Kutenganisha biashara na siasa: Kikwete ataweza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutenganisha biashara na siasa: Kikwete ataweza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GY, Dec 11, 2009.

 1. GY

  GY JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Toka aingie madarakani amekuwa akilisema sana hili la mtu kuamua aidha biashara au siasa (na uongozi wa umma).

  Na sasa anasema wanaandaa muswada wa hilo

  Swali langu ni kuwa, ikiwa wafanyabiashara ndio waliomfikisha ikulu, na bado wanakumbatiwa sana na chama tawala (ambacho yeye ni mwenyekiti wake), wakiwa na sauti kuliko mwingine yeyote yule

  Je anamaanisha asemayo?
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  USIMWAMINI kikwete kwa jambo lolote asemalo, daima amekua akifanya mambo kwa shinikizo na kupenda kusifiwa.
  Hii ndo serikali ambayo imekua ikifanya kazi baada ya maandamano na migomo.

  Kweli alilisema hili akitafuta sifa na ujiko toka kwa UMMA, niambieni miaka mingapi imepita tangu atoe ahadi hiyo mara ya kwanza?

  PILI YAPO mafungamano pacha kati ya CCM na wafanyabiashara hasa mafisadi papa, na tayari kina makamba wameaanza kusigana na makala juu ya kuendelea kupokea mishiko toka huko, kina Manji Yusuph wamekua wakiaandaa pesa kitambo sasa kwa ajili ya kupandikiza mapandikizi kwenye siasa na kuhakikisha wanaowaunga mkono wanabaki.

  Ukita kujua hilo ni gumu angalia Makala anahubiri kuacha kushughulika na wafanyabiashara kwenye Siasa za ccm wakati huohuo kapokea mamilioni toka kwa kina RA, KWA ajili ya kuingia bungeni.
   
 3. GY

  GY JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  nguvumali

  Juzi wamemuonyesha akiongea TBC na kusema kuwa punde watapeleka muswada bungeni ili sheria ipitishwe. Kama kweli linamkera, kwanini asingeanza kwa kutowaweka wafanyabiashara kwenye serikali yake. Mfano kama si sakata la richmond, karamagi angekuwa ndani ya serikali bado

  Is he serious about it?

  mwakani kwanini tusimuulize hili kabla ya kumpa kura
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ikiwepo nia thabiti bila unafiki ama ubabaishaji katika kusimamia suala zima la kutenganisha biashara na siasa/uongozi jambo hilo linawezekana. Nia yenyewe isiwe ni nia ya Rais tu bali ya vyombo vyote vya serikali na Watanzania wazalendo wadhamirie kuhakikisha siasa na biashara haviendani.

  Kitakachohitajika kwanza ni kuwaelimisha ipasavyo wananchi ili waelewe umuhimu wa kutenganisha biashara na siasa na sababu za uamuzi huo kuchukuliwa. Wananchi watakapoelewa ndipo watakapoweza kuwachuja ipasavyo wale ambao watajitokeza kutaka kugombea nafasi za uongozi.

  Pili, wote wanaotaka kugombea uongozi inawabidi wawatendee haki wananchi kwa kuwa wakweli kwenye dhamira zao. Waamue kwa dhati kabisa kujitolea kuwatumikia wananchi na kama wataona biashara ni muhimu kwao basi waachie wenye moyo wa kuwatumikia wananchi wagombee nafasi za uongozi.

  Lakini kutegemea dhamira peke yake haitoshi. Lazima iwepo miiko ya uongozi itakayoingizwa ndani ya Katiba ili iwe ya kudumu na iwapo itakiukwa hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mkiukaji. Hiyo itasaidia kupunguza wale ambao wangeliweza kutaka kufanya ulaghai wakielewa hakuna chochote kitakachotokea iwapo udanganyifu wao utadhihirika.
   
 5. GY

  GY JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Je ni kila sheria inapotungwa wananchi huelemishwa?
   
