Kutembelea na kusafisha makaburi ni kufanya ibada na marehemu?

kadovela

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
471
678
Habari zenu wana JF,

Ningependa kujua zaidi na kuwekwa sawa kwenye hii dhana ya kutembelea na kwenda kusafisha makaburi ya ndugu, jamaa na marafiki.

Je, kwa kitendo cha kwenda tu kutembelea na kusafisha maeneo hayo unakuwa umefanya ibada za marehemu?

Nb:
Sizungumzi wale ambao wanaenda kulia kwenye makaburi na kusali wakiamini kwamba marehemu zao wanaweza either kuwasaidia kufikisha maombi kwa Mungu au kwa kuwaombea MUNGU awarehemu japo hesabu zao zilishafungwa siku walipoaga dunia.

cc mshana jr.
 
majoto. lazima nikiri kuwa sina uelewa wowote kuhusu mila zetu katika hili
 
Siamini kama ni ibada ni kumuenzi tu mpendwa wala haina shida sababu wale wanaochomwa je?
 
Nakushauri ufuate mila na desturi za kabila au ukoo wenu zinataka nini kwenye masuala hayo.

Mfano kuna wengine wanautamaduni wa kwenda kusafisha makaburi kwa kuyalimia, kama ni makaburi ya wazazi, bibi au babu, wewe usipokwenda na ulikua unanafasi ya kujumuika na wenzako, unaweza ukapata matatizo.
 
ok nimekuelewa
 
Nawe umeamini unaweza kupata matatizo kwa kutokulimia kaburi? Basi wewe utakuwa umefanya zaidi ya wale wanaowaombea marehemu.
yaani nimemuelewa alichosema ila kufanya au kutofanya ni jambo ambalo lipo ndani ya uwezo wangu maana lipo ki mila zaidi
 
  • Thanks
Reactions: THT
Mtoa mada umeuliza '...je ni ibada?' Unajua maana ya neno 'ibada' Ibada ni kitendo cha kiroho. Ni kumwomba Mungu au roho ambazo sio Mung (kwa mfano mizimu au mashetani). Kwa hiyo, ni wazi kwamba kitendo cha kusafisha kaburi peke yake bila kukiunganisha na maombi ya aina yoyote hakiwezi kuwa ni ibada. Ibada ya mizimu ni pale unapoenda kuomba kwenye kaburi (liwe limesafishwa au la). Unapoenda kuomba kwenye makaburi unaenda kumwomba mtu au watu waliokufa zamani. Unakuwa umemwomba binadamu badala ya Mungu.Ni dhambi mbaya sana ya kumdharau Mungu maana ukifanya hivyo unamaanisha kwamba yule mtu unayemwomba ana nguvu sawa na Mungu.
 
nimekuelewa na utata naanza kuutoa maana kuna nadhari zinasema hata kutembelea tu ni kama kukengeuka kiimani
 
Ibada siyo lazima kuomba ila hata kufurahisha au kuamini kuwa ukitimiza jambo flani kunaepusha mabaa flani flani.
 
Kama imani yako haitambui marehemu utakuwa umekengeuka. Ila kama inatambua basi kulimia makaburi, kujengea n.k ni jambo jema kulifanya.
 
Mimi nina swali je wanachofanya RC kila mwaka wana misa ya kuwaombea wafu kanisani. Halafu wanaenda kusafisha kaburi au kulijengea na wanaenda na mchungaji anaombea marehemu. Je ni sahihi au sio sahihi?
 
Habari zenu wana JF,

Ningependa kujua zaidi na kuwekwa sawa kwenye hii dhana ya kutembelea na kwenda kusafisha makaburi ya ndugu, jamaa na marafiki.

Je, kwa kitendo cha kwenda tu kutembelea na kusafisha maeneo hayo unakuwa umefanya ibada za marehemu?

Nb:
Sizungumzi wale ambao wanaenda kulia kwenye makaburi na kusali wakiamini kwamba marehemu zao wanaweza either kuwasaidia kufikisha maombi kwa Mungu au kwa kuwaombea MUNGU awarehemu japo hesabu zao zilishafungwa siku walipoaga dunia.

cc mshana jr.
Ni jambo jema tena la heri kabisa lisilo na tatizo kabisa! Kumbuka roho za marehemu huwa na mawasiliano ya kiroho pale mwili ulipolazwa
 
Mimi nina swali je wanachofanya RC kila mwaka wana misa ya kuwaombea wafu kanisani. Halafu wanaenda kusafisha kaburi au kulijengea na wanaenda na mchungaji anaombea marehemu. Je ni sahihi au sio sahihi?
Ni sahihi kulingana na mafundisho yao. Kulingana na mafundisho, kanisa limegawanyika mara tatu ambapo kuna kanisa la washindi (hawa ni wale watakatifu walioko mbinguni), pili ni kanisa lililoko toharani (marehemu wanaostahili kuingia mbinguni ila walikufa wakiwa na dhambi ndogo au hawakutimiza malipizi baada ya kukiri dhambi zao) na mwisho kanisa la duniani (hili ni kanisa linalosafiri kuelekea mbinguni). Kulingana na mafundisho hayo sehemu hizo tatu zote zina ushirika uitwao ushirika wa watakatifu.
Unaweza kujiuliza mbona makanisa mengine hayana mafundisho hayo? Jibu la swali hili liko kwenye vitabu vya biblia vya agano la kale. Biblia ya wakatoliki ina vitabu 7 ambavyo madhehebu mengine hawana kwa sababu mwanzilishi wao Martin Luther alivikataa.
 
  • Thanks
Reactions: THT
Back
Top Bottom