Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,070
9,453
Ndugu zangu Rais Samia hakika amefanikiwa kujenga umoja wa kitaifa, amefanikiwa kuliunganisha Taifa, amefanikiwa kuwaweka watanzania pamoja, amefanikiwa kuishi katika mioyo ya watanzania , Amefanikiwa kupanda mbegu ya Uzalendo katika mioyo ya watanzania

Sasa picha ya Rais Samia inashangiliwa uwanjani Tena katika mchezo mkubwa siyo tu Tanzania Bali katika Bara Zima la Afrika, picha ya Rais Samia inaleta furaha na Tabasamu kwa mashabiki uwanjani, picha ya Rais Samia inakuwa sehemu ya burudani na furaha ya mchezo, mashabiki wote wa timu zote wanafurahi kuona picha ya Rais Samia ikiwa inapepea uwanjani

Hii ni kutokana na kuwa kila mtu na kila shabiki wa mpira anamuona Rais Samia kuwa Ni Rais wake na kiongozi wake, Hakuna mwenye chuki na Rais Samia, Hakuna mwenye kinyongo na mama Samia, hakuna mwenye Hasira na mama Samia. Kila Shabiki akiona picha ya Rais Samia mbele ya uwanja anaona furaha na Tumaini, kila mtu anahisi Rais Samia Ni mshabiki wa timu yake na anajisikia fahari,

Hakika Rais Samia Ni kipenzi Cha watanzania, Ni Tumaini la watanzania, furaha ya watanzania ,kiongozi aliyeteka mioyo ya watanzania, kiongozi anayekubalika na watu wote vijana kwa wazee. Ukifanikiwa kupenya katika mioyo ya wanamichezo maana yake umefanikiwa kukaa katika mioyo ya watanzania maana mchezo wa mpira ndio mchezo unaopendwa na watu wengi Sana Tanzania na unao waunganisha watu bila kujari itikadi zao za kisiasa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Duuh!!
Unashindwa kusifu,kuabudu, kumuimbia na kumchezea Mungu wako,badala yake unamgeuza binadamu mwenzako "mungu"!!!???

Kweli umasikini wa akili na kipato ni vitu vya kutorithisha watoto wetu.
Kwani kuandika ukweli ndio kuabudu. Kwani wewe unafaidika na Nini unapokuwa unapinga pinga kila kitu
 
Ukisikia viongozi wetu wanavyosifiwa huwezi kuamini kama kuna watu hata huduma ya maji safi na salama kwao ni ndoto.

Bado sijajua huu utaratibu wa kuwasifu na kuwasujudia kwa kuwaimba imba na kubabe picha za viongozi wetu ulianza lini, lakini nakumbuka awamu ya nne hii hali haikuwepo.

Nadhani hali ngumu ya maisha na ukosefu wa ajira ndio chanzo cha vijana wengi kuwa na tabia hizi za kichawa.
 

Ukisikia viongozi wetu wanavyosifiwa huwezi kuamini kama kuna watu hata huduma ya maji safi na salama kwao ni ndoto.

Bado sijajua huu utaratibu wa kuwasifu na kuwasujudia kwa kuwaimba imba na kubabe picha za viongozi wetu ulianza lini, lakini nakumbuka awamu ya nne hii hali haikuwepo.

Nadhani hali ngumu ya maisha na ukosefu wa ajira ndio chanzo cha vijana wengi kuwa na tabia hizi za kichawa.
Una miaka mingapi? Au siasa ulianza kufatilia baada ya Lowasa kutaka urais? Awamu kusifiana kulikuwepo vizur tu
 
Back
Top Bottom