"Kutekelezwa ahadi za CUF Zanzibar kunategemea huruma ya Rais wa CCM" - Maalim Seif Sharif Hamad | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Kutekelezwa ahadi za CUF Zanzibar kunategemea huruma ya Rais wa CCM" - Maalim Seif Sharif Hamad

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkeshaji, Jul 12, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema chama chake hakina uwezo wa kutekeleza Ilani yake ya uchaguzi wa Zanzibar 2010 kwa sababu hakina Rais huko na kuwa Rais aliyepo madarakani ni wa CCM.

  Maalim Seif aliyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha Dakika 45 cha ITV. "Katika makubaliano yetu tulikubaliana kuwa chama kitakachoshinda Urais ndicho ambacho Ilani yake itatekelezwa, na CCM ndiyo yenye Rais Zanzibar hivyo kutekelezwa kwa Ilani ya chama chetu kunategemea uungwana wa Rais aliyepo madarakani Dk. Shein" alisema katibu mkuu huyo wa CUF.

  Maalim Seif aliongeza kwa kusema kuwa CUF huko Zanzibar si chama cha upinzani tena bali ni chama tawala hivyo hakiwezi kupingana na serikali ya CCM.
  Hata hivyo Maalim Seif aliipongeza CHADEMA kwa kuibua hoja ya utaratibu wa posho hasa kwa wabunge. "CHADEMA wameibua hoja very strong kuhusu posho, hivyo ni jukumu la CCM kuijibu hoja hiyo kwa kuleta hoja yenye nguvu zaidi ya hiyo na siyo kubeza tu point" alisema Seif.

  Kipindi hicho kilioneshwa jana na kituo cha ITV.
   
 2. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kumbe muungano wao haukulenga kutetea maslahi ya wananchi bali Seif na CCM. Ngoja tusubiri hiyo sympathy.
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mods na nyie na hamisha hamisha yenu! Hii habari ni ya siasa inakuwaje mnaihamishia habari mchanganyiko.
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Alikuwa anatia huruma kweli kwa jinsi alivyokuwa anaongea.
   
 5. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  teh teh teh teh!! anasema CUF chama tawala hakiwez kupingana na CCM kwa hiyo sasa hv wanatekeleza sera moja kwa pamoja ya kumkomoa mwananchi badala ya kumkomboa.
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ccm +cuf=kifo cha halaiki.
   
Loading...