Kutembelea hifadhi ya Mikumi; Je, naweza kodi gari la tours nje ya hifadhi kwa unafuu au ni lazima nikalipie package kwenye kampuni kama mtalii?

Ngariba1

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
1,703
3,454
Wana JF wenzangu,

Naomba ifahamike kuwa kipato changu ni cha kawaida sana ila nina nia ya kutembela hifadhi ya taifa ya Mikumi mwezi Juni ili kufurahia rasimali zetu.

Plan yangu ni kutumia siku moja hifadhini.

Naomba kufahamu yafuatayo;-
1. Je naweza pata malazi aidha ndani au nje ya hifadhi kwa bajeti ya chini ya elfu 40 kwa siku?
2. Je, naweza fika Mikumi nikapata gari la kukodi kunizungusha hifadhini badala ya kwenda kulipia kwa package kwenye makapuni ya tours kama wafanyavyo watalii toka nje ya nchi? Kama ndio, naweza pata gari kwa bei gani?

NB: Nimewahi tembelea Tarangire. Nilienda kwa basi tu, nikashukia eneo la kibaoni. Nikakuta baadhi ya land cruiser zimepaki, wenyeji wakaniambia baadhi wanafanya deiwaka, hawana wateja. Nikaongea na dereva mmoja tukakubaliana 160,000 kwa siku.

Kwanza akanishauri ninunue lunch box then akanipeleka hifadhini nikalipia. Bahati nzuri nilikuta hostel/ lodge zinazomilikiwa na hifadhi zina nafasi. Nikalipia kabisa (20K au 25K kama sijasahau). Tulizunguka sana hifadhini. Around saa 9 akanipeleka Matete picnic nile lunch yangu (kuna mabenchi na vyoo safi). Baadae akanipeleka huko hostel/lodge nikalala, asubuhi akanifata kunitoa hifadhini.

Lodge nilikuta nzuri tu. Self contained, kitanda kizuri, free WiFi, tv.

Kwa kifupi nilitalii kwa gharama ya kawaida sana.

Naomba nijuzwe kuhusu Mikumi.
 
Mkuu wakikujibu unitag hata Mimi niliendaga pale Mikumi Tatizo ni Gari LA kukutembeza hifadhini.nafikiri inakuwa Rahisi Gari ukiitoa Mikumi Au kama Unatoka Dar,Nenda Fika Morogoro Tafuta logde lala,kabla ya Kulala Tafuta Tour Au Gari ya Kukodi asubuhi SAA 2 kurudi Moro Jioni SAA 10.
Nafikiri inaweza Isizidi laki 2.
Sina Uhakika ngoja wajuzi waje.
Asante mkuu. Vipi kuhusu gari?
 
Asante mkuu.
 
Mkuu nenda na iyo hela hadi pale mikumi mjini kula lodge kibao mfano genesis iko pale panaitwa green wale wenye lodge watakupa michongo yote unaweza kupata hata Noah ikakutembeza ndio dili zao pale
Asante sana mkuu. Vipi bei za hizo lodge za hapo Mikumi mjini?
 
Nipo mikumi muda huu kuna hotel na lodge nzuri tu @ 20-50 k per day.unalala huku mjini asubuhi unapelekwa kwa gari ya tour.ni mwendo wa dakika ishirini tu hadi hifadhini.magari ya tour yapo mengi yamezagaa hapa.
 
Mkuu nenda na iyo hela hadi pale mikumi mjini kula lodge kibao mfano genesis iko pale panaitwa green wale wenye lodge watakupa michongo yote unaweza kupata hata Noah ikakutembeza ndio dili zao pale
Well said!!
 
Nipo mikumi muda huu kuna hotel na lodge nzuri tu @ 20-50 k per day.unalala huku mjini asubuhi unapelekwa kwa gari ya tour.ni mwendo wa dakika ishirini tu hadi hifadhini.magari ya tour yapo mengi yamezagaa hapa.
Asante sana mkuu. Nimekupata wakati muafaka. Vipi magari ya tours wanataka bei gani?

Pia nitakuomba majina ya lodge nzuri ulizoziona.
 
Wqtu wa JF matata sana
Kila mtu kafika mikumi na kafanya tour wakiulizwa quotation ili kuwa ngapi hawaji!
Matusi yote ya kiken na kiumeni yanawahusu nyqmbaf zao
 
Wanataka kati ya 160 -200k per day! Hotel nzuri ipo inaitwa vamos,ipo ya kitalii inaitwa tan-swiss.kuna camp ya kitalii inaitwa bastian ,hawa na magari ya tour wanayo hadi ya watu wawili, gest house za mtaani zipo pia,kuna snake park pia huku mikumi mjini.
Asante sana mkuu. Nimekupata wakati muafaka. Vipi magari ya tours wanataka bei gani?

Pia nitakuomba majina ya lodge nzuri ulizoziona.
 
Vamos na tanswiss ni classic kidogo gharama ya kulala ni kwa usd ,sijajua ngapi,camp bastiani kutakufaa kama mchumi,magari yao yapo hapohapo kwa bei nafuu
Wanataka kati ya 160 -200k per day! Hotel nzuri ipo inaitwa vamos,ipo ya kitalii inaitwa tan-swiss.kuna camp ya kitalii inaitwa bastian ,hawa na magari ya tour wanayo hadi ya watu wawili, gest house za mtaani zipo pia,kuna snake park pia huku mikumi mjini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom