Kutenganisha biashara na siasa: Kikwete ataweza?

Tz yetu mwisho wake cjui itakuwa nn,, tunafanyaje sasa jamani?????????? to stop all these?
 
Na ndiyo maana wapo tayari Tanzania iangamie kuliko CCM inayowalinda na kuwakingia kifua wasishitakiwe kutolewa madarakani. Ukiwaangalia wote hawa wanajifanya ni makada wazuri wa CCM, lakini ukweli ni kwamba wanatumia CCM kama chaka la kujifichia ili kuepuka mkono wa sheria.

Watake wasitake siku moja watawajibishwa wawe hai au wamekufa, kizazi hiki au kijacho cha watanzania kitawawajibisha wao au watoto au wajukuu wao. Ni vizuri wakubali kubeba mzigo huu wao wenyewe leo hii na kuacha vizazi vyao vikiwa na amani. Nawaambia kwa hakika kuwa huko mbeleni familia zao zitawakana kama ukoma kwa kubadili majina yao ya ukoo
 
1. EDWARD LOWASSA

  • Alipokea mlungula wa Richmond
  • Kanunua nyumba London kwa 1bn/-
  • Anamiliki nyumba na ardhi nyingi Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi
  • Amekwapua eneo la zamani la Nyumba ya Sanaa jijini Dar na sasa anajenga gorofa
  • Anamiliki Alpha group of companies ikiwemo Alphatel (Vodacom Super dealer), Alpha High Schools, Alpha House, etc.
  • Ana shares kwenye makampuni mengi kupitia watoto wake na ndugu zake wengine

Kama unaweza kudanganya moja pia unaweza kudanganya mengine hivyo unajiondolea heshima na dhamana ya kuaminika. Alpha High School wala si ya Lowasa na hana hata habari kama shule hiyo ipo.

Alpha High School inamilikwa na familia ya Prof Mayo wa chuo kikuu cha Dar es salaam na Alpha ni muunganiko wa majina ya mke na mume yaani prof na mkewe. Hata kama mtu ana dhambi ndio umuongezee hata zisizomuhusu? Hvi ndivi mapolisi wetu wa kibongo wanavyoshindwa kesi kila siku utakuta mtu amefanya tukio moja la ujambazi wanambambikia na lingine ambalo hakuhusika nalo, ushahidi ukitolewa unaacha doubts nyingi wakati mahakamani ili mtuhumiwa atiwe hatiani ni lazima upatikane ushahidi usio na chembe ya shaka.

Haya sasa mimi nafahamu hilo la Alpha high school sifahamu mengine je nitakuamini vipi kama yote unayoyasema ni kweli?
 
Mwanasiasa kujihusisha na biashara hususani kipindi ambacho anamadaraka ni tatizo kubwa saana hasa kwa maana ya conflict of interests. Wengi wetu kama tutaikumbuka hotuba ya kwanza ya Kikwete alilizungumza hii.

Na akaonya namna ambavyo chama kimekuwa kikiwatumiwa wafanyabiashara katika mambo yake na baadae kujikuta kikilazimika kulipa fadhila. Kwa Tanzania ni vigumu saana kudhibiti hali hii kwa madai kwamba watu hujifanya hawaonekani ilhali wengi huwaona wanayofanya.

Hivi karibuni wengi walilazimika kukaa pembeni ya siasa kwa sababu hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha. Leo hii Rostam kakaa pembeni kuna kina Diallo na wengineo.

Dhana hii katika vyama vya upinzani inatazamwa vipi? Ni wazi kuwa Mbowe ni mfanyabiashara maarufu na wa siku nyingi lakini je, dhana hii inachuliwaje? Ni lini Mbowe ataonekana independent? Kwamba siasa zake hazisukumi au kusukumwa na biashara? Wengi tunayafaham ya tuhuma za familia ya Mkapa na sasa hivi ya Kikwete kujihusisha na biashara. Au hili kwa upinzani halina maana?
 
[h=2]05 DECEMBER 2011[/h][h=3][/h]

Na Martha Fataely, Moshi

BAADHI ya viongozi wanakwamisha maendeleo kutokana na kuegemea katika siasa, biashara na kusababisha mgongamo wa masilahi hivyo kuwafanya washindwe kutoa
maamuzi.

Bw. Madaraka Nyerere, aliyasema hayo jana mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro wakati akiongoza timu ya watu 90 kutoka ndani na nje ya nchi kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.

Alisema viongozi wengi wanakiuka maadili ya uongozi hivyo kusababisha matatizo katika utendaji kazi wa kila siku jambo ambalo linakwamisha juhudi za wananchi kujiletea maendeleo.

“Leo nimekuja kwa ajili ya kupanda mlima, sasa naona mnataka
nigeuze ajenda, yapo mambo yanatakiwa kubadilishwa, hii tabia ya viongozi kuchanganya biashara na uongozi inaleta mgongano wa masilahi, matatizo tuliyonayo leo yanachangiwa na hilo,” alisema.

Mapema akizindua safari hiyo ambayo imeandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Kampuni ya Kusafirisha Watalii ya Zara Tours , Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bw. Musa Samizi, alisema msafara huo pia unajumuisha waandishi sita wa habari.

Aliipongeza TTB, TANAPA na Kampuni ya Zara kwa kuandaa safari hiyo ili kuadhimisha miaka 50 ya uhuru pamoja na mambo mengine, safari hiyo inahamasisha utalii wa ndani ambao unaonekana kukua.

Bw. Samizi aliwataka washiriki wote kuhakikisha wanajitahidi
kufika kileleni katika siku zilizopangwa na kushuka Desemba 10 mwaka huu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Zara Tours, Bi.
Zainab Ansell, alisema kila mwaka kampuni yake itaandaa safari hiyo kwa lengo la kuutangaza ulima huo.

