Kutembelea wafugaji na wakulima hili ni la muhimu sana

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,817
9,060
TUFANYE HAYA ZIARA ZA KUTEMBELEA MFUGAJI/MKULIMA

Siku za hivi karibuni watu wamekuwa na mwamko wa kutembelea kujifunza kwa watu wengine.Kujifunza kilimo na pia ufugaji.
Watu hutembelea kujifunza ufugaji wa
- Kuku
-bata
-Sungura
-Kanga
-Samaki
Pia kilimo hasa cha mboga mboga na matunda na pia vitu kama uyoga na kadhalika.

ULISHA WAHI KUJIULIZA HAYA?
Kwa nini wafugaji wengi na wakulima wengi huwa wana kwepa wageni?
Au basi utapigwa tarehe za kutosha?

SABABU KUBWA NI HII,SEMA HUTAAMBIWA

Wengi wa wafugaji na wakulima hiwa hawaoni faida ya wao kukaribisha wageni.
Huwa anaona ni kupoteza muda wake bure.
Huwa anaona mgeni ataangalia mwisho wa siku ataseama asante sasa asante inasaidia nini?
Huwa wanaona ni kuchoreka au kusanifiwa au kuja kupeleleza.

TUFANYE HAYA
Unapo panga kumtembelea mfugaji au mkulima basi ukienda usiondoke mikono mitupu.

UMEENDA KWA MFUGAJI KUKU
Nunu hata kuku, nunu mayai,nunua vifaranga
Ikishindikana muachie hata pesa ya Vocha basi kama asante. Zile asante za mdomo ni za kijamaa zisha pitwa na wakati.

UMEENDA KWA MFUGA BATA
Nunu bata hata kama wewe hutamtum8a just nunua tu, au chukua mayai kadhaa.
Au muachie pesa ya vocha.

KWA MUFUGA SUNGURA
Baada ya kumaliza kujifunza nunua Sungura hata kama hutaenda kumla wewe wewe nunua tu, ataona una mjali sana tena mno.

KWA MFUGA NG'OMBE WA MAZIWA
Akisha maliza kukupa lecture nunua maziwa ondoka nayo. unaweza weka oda mapema kwamba uachiwe lita kdhaa za maziwa.
Imeshindikana muachie pesa ya muda wa maongezi.

KWA MKULIMA
Nunua mboga basi au matunda kutoka kwake.usiondoke tu mikono mitupu na kusema asante.

Kwa kifupi nunua chochote kinacho nunulika kutoka kwa mfugaji au mkulima ulie enda kumtembelea.
Hata kama ni kibaya wewe nunu hata kama utafika njiani utupe wewe nunua make ni sehemu ya shujurani kwake.

Tuachane na biashara za kupewa elimu mwisho wa siku unasema asante.

MBAYA ZAIDI

Umeenda kwake kujifunza halafu anasikia ulienda kununua Mayai kwa mtu mwingine, au kuku ulienda kuchukua kwa mtu mwingine na yeye katumia muda mwingi sana kukupa elimu.

Unaenda kwa minajili ya kujifunza ufugaji wa sungura/Samaki/Uyoga/Bata/Kuku na unapewa elimu free ila baadae kimya kimya tena kwa siri unaenda kununua kwingine.

Yeye unaishia kumuambia Oo najipanga, naandaa banda, nakusanya nguvu. kumbe zuga.

Najua kuna watakao chukia ila ukweli ndo huo.

Sikukuu njema

By
Chasha Farming
 
well said kiongozi kwa maana nyingine ni utalii wa kujifunza!!! hii ni elimu inayoeleweka kwa urahisi kulikko ya darasani
 
Back
Top Bottom