Kutekwa, kukaguliwa na kukamatwa lazima utambulisho kwanza

Barakaeli174

Senior Member
Aug 2, 2015
171
142
Wana JF

Naomba niwasilishe ombi kwa serikali yangu kuwa kuanzia leo wahakikishe kila askari ana kitambulisho ili amridhishe mwananchi kuwa yupo kazini na aje na mjumbe wa eneo husika vinginevyo watanzania hatutakubali kwa vyovyote vile kukamatwa, kukaguliwa au kupelekwa sehem yoyote ile.

Natoa ombi hili ni baada ya kusikia vyombo husika vikisema aliyetekwa hayupo mikononi mwao na waliokuja kumkamata walijitambulisha kuwa wao ni askari, hii inatupa wasiwasi sasa kuwa tutakuwa tunatekwa au ku sachiwa kisa mtu kasema yeye ni askari sasa tuta mwaminije, lazima serikali iweke na iboreshe mfumo wa kukamata na ku sachiwa kwa wananchi wake vinginevyo tutauwawa na watu wengine kwa kuambiwa ni askari, lazima askari akija aonyeshe kitambulisho akiwa na mjumbe na wakija zaidi ya mmoja basi mmoja avae nguo za kazi.

Naomba niwasilishe hili na lifanyiwe kazi maana wakija kwangu wasipokuwa na vitambulisho na wakija bila ya kuwa na mjumbe ndo kwanza najifungia ndani na napiga simu polisi kuwa navamiwa. Asanteni kwa kupokea ombi langu.
 
Back
Top Bottom