Kutenganisha kofia ya Urais wa nchi na Uenyekiti kutaisambaratisha CCM

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,793
12,238
Uimara na kuendelea kudumu kwa CCM kunatokana na nguvu za dola, nje ya hapo CCM ni chama dhaifu sana. Ndani ya CCM kuna wanachama waganga njaa wengi sana ambao maisha yao nje ya chama hayawezekani. Hivyo ili wanachama hawa waishi maisha ya heshima watafanya kila hila ili mwenyekiti wao awe Rais wa nchi.

Vurugu na mauaji ambayo hutokea wakati wa uchaguzi mkuu husimamiwa na hawa waganga njaa ndani ya CCM. Watu hawa kwa sasa wana wasiwasi mkubwa kuelekea kumsimika Rais Samia kuwa mwenyekiti mpya wa chama. Watafanya kila hila na hata kuua wapo tayari endapo vuguvugu hili la kutenganisha kofia litaendelea kupamba moto.

Kwa hiyo tahadhari ichukuliwe kwa ye yote atakayeweka wazi hoja hii vinginevyo ajiandae kuhama nchi endapo hoja yake itazimishwa si kwa kura bali kwa nguvu za dola. Bahati mbaya sana miongoni mwa waganga njaa ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wote ni wanachama wa CCM.
 
Hivi Rais wa sasa wa Tanzania asingekuwa Mwanamke (ambaye Kiafrika Wanawake wanapuuzwa) huu Mjadala wa kwamba Rais asiwe na Kofia nyingine ya Mwenyekiti Taifa ( hasa kwa CCM) ungeibuka au kuanza Kujadilika kila Kona hivi sasa?

Acheni Unafiki Samia (Rais) kama walivyokuwa Watangulizi wake awe pia Mwenyekiti Taifa wa CCM. Naamini itakuwa hivyo tu. Tunaacha Kujadili ya maana tuko katika Jambo la Kikatiba ndani ya CCM. Mbona wakati wa Hayati huu Upuuzi wenu hamkuusema ili awanyoosheni vizuri hadi mkome?
 
Sasa ndiyo nafahamu kwanini Mama Samia alikuwa akilalamika na hata kwenye hotuba ya bungeni kugusia hilo. Kuna fukuto la kutaka kumnyima kofia ya chama. Lakini “when all is said and done, Mama will prevail”
 
Msemo wao chama kushika hatamu, sasa bila ya Raisi kuwa mwenyekiti wa chama hizo hatamu hatokuwanazo . Suluhisho la yote haya nilazima katiba ya nchi ibadilishwe.
 
Kwani Kuna mtu amejitokeza kugombea uenyekiti wa CCM Hadi mnalijadili hapa?

Huyo ajitokeze tumuone. Kama Kuna aliyemdanganya amuulize mzee Makamba . Au amuulize Bashir kilichomfanya awe mpole Kama ndama.
 
Hivi Rais wa sasa wa Tanzania asingekuwa Mwanamke ( ambaye Kiafrika Wanawake wanapuuzwa ) huu Mjadala wa kwamba Rais asiwe na Kofia nyingine ya Mwenyekiti Taifa ( hasa kwa CCM ) ungeibuka au kuanza Kujadilika kila Kona hivi sasa?

Acheni Unafiki Samia ( Rais ) kama walivyokuwa Watangulizi wake awe pia Mwenyekiti Taifa wa CCM. Naamini itakuwa hivyo tu. Tunaacha Kujadili ya maana tuko katika Jambo la Kikatiba ndani ya CCM. Mbona wakati wa Hayati huu Upuuzi wenu hamkuusema ili awanyoosheni vizuri hadi mkome?
Mjadala huu si wa leo wala jana, ulianza tangu enzi za Kikwete lakini kwa sababu za uungwana wa Kikwete ilionekana hakuna sababu za kuendelea nao. Kwa sasa mjadala huu ni muhimu sana kutokana na udikteta wa Magufuli ambao umeathiri mshikamano wa CCM na Taifa kwa ujumla!
 
Msemo wao chama kushika hatamu, sasa bila ya Raisi kuwa mwenyekiti wa chama hizo hatamu hatokuwanazo . Suluhisho la yote haya nilazima katiba ya nchi ibadilishwe.
Ni kweli lakini hata ndani ya CCM kunatakiwa kuwe na Mwenyekiti imara na mgombea Urais imara!
 
CCM kuwa na mwenyekiti ambaye Rais aliyetokana ccm hakujaizuia ccm kufa, yaani badala yake kumeiua ccm kwa kasi sana, kiasi kwamba sasa hivi ccm hawezi kifanya siasa tena bila dola.

sasa kama kweli ccm wanataka kuwa chama cha siasa kweli ambacho kitaweza kufanya siasa bila dola ni lazima watenganishe kofia ya rais na uenyekiti wa chama, hii kutaiaaida sana ccm kama chama cha siasa,

zaidi ya hapo hakutakuwa na CCM kama chama siasa, ila ni vyombo vya dola vinavyotumia jina la ccm kutawala na kufanya maigizo ya siasa,.sasa hii ni mbaya zaidi maana siku ikitokea dola imetoka mikononi wa mwa hao wanatumia jina la ccm kutawala, ndio utakuwa mwisho wa ccm, kama ilivyokuwa KANU kule kenya, tatizo wao wanawaza kuwa watatawala milele,

ila hawajui wakati wanapanga MUNGU naye anapanga, mjifunze kwa Magufuli, kama imetokea kwa Magufuli inaweza tokea kwa ccm.
 
Uimara na kuendelea kudumu kwa CCM kunatokana na nguvu za dola, nje ya hapo CCM ni chama dhaifu sana. Ndani ya CCM kuna wanachama waganga njaa wengi sana ambao maisha yao nje ya chama hayawezekani. Hivyo ili wanachama hawa waishi maisha ya heshima watafanya kila hila ili mwenyekiti wao awe Rais wa nchi.

Vurugu na mauaji ambayo hutokea wakati wa uchaguzi mkuu husimamiwa na hawa waganga njaa ndani ya CCM. Watu hawa kwa sasa wana wasiwasi mkubwa kuelekea kumsimika Rais Samia kuwa mwenyekiti mpya wa chama. Watafanya kila hila na hata kuua wapo tayari endapo vuguvugu hili la kutenganisha kofia litaendelea kupamba moto.

Kwa hiyo tahadhari ichukuliwe kwa ye yote atakayeweka wazi hoja hii vinginevyo ajiandae kuhama nchi endapo hoja yake itazimishwa si kwa kura bali kwa nguvu za dola. Bahati mbaya sana miongoni mwa waganga njaa ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama ambao wote ni wanachama wa CCM.
Labda kusambaratika kunahitajika kwa manufaa ya umma.

Wanasema huwezi kukaanga mayai bila kuvunja yai.
 
Back
Top Bottom