 6. A

  Amanikwenu Senior Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Dec 1, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kinachotakiwa ni kuwa, ukishakuwa mfanyabiashara sahau habari ya kuwa mwanasiasa.
   
 7. GY

  GY JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Hapana sidhani kama ni ivo, lengo ni kuwa ukiwa mfanyabiashara na unataka kuwa mwanasiasa, achana na biashara zako kwanza, fanya kazi ya umma, halafu pale unapoamua kuachana na siasa, rudi kwenye biashara zako.

  Ila ukishakua mwanasiasa, sahau habari ya kuwa mfanyabiashara
   
 8. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,429
  Likes Received: 3,792
  Trophy Points: 280
  Hataweza.........Kile kiwanda chake cha mafuta ya kula kilichojengwa pale karibu na bandari in the name of Mohamed interprises atakifanyia nini...???
   
 9. GY

  GY JF-Expert Member

  #9
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Taratibu mzee yeye si alisema ni mkulima tu si mfanyabiashara, huenda akawa anasupply alizeti tu!
   
 10. F

  Fareed JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  BIASHARA & SIASA: Viongozi waliotajirika kupitia siasa hawa hapa


  1. EDWARD LOWASSA

  • Alipokea mlungula wa Richmond
  • Kanunua nyumba London kwa 1bn/-
  • Anamiliki nyumba na ardhi nyingi Dar es Salaam, Arusha na nje ya nchi
  • Amekwapua eneo la zamani la Nyumba ya Sanaa jijini Dar na sasa anajenga gorofa
  • Anamiliki Alpha group of companies ikiwemo Alphatel (Vodacom Super dealer), Alpha High Schools, Alpha House, etc.
  • Ana shares kwenye makampuni mengi kupitia watoto wake na ndugu zake wengine

  2. ROSTAM AZIZ


  • Katumia nafasi yake ya Mbunge na alipokuwa mweka hazina wa CCM kuwa multi bilionaire.
  • Alitumia nafasi yake ya mweka hazina wa CCM kuchukua hisa kwenye Vodacom

  • Alitumia nafasi yake kama swahiba wa Lowassa kupata pesa kupitia Richmond
  • Alitumia nafasi yake ya mweka hazina wa CCM kuchoka 40bn/- za EPA kutoka BoT kupitia kampuni yake ya Kagoda
  • Alitumia nafasi yake ya ubunge kupata msamaha wa kodi na kuagiza mchele kutoka nje na kuuza kwa faida kubwa
  • Alitumia nafasi yake ya ubunge kupata pesa kupitia Commodity Import Support scheme
  • Alitumia nafasi yake ya Ubunge kupata tenda kwa kampuni yake ya Caspian construction kwenye miradi mikubwa ya Tanesco, madini na ujenzi

  3. ANDREW CHENGE


  • Alipokea mlungula wa rada bila mashaka yoyote

  • Alipokea milungula kwenye mikataba mingi mibovu ya serikali

  4. BENJAMIN MKAPA


  • Yeye na mke wake walianzisha kampuni ANBEM na kufanya biashara wakiwa Ikulu
  • Aliutwaa mgodi wa Kiwira
  • Yeye na mke wake wamepora magorofa mengi ya mashirika ya umma kama ATC, NBC na mengine
  • Anamiliki nyumba nchi za nje

  5. NIMROD MKONO


  • Huyu amepokea malipo ya billions of shillings kwa malipo ya wizi ya kisheria. Aliyekuwa AG, Andrew Chenge, aligawa kesi zote kubwa za serikali kwa Mkono in return for illegal kickbacks. Kesi hizo ni za Benki Kuu, Tanesco na idara nyingine za serikali. Pamoja na kampuni yake ya kisheria, ana miliki Bank M na mafisadi wengine.