Alisema sekta ya utalii nchini imepata mafanikio mbalimbali ndani ya miaka 50 ya Uhuru huku amani na utulivu, ikiendelea kuwavutia wageni kutoka mataifa yote duniani.

Awali Mhariri Mtendaji wa gazeti hili, Bw. Ima Mbuguni, ambaye ni miongoni mwa waandishi sita wanaopanda mlima huo, alisema anajivunia kuzaliwa ndani ya miaka 50 ya Uhuru waakati Tanzania ikiendelea kuwa nchi ya amani na utulivu.

Aliwataka Watanzania wa kada zote pamoja na vyombo vya
habari, kutangaza mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka hiyo na kueleza changamoto zilizopatikana kwa kipindi hicho ili zifanyiwe kazi na kuleta maendeleo endelevu.

Akizungumzia safari hiyo, Ofisa Uhusiano wa TTB, Bw. Godfrey
Tengeneza, alisema bodi hiyo ilikusudia kuandaa ziara hiyo ili kutangaza utalii wa ndani ndani ya miaka 50 ya uhuru.



 
Yeah, Madaraka Nyerere angalau unawaambia hao viongozi wenye Macho ya Makengeza, Moja ndani ya siasa lingine ndani ya biashara
 
Madaraka pamoja na kuwaambia hayo watawala wetu kupitia Azimio la Zanzibar miiko yote ya uongozi na maadili mbalimbali waliyaweka kapuni. Watawala wetu sasa hivi wako kwenye mashindano ya kufanya dili mbalimbali utafikiri ni investment bankers.
 
Kweli Katiba inaweza kutenganisha biashara na siasa? au itaziunganisha ili kufanikisha nafsi za wagombea Uongozi?
 
good point, Madaraka ingawa sidhani kama kuna mtu anasikiliza...; by the way, nini prospects ya watoto wa Mwalimu katika siasa za sasa na za baadaye za Tanzania? it looks like wakati watoto wengine wa viongozi wako busy kuji-position strategically tayari kuchukua nafasi muhimu za ulaji, hawa jamaa wanazidi kuwa relegated to political oblivion
 
Jamani ule msaada wa sheria, ambao Rais alinielimisha kwa kinywa chake, mimi na wewe kwa kutumia vyombo vya habari kuwa, Serikali ya Awamu ya nne imedhamiria kutenganisha Biashara na Siasa kwa wanagombea, kuepuka maslahi binafsi na akaahidi angeupeleka bungeni.

Nimevuta subira miez imepita na kama si miaka awamu yake inayoyoma. Kuna nini nyuma ya Pazia, Nani alimkwamisha mkuu wa Nchi au umezimia si ungekuta umezinduka, umezimwa na nani maana Rais ndiye yuko juu. Ulikuwa na madhara gani kwa ustawi wa siasa safi au Taifa. Kulikoni?, Kunani? Naombeni majibu ya maswali hayo au mojawapo.

Ahsanteni kwa michango yenu msinibanie toka magogoni Raisi na watendaji tuliowapangishia hapo msimamie Ukweli, wazalendo mnaofanya kazi magogoni, wizarani, wadau na wote kwa hoja zenu kujibu kulikoni ???karibuni, nawasubiri kwani Tanzania ni zaidi ya Ujuavyo;>
 
nijuavyo, ni asilimia ndogo sana ya yale yanayosemwa na JK huwa yanatekelezwa. sioni cha ajabu. He always have very good ideas but very poor actions for most of.
 
Wanasema hautekelez kwa kuwa wanasiasa wengi hasa wa ngazi za juu ni wafanyabiashara na hata wajao wakiwemo watoto wao wanaowapigiachapuo ni wafanyabishara tena zenye kutiliwa mashaka
 
Wadau,

Nakumbuka hapo kipindi cha Nyuma Rais wa JMT alianzisha Mada ya Wafanyabiashara kutojihusisha na Siasa maana biashara zitaathiri Biashara zao, au Biashara zitaathiri Siasa zao mwishowe ikaleta mvurugano katika jamii.

Hakuna Shaka kua Bw. EL anahuitaji Urais kwa udi na uvumba, Sasa nlianzisha Maada nikiuliza kuhusu sources of Income za Mheshmiwa wetu huyu na wengi wamejibu kua ni Mfanyabiashara mkubwa, ambayo pia haina ubishi.

Sasa kwakua Rais alishasema (sio kuamuru) kua wafanyabiashara wasijihusishe na Siasa, ule ushauri haumuhusu huyu Bwana?? Akipata Urais hatautumia kuendeleza biashara zake? Akiupata Urais (kama ikitokea), atajiepusha vipi kutoyapa upendeleo makampuni yake katika tenda mbalimbali ambayo zinayahusu??

Je hii dhana ya kutokuchanganya Siasa na Biashara ina mantiki yoyote kwa sasa? Tukimpata Rais ambae anajulikana fika kua ni Mfanyabiashara kuna madhara gani? Je hakutakua na Faida zake vilevile? Teseme labda akiingia Rais anaejiweza kifedha, haitatuaminisha kua hatahongwa maana hatakua na njaa ndogondogo za hapa na pale??

Tujadili.
 
Ruksa,maana mwanasiasa sharti awe na elimu/idea ya ujasiri-mali au kwa lugha nyepesi/kitaalamu material-confidency.hapo upo ndugu!,kama si hivyo basi usingesikia kelele za wale walioliwa pesa zao alafu wakatoswa uongozi.chezea siasa wewe ni deal kama deal nyingine na ni mwanvuli mzuri sana wa kujikinga na mvua isipokuwa radi tu.
 
Back
Top Bottom