Kutembea ukiwa usingizini

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,754
1e7761d954f8c945a4d62ec22c410c19.jpg

Wengi wetu tumeshakumbana na hili tatizo aidha sisi wenyewe ama kupitia ndugu jamaa au hata rafiki, ni tatizo la kiufahamu ambalo husababishwa na matatizo mengine mwilini kama mfumo wa upumuaji kutokuwa sawa, shida kwenye mfumo wa kusukuma damu, madawa msongo wa mawazo uchovu fikra za kufikirika nk

Kiroho pia ina tafsiri yake kwamba hata unapokuwa umelala na hujitambui ufahamu wako huwa active na kufanya mengine yote bila wewe mwenyewe kwenye nafsi ya utashi ukishindwa kutambua lolote.

Kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa hata wale wanga na wachawi wanaochukua watu usiku hutumia formula ya ufahamu kuchukua watu kwenda kuwafanyisha kazi kisha kuwarudisha bila wao kujitambua
70ae5819adbbc390a659e7b1670ca3ec.jpg

Dalili za tatizo hili kwa baadhi huanza utotoni ambalo wala mtoto hana stress nk, na utakuta mtoto anaongea pekeyake bila kutoa sauti anakunjua sura ama kukunja na wakati mwingine kushtuka,(hapa mambo ya kishirikina pia huhusika sana)

Hali hii hutokea masaa takibran matatu baada ya kulala ama kwenye usingizi mzito usiku wa manane na huweza kudumu kuanzia sekunde 30 mpaka nususaa.

Tatizo hili hutofautiana ukubwa, wengine huamka tu kitandani na kuzunguka ndani ya chumba na kurudi kulala! Ila wengine huamka na kama ni mwanafunzi huvaa uniform kabisa na kutoka mpaka nje hata wafanyakazi pia!

Akiwa katika hali hiyo huweza kutembea mpaka hatua kadhaa kisha kurejea ndani na kulala tena huku mwenyewe kwenye hali ya utashi akiwa hajui lolote
Nimekutana na kesi za namna hiyo na watu wakitibiwa kwa kitunguu saumu ama ndimu(hii ni tiba mbadala)kwakuwa kwa hospitali hizi za kizungu hili halina tiba bali hupotea lenyewe au kwa njia ya kutibu chanzo, hasa kama limesababishwa na viashiria vya wazi kama madawa msukumo wa damu stress nk

Kiafrika haishauriwi kabisa kumshtua mtu anayetembea usingizini kwakuwa kile kitendo si utashi wake bali ni command ya ufahamu ambalo haukuwalisiana na nafsi ya utashi (kutenda kwa uamuzi)kinachotakiwa ni kumshika mkono na kumrudisha kitandani taratibu na mara nyingi ufahamu hutii....!

Si wote wanaoamka asubuhi wakiwa wachovu au wamechafuka miguu nk ni matendo ya kishirikina, wengine ni hili tatizo la kutembea usingizini.
 
Kwa baadhi ambao hawana tatizo lingine lolote lakini huwa mahiri na waliobobea kwenye fikra za kufikirika hufikia kutengeneza matendo halisi kwenye ufahamu na kujikuta wanayatekeleza usingizini bila utashi wa nafsi
2012cab92a1a91bfd312924a2ca2dc92.jpg
 
Mimi nimeshawahi kutoka kitandani nikiwa usingizini na kukimbilia mlangoni huku napiga kelele, nikifika mlangoni nazinduka na kujikuta napiga kelele huku niking'ang'ania kufungua mlango na huku nikiwa ninatoka jasho sana, hii imeshanitokea zaidi ya mara mbili nikiwa tayari mtu mzima, mara moja ilinitokea nikiwa kwangu na mara mbili imenitokea ugenini kabisa na kusababisha watu wote waliokuwa wamelala kukurupuka toka usingizini. Siku niliyofanya hivyo nilipokuwa kwangu kuna mtu alikuwa anachungulia dirishani nilipozinduka baada ya kupiga kelele akakimbia sana sikujua ni nani ila kesho asubuhi yake mlinzi wa jirani akaacha kazi na pale dirishani tulikuta maua yakiwa yamekanyangwa kanyagwa,, mpaka leo huwa najiuliza kuna connection gani hapo :D:D:D
 
Hii haina uhusiano kabisa na kutembea ukiwa usingizi, wewe ilikuwa ni michezo ya kichawi au wanga
Matendo ya kutembea usingizini hutendeka kwa mpangio na bila kelele na mhusika huenda na kurudi bila kujitambua na kuendelea na usingizi wake
 
vipi ukiwa umelala then ukatembea usingizi ukalala kwenye karo la choo njee, unajikuta asubuhi hapo? kingine kwenye mtu kuongea akiwa amelala unaweza dadavua zaidi?? kuna siku niliota rasta nyoka. hahaha unatisha
 
Mtu akitembea akiwa usingizini ni psychological disorder[Somnambulism], mara nyingi hutokea zaidi kwa watoto kuliko kwa watu wazima.
Somnambulism inaweza kusababishwa na vitu kama Genetic ya mtu, hofu, matumizi ya baadhi ya dawa, kubadilika kwa mazingira ya kulala, kulala ilhali kibovu kimejaa, n.k.
Hakuna uchawi ama ushirikina unaohusika wakati wa mtu kutembea akiwa amelala.
 
vingine ni hallucinations
Vingine ni mind tricks
Vingine ni michezo ya wanga
Vingine ni shida kwenye akili
 
Mtu akitembea akiwa usingizini ni psychological disorder[Somnambulism], mara nyingi hutokea zaidi kwa watoto kuliko kwa watu wazima.
Somnambulism inaweza kusababishwa na vitu kama Genetic ya mtu, hofu, matumizi ya baadhi ya dawa, kubadilika kwa mazingira ya kulala, kulala ilhali kibovu kimejaa, n.k.
Hakuna uchawi ama ushirikina unaohusika wakati wa mtu kutembea akiwa amelala.
13d59bf1dfc58080d50d680951ebba66.jpg
 
Back
Top Bottom