  6. MOHAMED DEWJI  • Huyu tayari anatoka kwenye familia ya kitajiri lakini ameweza kupata tenda kubwa za serikali na misamaha ya kodi kwa kutumia nafasi yake ya Ubunge. Hivyo anaendelea kutajirika kwa kutumia nafasi yake ya ubunge, huku akiwalaghai wanananchi wa Singida kwa kuwapa pesa ndogo ndogo (bread crumbs).
  7. DR. HUSSEIN MWINYI

  • Among other things, anamiliki apartment buildings kadhaa Dar es Salaam zenye thamani ya bilions of shillings. He is becoming a real estate magnate. Huyu anatajirika kimya kimya bila watu kujua (silent mover).

  • Amewahi kupokea more than 400m/- kutoka kwa Malegesi aliyechota pesa za EPA na mpaka sasa kesi yake haiko mahakamani.

  8. OTHERS

  Wengine waliotajirika kupitia nafasi zao za serikalini ni Basil Mramba, Gay Mgonja, Chrisant Mzindakaya, Nazir Karamagi, (to be continued...)
   
 11. F

  FUSO JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,878
  Likes Received: 2,343
  Trophy Points: 280
  harafu mnasema eti nchi hii maskini wakati imezaa matajiri wenye mabillion ya dola - maskini Tanzania pole kwa kukamuliwa kila kona kila kukicha.

  Si wote waimbao - Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote..... wanamaanisha hivyo, bali wengi wao ni wanafiki wakubwa, uwe mwangalifu.
   
 12. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Tanzania kwa mwendo huu tumekwisha!
   
 13. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Waow!
  Mie Mkweche sina Shida!Ni wa humu humu!Kama Ulanzi napata, kama Hela ya Lita mbili za komoni sikosi!
  Kipya kwangu hapa swala la kununua Hisa za VODA ni lazima uwe na Ka-Cheo kwanza!Hili jipya!
  Orodha ndefu kwali ila maelezo yake mengine ndio yamekosa mantiki!
   
 14. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Tanzania kuna nyumba zinauzwa $3m just one family, hapo ndo ujue Tz kuna matajiri.
   
 15. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ivi shida ya kuwashtaki hawa ni nini kama mna evidence?
   
 16. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Hapa ndipo penye UTAMU....
  HAPATATAJWA WOTE WALIOTAJIRIKIA SIASANI WALA WALE WALIOINGIA KWENYE SIASA ILI KUFICHA MAOVU YAO...!!!
  MBONA WAKO WENGI TU NA WANAJULIKANA KUWA KWANINI WAMO KWENYE SIASA...
  HII NCHI INAHITAJI MAGEUZI YA KWELI NA SI YA VYAMA...
  KUTAJA PEKEE BILA HATUA NI KAMA MBWA ALIYE BANDANIKUBWEKEA MWIZI WA KUKU ANAEONDOKA NA KUKU!!!
  Ila si mbaya TUMERITHI kwa mababu... WATU WAOVU WALIIMBWA KWENYE NGOMA WAKAHAMA KIJIJINI!!!
   
 17. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Hawa wote ni wakukamata na kupeleka kunyea debe hasa Lowassa, Rostam, Chenge, Kkwete na Mijambazi mingine zipo siku zao wako wapi wakina Hosni Mubarak, Saddam Hussein na Gadaff huyo karibuni watamtundika Mahakamani.

  Kikwete na majambazi wenzako soon mtakuwa Next
   
 18. D

  Derimto JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna hawa watu lakini hawajulikani sana wala kujionyesha kama wenzao

  1. Ami Mpungwe aliyekuwa balozi wa tanzania nchini africa ya kusini.

  2. Joseph Mungai na wengine wengi sana hebu endeleeni kuleta list hapa jamvini.
   
 19. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama ni kweli TAKUKURU iongezwe kwenye list!
   
 20. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Huyo hapo kwenye RED anamajumba kibao Huko South Africa, aliifanya Ofisi ya Ubalozi pale Pretoria kama ndio ofisi ya kufanyia biashara zake, Mwizi sana huyo Mzee na ndio aliotuletea balaa hapa Arusha la Tanzanite one.
   
Loading...