Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Kutembea na mume wa mtu sio jambo zuri japo wanawake wengi wanaona ni kawaida bila kujua wanajilimbikizia laana itakayofanya maisha yao kuwa magumu mbeleni.

Machozi ya uchungu ya mwanamke mwenzio juu ya mume wake hayafutiki haraka.. Ni kama zigo la kinyesi mgongoni linavutiwa na inzi pekeake.

Huyo mwanaume unaemuona Leo ana mke, Pesa na mali na kuona ndo fursa kwako kumpata kwasababu anajua kujali na anapesa za kutosha kukugharamia.... Ukirudi nyuma miaka 10-15-20 mwanaume huyo huyo alikuwa kama huyu unae mkataa leo .

Unaye muona hajui kuvaa.... Hana pesa za kutosha.. Hana mali kwahiyo hakufai.
Wanaume wengi wanaanzia chini... Jitihada za wake zao zinawafikisha walipo Leo. Heshimu jitihada hizo.

Heshimu siku walizofunga kwa ajili ya waume zao.
Heshimu machozi waliomlilia Mungu awafikishe walipo...
Heshimu muda na jasho walilolitoa kuhakikisha waume zao wanaonekana watu mbele za watu.

Muombe Mungu akupe wa kwako hata kama masikini mpate utajiri pamoja. Na wewe ubige magoti , ulie na kufunga.

Wanawake wengi wanalalamika hawaolewi au Wachumba wanawaacha bila sababu za msingi. Wanasahau zigo LA kinyesi walilobeba mgongoni. Mwanamke piga magoti muombe Mungu akusamehe kwa kumliza mwanamke mwenzio.

Tuwaombee watoto wetu na kuwaonyesha njia iliyo bora. Kuwafundisha dini ili wawe na mahusiano mazuri na Mungu... wasikumbwe na laana hii.

Ewe mama elimisha watoto wako. Ewe dada elimisha wadogo zako.
Tukishirikiana kwapamoja tutayafuta machozi ya wanawake wenzetu.

Credit: Madame S
 
Huu ujumbe ni muhimu sana hasa kipindi hichi ambacho binadamu wanapenda shortcut.
Wakisikia kuna nabii/mtume huyu akikuombea mambo yako yananyooka fasta basi ataacha anaposali atakimbilia kule,akisikia kuna mwingine kaibukia sijui wapi atafunga safari ilimradi apate utajiri,mafanikio ya harakaharaka.
Wengine wanapelekana kwa waganga kusafisha nyota-watu kama hawa wakipata mume wa mtu katu hawamwachii ndo watajua ndo nyota ishan'gaa hivyo,atamchochea jamaa madawa mpaka asahau familia.

Kuna story moja ngoja niwape,miaka ya nyuma kidogo nilikua nimekaa kwenye ka night pub fulan hivi kwenye moja ya mikoa iliyochangamka,hamadi akatokea bint mmoja nilomwachaga kitaa kipindi hicho akinipa shikamoo huku akipiga kigoti kidogo si unajua watu wa kule tena,ila this time nilivyokutana nae aliniita kwa jina na kuniambia fulani mambo huku akitingisha ufunguo wa gari,mi sikujali nilimwitikia poa tuu moyoni nikajisemea bint amekua.

Basi akanijoin kwenye meza tukawa tunapiga mbili tatu,huku tukipiga story mbili tatu,si ndo akafunguka kumbe amepata mdingi fulani mwenye familia yake kamzalisha mtoto mmoja na amemjengea na kumpa na gari,nikamtania we utakua umemloga si bure,na yeye bila iyana akanijibu mjini hapa ukifanikiwa kupata shahawa(sperm) za mwanaume unayemtaka,kuna bibi yupo maeneo ya jirani ukimpelekea tuu kwisha habari yake,maji ataita mma!

Nilimuogopa kiasi kwamba nikienda chooni nilikua nahakikisha kwenye chupa sijaacha kitu,nikija naagiza ingine,mda ulipofika nikamuaga huyo nikasepa zangu.
(Mshana ukipita hapa tunaomba utupe kidogo mahusiano ya manii na ulozi.)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kweli mabinti wengi warembo huitumia hiyo fursa sana,
Sema nao wanawake Mara nyingine huwa chanzo cha migogoro katika ndoa zao hasa wanao fanya kazi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom