Kutawanyika kwa wayahudi na mwanzo wa Zionism Movement

Darnes 2016

Member
Aug 5, 2018
19
7
IMG_2820.JPG
IMG_2819.JPG


PART 2 : tulipoishia....

Jina “WAYAHUDI” lilitumiwa kwa mara ya kwanza na Mordekai ndani ya Biblia katika kitabu cha Esther kuwatambulisha watu wa kabila la Yuda waliokuwa uhamishoni kwenye nchi za kigeni.

Baada ya Maliki Cyrus The Great kuwaruhusu wayahudi kurudi makwao, sio wote walirejea wengine walibaki. Mnamo mwaka 530BCE Cyrus The Great alikufa vitani alipokuwa akipambana na moja ya makabila massagatae ambayo kwa sasa yanapatikana ndani ya nchi ya Kazakhstan na Uzbekistan. Baada ya kifo chake mwanaye Cambisse Wa Pili alitawala kwa miaka 8 tu hadi 622 BCE. 622 BC Bardiya mjomba wa Cambisse Wa Pili alitawala kwa miezi minane pekee alipouliwa na Darius The Great...

Chini ya Ufalme wa Darius Wa Tatu known biblically as Artashasta, Mwana-mfalme Alexander The Great wa Makedonia aliweza kuumaliza ubabe wa waajemi kwa kumshinda Darius Wa Tatu kwenye vita ya kukata maneno ya Gaugamela 331 BC hivyo kuifanya Makedonia(Ugiriki) kuwa milki kuu ya dunia. Akiwa na umri wa miaka 32 tu Alexander The Great alifariki kwa kuwekewa sumu kwenye kileo na kuacha nyuma yake milki kubwa isiyokuwa na mrithi sahihi. Baada ya mivutano wa hapa na pale wa nani mrithi halali wa Alexander mwishowe milki yake iligawanywa mara kwa majenerali wake wanne: Cassander, Lysimachus, Seleucus Nicator wa Kwanza na Ptolemy Soter wa Kwanza.

1: Cassander alipewa Makedonia
2: Lysimachus akachukua Thrace
3: Ptolemy Soter Wa akachukua Misri na eneo lote la Afrika
4: Seleucus Nicator 1 akapokea eneo lote la Asia, hivyo Yudea ikajikuta kwa mara nyingine tena chini ya mgiriki mwenye asili ya kisiria

Baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Seleucus Nicator 1 na Jenerali mwenzake Lysimachus, Seleucus alijikuta akirule eneo kubwa sana Near East hivyo kumfanya asiyepingika na kusaidia kusambzwa kwa utamaduni wa kigiriki kwa kasi sana kwenye maeneo ya Asia.
Ushindi wa Seleucus Nicator 1 dhidi ya Lysimachus ulisaidia kuenea kwa kasi kwa utamaduni, lugha ya kigiriki Asia. Baada ya kifo chake utamaduni wa kigiriki uliendelea kushamiri kwenye maeneo mengi ya dunia. Miungu yao iliabudiwa almost everywhere ulimwenguni isipokuwa tu kwa wayahudi ambao walikuwa na namna yao ya kuabudu differently.

Mnamo mwaka wa 168 BCE Mfalme wa Nasaba Ya Seleucus ( Seleucid Dynasty), Antiochus Epiphane wa Nne alipiga marufuku kabisa ibada ya kiyahudi. Akaweka sanamu ya Zeus, mungu wa kigiriki ndani ya hekalu la Jerusalem, na kuwaamrisha makuhani kufukiza uvumba kwenye sanamu hiyo.

Mattathias mmoja wa makuhani aliyechukizwa na kitendo hicho cha kufukizia miungu ya kigeni uvumba, alijiinua na kupingana na agizo la mfalme huyo hivyo kujifanya adui wa wagiriki na wayahudi waliojigirikisha au hellenists. Mattathias alimuua hadharani mmoja wa makuhani wenzake alipokuwa akitoa dhabihu mbele ya sanamu hiyo. Mattathias aliukimbia mji yeye pamoja na wanae pamoja na wayahudi kadhaa waliomuunga mkono na kuenda kujificha mashambani. Mwaka mmoja hivi baadae 166 BC, Mattathias alifariki, na mwanaye Judas Maccabee akashika nafasi yake. Judas aliliongoza jeshi unskillful la wayahudi waasi kwenye pambano dhidi ya majeshi ya kigiriki na kisiria na kuweza kuwashinda vibaya sana. Akafanikiwa kuliondoa lile sanamu hekaluni, akaondoa madhabahu za kipagani kijiji kwakijiji, akalazimisha vijana wote wa kiyahudi watahiriwe.
Baada ya ushindi mmoja badala ya mwengine wamakabayo hawa waliweza kuingia Jerusalem kwa ushindi kulitakasa hekalu kwa shangwe, wakamweka Jonathan Maccabee kuwa Kuhani Mkuu. Baada ya kupata uhuru kamili wamakabayo walianza kujitawala chini ya sheria zao wenyewe na kuanzisha Nasaba ya wahasmoni (Hasmonean Dynasty).
Kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya ndugu wawili Aristobulus Wa Pili na Hyrcanus Wa Pili kupamba moto ililazimu msuluhishi kutoka sehemu nyingine. Generali Mroma Pompey ambaye alikuwa kwenye kampeni yake dhidi ya wasiria wa nasaba ya Seleucid aliweza kumtuma naibu wake Marcus Aemilius Scaurus kuchukua milki ya Syria, alipofika Jerusalem ndugu hao wawili walimletea kila mmoja wao zawadi yake ili apate favor ya kuwa Kuhani Mkuu na kiongozi wa Yudea. Aemilius akamfavor Aristobulus na kumfanya kuwa Kuhani Mkuu na Kiongozi wa Yudea. Aemilius aliporudi Damascus Hyrcanus aliasi na kuunda jeshi lake hali iliyopelekea kuzaliwa upya kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na wayahudi wengi kukimbia miji yao. Aristobulus alimshinda vibaya sana mpaka Hyrcanus alipokimbilia kwa wanabateans na kusaini mkataba wa amani na nduguye.
Mwaka 63 BC, Pompey alipofika Syria ndugu wote wawili waliweza tena kutuma kesi zao kwake. Kwa vile Aristobulus alikuwa na misimamo mikali ambayo haikuwafaa hasa Waroma, Pompey akamchagua Hyrcanus nduguye kuwa Kuhani Mkuu ila Ufalme akampa Antipater Mwidumea. Kwa zamu yake pia Aristobulus alipingana na uamuzi wa Pompey na kuanzisha vita mpaka pale aliposhikwa majeshi ya Roma na kupelekwa mateka mjini Roma.


Itaendelea...








Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom