Kutekwa, Kuteswa, serikali, bunge, wananchi na Dr Ulimboka steven | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutekwa, Kuteswa, serikali, bunge, wananchi na Dr Ulimboka steven

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Jun 30, 2012.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  alitekwa akiwa na baadhi ya watu, maelezo yanasema waliambiwa waondoke na wanamtaka Dr ulimboka. swali je waliokuwepo baada ya kuona purukushani zile hawakupiga kelele, hawakuita watu wa jirani, hawakutafuata ?? Je maelezo ya jumla ambayo nayapata kutoka kwenye media yananiacha na mawazo mengi sana. Naomba yeyote anayemjua aliyekuwepo kabla Ulimboka hajachukuliwa amhoji au ajitokeze atoe maelezo. je ni nani aliyekuwa anapiga simu, ni nani aliyeonyesha wasi wasi wakati yuko kwenye line ya simu??

  Je kwa nini kama ni serikali wanafikiri kumtesa au kumuua Dr ulimboka ni suluhu ya matatizo ya taaluma ya madaktari? Je ni kweli bila ya Dr Ulimboka madaktari hawatadai haki zao. kwa nini serikali haioni kuwa wakati umefika wa kuatatua matatizo ya ukweli badala ya kutishia vitisho ambavyo haivisaidii??

  Kwa nini wananchi wa TZ hawaoni kuwa migomo hii ya madokta inatuathiri sisi wananchi masikini?? Wabunge na ikulu wamejikatia bima zinazo wapeleka Apollo India kwa fedha zetu na kuona uimara na huduma bora wa hospitali zetu hauwahusu. Wabunge na serikali hawana uchungu na huduma za afya TZ kwani wote wanatibiwa India hata wakiwa na mafua na wanalipiwa na fedha za kodi zetu sisi masikini. Ni vigumu sana kusikia mbunge mwenye uchungu wa dhati kufufua huduma za afya au kutetea maslahi ya madakatari kwani kwa wao madaktari wao wako India.

  Bunge limekosa uhalali wa kuwakilisha wananchi, wabunge wanawakilisha matumbo yao na maisha yao huku wakitetea mishahara na posho zao wakiendekeza unafiki kwa kujua watanzania wengi vilaza na hawajapata elimu ya ktosha kuanisha, kuhoji na kutamnbua dhuluma wanayofanyiwa kwa kodi zao.

  Spika amaeshindwa kutumiwa muhimili wa bunge kuhoji kwanini watumishi hawa wa afya wagome mara tatu kwa mwaka bila suluhu huku serikali chini ya JK, Pinda wakiahidi mgomo kutoktokea tena.

  Kama serikali haitumii huduma za nchini wanakopata mishahara, posho na kuishi tusahau kuwa na huduma bora. Read my lips hawa viongozi wakistaafu huwa ni wakwanza kulalamikia huduma mbovu kana kwamaba hawakuwa wakitoa maamuzi ya kuziuwa huduma hizi wakiwa na uwezo wa kupeekwa India na kwingineko.

  Kumteka, kumpiga, kumuuwa Dr Steven Ulimboka hakuwezi kumaliza tatizo la afya nchini zaidi ya kujenga chuki dhidi ya watumishi wa afya na serikali, polisi, wananchi nk kwani joto la hasira kwa kada mbali mbali dhidi ya uongozi wa nchi limekuwa kubwa sana.

  Siamini kama usalama wa taifa, CID, nk ndipo walipofikia. Je uelewa wa viongozi wetu ndivyo ulivyoelekeza? sitaki kuamini ila nashawishika kuwa ndivyo ilivyokuwa.

  Akiwa hai au amekufa hujuma haishindi hata siku moja. Dr Ulimboka alikuwa ni kiongozi tu wa madaktari, angekuwa yeyote yule mgomo usingeepukika. Kumwua au kumtesa ni kushindwa kufikiri na vyombo vya usalama kushindwa kuwa na watu makini.

  Je wanausalama hawakujua mgomo unakuja, mgomo wenyewe ulitangazwa siku nyingi kabla ya kutokea. Serikali hii inawatu wanaotakiwa kuondolewa kwani uwezo wao na wakati wao umepita. Tuilinde tanzania kuliko kulindana, wengi tunahitaji nchi yenye amani na utulivyo inayotumia rasilimali zake kuendeleza watu wake. Tuache ubabe kuongoza nchi.

  Kinepi wa nepi
  Kufa na kuishi ni mapenzi ya Mungu
  Nipo kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu
  Hakuna atakayeishi kama jiwe
  Kaburi ndio mwisho wetu wote hata kwa watesi wetu
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Upeo wa viogozi wetu unapofikia kikomo cha jinsi ya kutatua Matatizo ya jamii! The last alternative is TOUCHER AND INTIMIDATE1. Kupata afaya ya taifa ... Tesa, Toa meno mawili, toa kucha Ishirini ...2. Kupata umeme do as no 1. but this time ongeza dose ... Kata mkono mmoja3. Tatizo kuogezeka kwa bei ...Do as no 1 and 2 but this time .. Ongeza idadi ya Victims fanya 20% of National population... AND where do you end with this ... Syria!!!!!!
   
Loading...