Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,584
Kwa kuwa wasemaji Rasmi wa Serikali wanasema kwamba Msanii Ibrahim Mussa al maarufu kama Roma Mkatoliki hashikiliwi na chombo chochote kile cha dola, na kwa kuwa hao hao watu wa serikali walisema kuwa aliyemtishia kwa Bastola Nape Nnauye naye si mtu wa hivyo vyombo vya dola, basi sisi wananchi wa kawaida tuamini kuwa usalama wetu upo mashakani na tunatakiwa kubadili mtizamo wetu kuhusu mahusiano yetu na vyombo vya dola!
Kwanza kuanzia sasa isiwe kawaida kujiruhusu ama kuruhusu watu wanaokuhusu kukamatwa usiku au kukamatwa mchana na watu waliovaa kiraia hata kama watu hao wanasema kwamba ni polisi. Ni lazima tuwalazimishe "wakamataji" hao kwanza kupitia kwa wenyeviti wetu wa mitaani ili ukamataji wanaotaka kuufanya uwe na kumbukumbu ya ithibati kwamba wakamataji kweli wanatoka kwenye vyombo vya dola.
Ni muhimu watu kuondoa hofu na badala yake watumie simu zao za mikononi kuwapiga picha watu wanaokuja kukamata watu maeneo yetu ili kama wenye dola wanaposema kwamba wakamataji hao hawatoki kwenye vyombo vya dola, basi taswira zao zitumike kuwatafuta kama wahalifu hatari kwenye jamii yetu.
Hapa Iringa kuna kijana alitoka akiwa mzima nyumbani kwake, lakini siku tatu baadaye akapatikana Hospitali ya Mkoa akiwa hoi taabani hajitambui chini ya ulinzi wa Polisi na baadaye kushitakiwa kwa ujambazi na mpaka sasa yuko Magereza kwa kosa hilo. Huyu naye kama Ben Saanane alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA na alikuwa pamoja na Mwangosi siku anauawa.
Shime tuwe kitu kimoja tushikamane kupinga utekaji huu unaotaka kuhalalishwa kwa hoja kwamba vyombo vya dola havihusiki. Vyombo vya dola kama havihusiki kuteka ni lazima vihusike katika kuhakikisha aliyetekwa anapatikana na watekaji wake nao wanapatikana. Kuna wakati tuliambiwa kwamba Jeshi letu la Polisi linaboreshwa, waliokuwa wanasema kwamba linaboreshwa walikuwa wanamaanisha kuboreshwa kwa jeshi hilo ndiyo kukoje?