanzania wote tunafikiri hivyo. Mara kadhaa vikundi fulani vyenye ushawishi katika vyama hasa CCM wanapomkataa au kumtaka mtu fulani hupenyeza hoja ambazo hazina msingi wa kikatiba wala za kanuni zinazowaongoza. Kwa mfano, WanaCCM wanachukua fomu ya kuomba nafasi mbalimbali za uongozi kama Uspika. Hapo utasikia kwamba safari hii ni zamu ya mwananamke. Wanafanya hivyo wakijua kuwa katiba na kanuni zinazowaongoza kupata wagombea katika nafasi mbalimbali hazifafanui hivyo wala mantiki haikubaliani na hilo.

  Kuhusu suala la nafasi ya urais na uenyekiti wa chama, WanaCCM walijua kuwa kwa upande mmoja kuwa suala la kuunganisha vyeo hivyo kwa mtu mmoja siyo la kikatiba wala la kikanuni na kwa upande wa pili hata kutenganisha nako hakujatajwa katika katiba wala kanuni. Kiongozi yoyote anachaguliwa pale anapokuwa na sifa za kuchaguliwa na hayo yanatajwa katika katiba ya kikundi husika. Sababu za kutenganisha kofia mbili lazima ziwe na msingi unatokana na katiba na isiwe kutokana na hali inayojitokeza leo.

  Udhaifu wa Jakaya Kikwete unaonenakana wazi iwe katika nafasi yake kama Rais wa Tanzania au kama Mwenyekiti wa CCM. Katika utaratibu wa kawaida wa kikatiba Rais Kikwete atatoka madarakani kwa njia ya kura za wananchi au bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye. Kama Mwenyekiti wa CCM atatoka kwa mujibu wa Katiba ya CCM. Kimsingi wanaCCM watakapoona kuwa mwenyekiti wao amepoteza sifa za kuwaongoza, wao watamua kukaa chini na kuangalia kwamba kwa mujibu wa katiba yao watamwondoaje katika nafasi yao. Hivyo, hoja ya kutenganisha kofia ya urais na uenyekiti siyo la kikatiba bali ni ya kihuni. Ni kwanini watu wanashindwa kutaja wazi wazi kuwa Jakaya Kikwete amepoteza sifa za kuwaongoza wanaCCM? Aondoke katika nafasi ya Uenyekiti wa CCM kwa sababu amekosa sifa na siyo kwa sababu ana kofia nyingine ya urais kana kwamba kofia mbili zinambana.
   
 11. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  I support you 100% RINGO EDMUND,jana JK alikua Katavi,amezidi kusisitiza WATANZANIA watoe support kwa wawekezaji kwani ndo watakao tukwamua na umaskini.Sasa najiuliza Buzwagi,Bulyanhulu,North Mara etc vimetusaidia ktk kuundokana na umaskini?,au vimeuzidisha?Jamaa sijui wanatupeleka wapi haki ya MUNGU.
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Thank you my friend.
   
 13. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Anaweza kuwa mwenyekiti as symbolic, alafu kazi ifanywe zaidi na katibu, nk. As you said, its a threat kwake kama hatakuwa mwenyekiti wa chama, maana anaweza kuzidiwa kete na maadui zake kwenye chama. Usifananishe na Marekani maana kule wanafuata system tofauti. As long as you can get support and have the money, mtu yeyote yule anaweza kugombea urais. Hapa lazima upitishwe na caucus ya chama.
   
 14. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu. Kila mtu anapenda madaraka na kila mtu anapenda nguvu lakini nguvu na maamuzi kufungwa ndani ya kundi dogo la watu si nzuri kwa taifa. Ndiyo maana wenzetu walioendelea kuna separation of power na checks and balances. Sasa sisi bado tuna ile mentality ya kwamba mtu mmoja akipewa nguvu nyingi ndiyo atakuwa na uwezo wa kuleta maendeleo.
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Gurtu

  Nakushukuru kwa maoni yako. Ndiyo swala la kofia mbili la mwenyekiti na raisi siyo la kikatiba. Ndiyo wanaCCM wana haki ya kumuondoa au kumbakisha mwenyekiti kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama. Ila kumbuka "change is constant". Huwezi kufanya vitu vile vile kila siku. Kuna ubaya gani wanachama kutafakari na kuamua kuwa ili kuwa na utendaji mzuri zaidi tutenganishe makofia haya? Haimaanishi yakitenganishwa itakuwa kwa JK tu.

  Politics revolve. Mnaangalia nini kina fanya kazi na nini hakifanyi kazi. Saa nyingine kitu kinafanya kazi ila mnabudi mbinu za kuongeza ufanisi zaidi. Sasa kung'an'gania tu status quo ina hasara yake kwa dunia inazunguuka, siku zina sogea na mambo yana badilika. Kwa maana watu wote wangekua wanafikiria wewe unavyo fikiria basi hadi leo tungekua na chama kimoja tu na kiongozi mmoja anae kaa mpaka atakapo kufa. Hata Nyerere mwenyewe aliona umuhimu wa kuachia ngazi japo kikatiba angeweza kukaa mpaka mwisho wa uhai wake.

  Kwa hiyo nakuchallenge mkuu try to thing outside the box. Mabadiliko siyo lazima yafanyike ila siyo vibaya kutafakari kama unacho fanya ni sahihi. Ndiyo maana kuna coming up with a plan, evaluating a plan then choosing to continue or discontinue the plan. Sasa ukizoea kupita njia moja tu ina maana utaipita hata ukijua mbeleni kuna shimo.

  Ni hayo tu mkuu.
   
 16. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  mwenyekiti wa chama akiwa raisi hachelewi kulalamika kwenye vikao vya chama kwani ni bei ya mafuta ya taa yanapanda kila kukicha....halafu anadai hamjui mmiliki wa richmond...

  serekali hukata, chama hupuliza..kuna haja ya kutenganisha nafasi hizo kwa ajili ya ustawi wa taifa
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  The move is very good for party and nation..

  Haitafanikiwa kwasababu wanaofanya hivyo wana "ill intentions"
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  And what are the ill intentions mkuu? Hebu nifafanulie....
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mimi kingine kinacho nichanganya ni unakuta chama chini ya mwenyekiti inaipa ushauri serikali ambayo inaongozwa na raisi huyo huyo na vikao hivyo vya chama vimejaa wajumbe kibao ambao wapo serikalini. Sasa hapa inakuaje? Inakuaje Mwenyekiti JK anampa ushauri Raisi JK?
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mojawapo ni urais 2015 missions

  Lakini ukiondoa hiyo nafikiri ni jambo zuri
   
Loading...