Kutapika na Kichefuchefu wakati wa Safari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutapika na Kichefuchefu wakati wa Safari

Discussion in 'JF Doctor' started by Swts, Feb 28, 2012.

 1. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Helow Jf doctorz..
  Shukran kwa michango yenu mizuri ktk jamii.
  Me ningependa kujua,kuhusu tatizo la kichefuchefu na kutapika wakati wa safari either mtu awe amekula kabla ya kupanda gari au hajala,au pia akala katikati ya safari,iwe gari binafsi ama ya umma,eithr safari ndefu au fupi,je kunasababishwa na nini na nini tiba yake..
  Nimejaribu Nosic everytime lakini bado.
   
 2. m

  mkazamjomba Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kabla ya kuanza safari kula phenegan utalala lakini ukija amka huwezi amini utakula kila kitu no kutapika no kichefuchefu mwenzio nlijaribu kwa rafiki yangu amenishukuru kwa tiba hiyo so na wewe jaribu ni serious
   
 3. Swts

  Swts JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 3,072
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  nashukuru sana,ila nlshajaribu kweli,ad nakosa raha ya safari,iv tatizo lnatokana na nini na nitawezaje kuepuka kabisakabisa
   
 4. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kichefu chefu au kutapika wakati uko safarini sio maradhi. Inakuwa hivyo sababu ya mishipa ya fahamu katika masikio yako iko very sesitive kwa changes za posture na altitude. HHamna mazoezi au tiba unayoweza kufanya. Kuna kinga nzuri ambayo umei elezea kuwa umetumia lakini haikukufaa.

  NOSIC. Hii inakupasa uitumie usiku kabla ya siku ya safari ili ikusaidie mwanzoni mwa safari na punde uanzapo safari. Tumia hivi. Vidonge viwili usiku kabla ya safari na kimoja ukisha anza safari. Ukitumia hivi nina uhakika itakusaidia.
   
 5. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 955
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hata mimi ninasumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu tangu nikiwa mtoto hadi hivi sasa nina umri wa miaka 28.Kutapika, Kichefuchefu na Kizunguzungu Kichwa kugonga na hupelekea ninapotapika natapika nyongo.
   
 6. Rjohn

  Rjohn JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 599
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  hata mimi binafs ni tatizo sugu kwangu ,nashukuru kwa ushauri
   
 7. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nionacho ttumbo huchafuka zaidi kwenye rough roads, mfano Nzega-Tabora, Mwanza/Shinyanga-Bariadi, Mwanza-Kigoma/Mbeya, Mbeya-Sumbawanga/Mpanda etc. Katika barabara za lami michafuko ya tumbo hutokea nadra kulinganisha na rough roads.
  Nimekuwa nikisafiri mara nyingi kwa bus na hata nikiwa self driving...akina dada ndio huongoza kwa kulakula hovyo njiani, na hii huwa ni hali mithili ya kujionyesha mbele za wengine. Nimeshuhudia dada 1 nikiwa safarini Nzega akila mishikaki na chipsi na juice, chini ya kilometa 10 akaanza kusimamisha bus akajisitiri.
  NIFANYACHO: Binafsi hujiepusha kula vyakula vyenye vimiminika njiani, badala yake hupendelea kunywa maji, soda na aidha slices za breads. Vyakula hivi hunisaidia sana kwani huwa nasumbuliwa sana na tumbo nje ya safari, na husitirika na matumizi ya aina hii ya vyakula.
   
 8. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  unaposafiri kaa mbele kabisa kwenye gari, hakikisha unaangalia kupitia wind screen na sio vioo vya dirishani. Hii itakuepusha kuona kama miti au majengo yakikimbia na hivyo kusababisha mvurugo wa tumbo. Hakikisha kabla hujaanza safari umekula chakula na epuka kutumia vyakula vyenye sukari nyingi.
   
 9. Mabwepande

  Mabwepande JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni Dalili ya ujauzito
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we unasafiri usiku unakesha kuagana na baba jr wako unategemea usipate kichefuchefu?...
   
 11. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mimba changa
   
 12. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mimi nilikuwa na huo ugonjwa tangu utotoni nilipofika ukubwani nikaacha. Sikuenda kwa Dr wala nini, ninanvyofahamu ni kuwa saa nyingine inasababishwa na position uliyokaa kwenye gari, kama mdau alivyosema kuona miti inakimbia, jengine tafuta siti inaweza kuingia hewa ili kupunguzia hiyo hali.

  Cha zaidi mimi binafsi ni kutokuwa na uzoefu wa kusafiri safiri longroute pia inachangia. Maana mimi niliacha baada ya kuanza kufanya kazi, ambapo pana umbali si chini ya 50 km on daily basis. Chengine avoid safari za mchana zinakuwa mbaya zaidi.
   
Loading...