African Believer
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 436
- 425
Natumai wanajamvi wenzangu mu wazima,
Lengo la uzi wangu linakwenda sambamba na kichwa cha habari hapo juu.
Sababu kubwa iliyonihimiza kuandika ni kutoweka kwa kasi kwa ladha ya majina yenye asili ya Kiafrika na punde tu hatutasikia tena majina kama vile;
Nwangomale
Mushi, Massawe
Tibyampansha
Mwalukuta
Ambakisye,
Loibanguti
Anyosinsye
Ludelengeja
Mapunda
Makanyanga
Ng'ondwa
Mwakaringa
Mushumbusi
Nchimbi, Amanyisye, Ndomoji, Mwakibuja, Chasimba na mengine mengi yenye kupendeza na yanayoleta positive energy za kweli kabisa pindi yanapotamkwa.
Kwa miaka mingi sasa tangu ujio wa wageni katika maeneo yetu ya Afrika Mashariki hususani Tanzania watu wengi wamekua wakitelekeza majina yao ya kiasili na kukumbatia yale ya kigeni hata kama matamko yake yana maana sawa na majina yetu.
Mtu ataona ni sawa kumwita mtoto wake wa kimakonde jina kwa lugha ya kiaramu (Aramaic) ilhali neno mbadala la kimakonde likiwepo, mtu anamwita mtoto SEIF= UPANGA ila hawezi kumwita mwanae upanga.
Kwa kipindi cha nyuma kasi ya uitaji wa majina hayo ilikuwa si kubwa sana lakini katika zama hizi za kukua kwa sayansi na teknolojia imeongezeka mara dufu.
Mtu hamwiti mwanae jina ni mpaka akagoogle. Utawasikia mastaa wetu kama kina Nasibu Abdul ( akijiita diamond Platnamz) na wanae Tiffany na Prince Nillan, utamsikia Ray Kigosi akimwita kijana wake Jaden na hii ni mifano michache tu. Ninachoweza kusema huu ni utumwa wa kifikra (mind colonization) wa kuhisi kila cha wenzetu ni bora kuliko chetu.