Kutawanyika kwa wayahudi na mwanzo wa Zionism Movement

Darnes 2016

Member
Aug 5, 2018
19
7
IMG_2818.JPG




PART 1 : JEWISH DIASPORA


Ni matumaini yangu mwana JF mwenzangu kuwa u mzima wa afya. Nataka nikuletee kwa ufupi hii mada inayosumbua ulimwengu wa leo


Kwanza tutaanzia mwanzo kbs kwenye zama za Biblia. Waisraeli ni jamii ya watu wa ukoo wa Abraham. Baada ya kutoka Misri utumwani wana hawa wa Abraham waliweza kuwashinda makabila ya Kanaani na hivyo kumiliki maeneo hayo kulingana na Biblia. Kufikia mwaka wa 1000 BCE Waisraeli walikuwa wakiongozwa na mfalme Daudi ambaye baada ya kifo chake mwanaye Sulemani alirithi utawala wake. Sulemani alikufa mnamo 931 BCE. Baada ya kifo chake ndipo ulipotokea mgawanyiko wa makabila kumi na mbili ya Waisraeli ambapo makabila kumi yaliasi na kumfanya kijakazi wa Sulemani, Jeroboam, kuwa mfalme juu yao huku makabila mawili pekee, kabila la Yuda na kabila la Benyamini, yakibaki na mwana wa Sulemani kama mfalme wao.
Hali hii ikapelekea taifa moja kuwa na falme mbili yaani Ufalme wa Kaskazini na Ufalme wa Kusini. Ufalme wa Kaskazini ulifahamika kama Ufalme wa Israeli sababu ndio uliojumuisha makabila mengi huku Ufalme wa Kusini ukiitwa Ufalme wa Yuda sababu Yuda ndio lililokuwa kabila kubwa kwenye falme hii vilevile ndilo lilikuwa kabila la wafalme. Hapa hatutazungumzia sana, wacha tuende straight kwenye mada yetu ya leo.

Kuanzia mwaka wa 732 BCE Ufalme wa Kaskazini ulikuwa chini ya Mfalme Hoshea. Ufalme wa Hoshea ulikumbwa na misukosuko sana hasa pale Mfalme Shalmaneser Wa Tano wa Syria alipoamua kuuzingira Samaria mji mkuu kwa miaka mi3 hadi Hoshea akasalimu amri na kuwa kibaraka wake. Alipoona hali ni ngumu Hoshea aliomba msaada kwa Pharaoh Osorkon Wa Nne wa Misri hali iliyopelekea mnamo 773 BCE Mfalme Tiglath-Pileser wa Tatu wa Syria kuingilia kati kumfunga, na kumpeleka uhamishoni yeye pamoja na baadhi ya Waisraeli. Mnamo 722 BCE, mfalme Sargon Wa Pili wa Syria aliharibu kabisa Ufalme Wa Kaskazini na kuwatoa Waisraeli wengi kwenye miji yao, kuwapeleka uhamishoni na kuwaleta watu wake wasiria kwenye miji ya uhamishoni. Huo ndio uliokuwa mwisho wa Ufalme Wa Kaskazini.


Baada ya kumshinda Pharaoh Necho Wa Pili kwenye ile vita ya kihistoria ya Karkemishi mnamo 605 BCE, Mfalme wa Babylon Nebuchadnezzar wa Pili aliuvamia Ufalme wa Yuda na kumuomba mfalme Jehoiakim asalimu amri. Mfalme alikataa hivyo Nebuchadnezzar Wa Pili akamzingira na kumpeleka kama mateka Babiloni, na kumuweka nduguye, Zedekiah, nafasi yake mnamo 597 BC. Baada ya miaka si mingi ya utawala wake Zedekiah alianza kumuasi mfalme wa Babyloni, hapo ndipo wababiloni walipouzingira Jerusalem, mji mkuu, kuuharibu na kuuchoma moto, pamoja na hekalu lao waliloliona kama kitovu cha imani au uhusiano wao na Mwenyezi-Mungu. Mfalme Zedekiah ambaye alikuwa anajaribu kutoroka alishikwa akatobolewa macho na kupelekwa kifungoni huko Babeli mpaka siku alipokufa. Wababiloni wakahuharibu kabisa Jerusalem na kuwapeleka watu wooote uhamishoni Babiloni isipokuwa wachache ambao waliachwa kama walinzi wa mashamba.

Kufikia hapa tumeweza kiuchache kuona hali zilizowapata hawa watu mpaka wakajikuta wanaishi kwenye ardhi ambazo sio asili yao. Lakini je hii inatosha? Walifikaje sasa kwenye mataifa kama Spain, England, France, Ujerumani ilhali tumeona uhamisho wa kwanza walipelekwa Syria na wapili Babiloni wakati mataifa yote haya kwenye ramani za kisasa yote yapo Bara la Asia? Ok ngoja tuendelee.

Baada ya Mfalme Cyrus The Great(biblical Koreshi) kuishinda Babylon mnamo 538 BC, alitangaza ile ambayo leo inaitwa Edit Of Restoration au Edit Of Cyrus, ambayo iliwapa uhuru wa kurejea makwao wafungwa wote wa kiyahudi na kuwapa uhuru wa kujenga mahali pao pa Ibada tena. Lakini sio wayahudi wote waliorudi kwao, wengi wao ambao walikuwa tayari wameshazoea makazi yao mapya hawakurudi kwenye nchi ya asili yao.

NB: Neno “wayahudi” linatoa mizizi yake kwenye Yuda ambalo lilikuwa moja ya makabila 12 ya Waisraeli hivyo kiukweli haliusiani kabisa na taifa nzima la Israel in total.

Inaendelea....
IMG_2817.JPG


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom