Kutembelea Makaburi ya Kigali ukiwa na miezi minne madarakani kukusaidie kutambua dhamana uliyopewa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
543
1,000
Kabla ya mauaji Rwanda viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola waliminya watu Kama tunavyoshuhudia hapa nchini Sasa. Leo Mhe. Rais ametembelea Makaburi yaliyosababishwa na watu wachache walioona wao ndio waliozaliwa kutawala.

Mwenyenzi Mungu anakusudi kumpa safari siku chache baada ya dola kumweka Mbowe Ndani. Amepata safari hii kwa lengo la kujifunza madhara ya siasa chafu, kujifunza madhara yakutengeneza kundi la watawala na watawaliwa.

Nimeona uteuzi wake nadhani alilenga kuendeleza koo zile zile za akina zelothe, Robert, Katarahia, Nnauye na wa kariba hii. Hii ni nchi, watu wanaona na wanavumiliana. Matembezi yako Kwenye Makaburi yakufanye unaporejea nchini uliutubie Taifa, utoe dira upya ya wapi unataka tuelekee maana tumepoteana.

Ukiwa Rais utengenezewi jina zuri unatengeneza jina zuri, Waziri anaweza akatengenezewa jina na Rais lakini Rais Hana wakumtengenezea jina. Njoo nchini ukiwa unatafakari ufupi wa maisha yetu hapa Duniani, turejeshea amani.
 

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
5,198
2,000
Kweli kabisa, Mana uongozi unakuwa ni wa watu wa aina fulani wenye connection, wakati nchi yetu wote , na Mimi Nataka teuzi, hata kama kwetu hatuja toa viongozi lakini Nataka kuwa wa kwanza kuwa kiongozi kutoka ukoo wetu.
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,762
2,000
Mkuu, 'Beatrice Kamugisha', moja ya mada zako makini sana.

Kama angekuwa na watu makini hapo ofisini kwake wanaomfikishia taarifa toka pande hizi, hakika wasingekosa kumfikishia hii ya kwako.

Ni fupi, haichoshi kusoma, lakini imebeba ujumbe muhimu sana, tena ujumbe unaohusu hali halisi inayomkabili katika uongozi wake hapo alipo.

Lakini ajue ana hiari ya kuchagua alichofuata huko. Anaweza kujifinza mbinu mbaya zinazotumiwa na mwenyeji wake kwa lengo la kuzima hali tete iliyopo huko, yeye akadhani ndiyo inayoweza kufanya kazi hapa kwake pia!

Tutaona maendeleo yake.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom